Hadiyth Ya 25 - Watu Watatu Watakaokuwa Wagomvi Wa Allaah Siku Ya Kufufuliwa



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  ((قَالَ اللَّهُ ثَلَاثَةٌ أَنَا خَصْمُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ رَجُلٌ أَعْطَى بِي ثُمَّ غَدَرَ وَرَجُلٌ بَاعَ حُرًّا فَأَكَلَ ثَمَنَهُ وَرَجُلٌ اسْتَأْجَرَ أَجِيرًا فَاسْتَوْفَى مِنْهُ وَلَمْ يُعْطِ أَجْرَهُ)) البخاري, أحمد وابن ماجه

Kutoka kwa Abu Hurayrahرضي الله عنه   kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: ((Allaah Amesema: Kuna watu watatu watakaokuwa wagomvi Wangu siku ya kufufuliwa: Mtu aliyetoa neno lake (ahadi) kwa Jina Langu na asitekeleze, mtu aliyemuuza mtu huru na pesa akazitumia; na mtu aliyeajiri mfanyakazi wakakubaliana kisha asimpe ujira wake)) [Al-Bukhaariy, Ahmad na Ibn Maajah]