Hadithi Ya 02: Kuja Kwa Jibriyl عليه السلام Kuwafundisha Waislamu Mambo Ya Dini Yao
HADITHI YA 2
KUJA KWA JIBRIIL عليه السلام KUWAFUNDISHA WAISLAMU MAMBO YA DINI YAO
الحديث الثاني
"مجىء جبريل ليعلم المسلمين أمر دينهم"
عَن
عُمَر رضي اللهُ عنه أَيْضاً قال: بَيْنَما نَحْنُ جُلْوسٌ
عِنْدَ رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ذات يَوْم إذْ طَلَعَ
عَلَيْنَا رَجُلٌ شَدِيدُ بَياضِ الثِّيَاِبِ شَديدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لا
يُرَى عليه أَثَرُ السَّفَرِ ولا يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، حَتى جَلَسَ
إلى النَّبِّي صلى الله عليه وسلم، فأسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إلى رُكْبَتَيْهِ
ووَضَعَ كَفَّيْهِ على فَخِذَيْهِ، وقال: يا محمَّدُ أَخْبرني عَن
الإسلامِ، فقالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم:(( الإسلامُ أَنْ تَشْهَدَ
أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمِّداً رسولُ الله، وتُقِيمَ الصَّلاةَ،
وتُؤتيَ الزَّكاةَ، وتَصُومَ رَمَضان، وتَحُجَّ الْبَيْتَ إن اسْتَطَعتَ
إليه سَبيلاً)). قالَ صَدَقْتَ. فَعَجِبْنا لهُ يَسْأَلُهُ ويُصَدِّقُهُ،
قال : فَأَخْبرني عن الإِيمان. قال: ((أَن تُؤمِنَ باللهِ، وملائِكَتِهِ
وكُتُبِهِ، ورسُلِهِ، واليَوْمِ الآخِرِ، وتُؤمِنَ بالْقَدَرِ خَيْرِهِ
وشَرِّهِ)) قال صدقت. قال : فأخْبرني عَنِ الإحْسانِ. قال:(( أنْ تَعْبُدَ
الله كَأَنَّكَ تَرَاهُ فإنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فإنَّهُ يَرَاك)). قال:
فأَخبرني عَنِ السَّاعةِ، قال: ((ما المَسْؤولُ عنها بأَعْلَمَ مِنَ
السَّائِلِ )). قال: فأخبرني عَنْ أَمَارَتِها، قال:(( أن تَلِدَ الأمَةُ
رَبَّتَها، وأَنْ تَرَى الحُفاةَ العَُراةَ العالَةَ رِعاءَ الشَّاءِ
يَتَطَاوَلُونَ في الْبُنْيانِ )) ثُمَّ انْطَلَقَ، فَلَبِثْتُ مَلِيّاً،
ثُمَّ قال : ((يا عُمَرُ، أَتَدْرِي مَنِ السَّائِلُ؟)) قُلْتُ: اللهُ
ورسُولُهُ أَعلَمُ . قال:(( فإِنَّهُ جِبْرِيلُ أَتاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ
دِينَكُمْ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 2
KUJA KWA JIBRIIL عليه السلام KUWAFUNDISHA WAISLAMU MAMBO YA DINI YAO
Kutoka kwa 'Umar رضى الله عنه ambaye amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa na Mtume صلى الله عليه وسلم ,
hapo alitokea mtu ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na
nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu ya
safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi
aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Mtumeصلى الله عليه وسلم akaweka
magoti yake karibu na magoti yake (Mtume) na akaweka viganja vyake
juu ya mapaja yake kisha akasema; Ewe Muhammad! Niambie kuhusu
Uislamu. Mjumbe wa Allaah صلى الله عليه وسلمalisema:
Uislamu ni kukiri kuwa hakuna mola isipokuwa Allaah na Muhammad
ni Mjumbe wake, kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah, kufunga Ramadhaan na
kwenda kuhiji (Makkah) ukiweza.
(Akasema
yule mtu yaani Jibriyl) Umesema kweli. Tulipigwa na mshangao kwa
kumuuliza kwake Mtume na kumsadikisha. Na akasema
tena: Niambie kuhusu Iymaan. Akasema (Mtume صلى الله عليه وسلم) Ni
kumwamini Mwenyeezi-Mungu, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake na
siku ya Qiyaama, na kuamini ya kuwa kheri na shari zinatoka Kwake
(Allaah سبحانه وتعالى ). (Akasema Jibriyl): Umesema kweli, akasema hebu nielezee kuhusu Ihsaan. Akasema Mtume صلى الله عليه وسلم Ni kumuabudu Allaah سبحانه وتعالى kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona. Akasema (Jibriyl): Niambie kuhusu Qiyaama. Akajibu (Mtume صلى الله عليه وسلم : Muulizwaji si mjuzi kama asivyo vilevile Muulizaji. Kisha akamwambia: Nijulishe alama zake: Akajibu (Mtume صلى الله عليه وسلم):
Kijakazi atazaa bibi yake, na utaona wachunga wenda miguu chini, wenda
uchi (wasio na uwezo wa kumiliki hata mavazi), mafukara (wasiokuwa hata
na sehemu ya kuishi kwa umaskini) wakishindana kujenga majumba ya
fahari. Kisha akaondoka (Jibriyl) na nilitulia kidogo
(nikitafakari). Kisha akasema Mtume صلى الله عليه وسلم :
"Ewe 'Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza? Nikasema:
Allaah na Mjumbe wake wanajua zaidi. Akasema Mtume صلى الله عليه وسلم: Ni Jibriyl, alikuja kuwafundisha dini yenu.
Imesimuliwa na Muslim