Al-Hashr (59)

سُورَةُ  الْحَشْر
Al-Hashr (59)

(Imeteremka Madina)



Sura imeanzia kwa kutoa khabari kwamba kila kitu kilioko katika mbingu na ardhi kinamsabihi na kinamtakasa Mwenyezi Mungu na kila kitu ambacho si laiki naye. Na kwamba Yeye ni Mtukufu Mwenye nguvu asiye shindika, ni Mwenye hikima katika kuendesha kwake na kupanga kwake Sharia. Na katika matokeo ya nguvu zake na hikima yake ni yale yanayo simuliwa na Sura hii yaliyo wapata Bani Nnadhiiri, nao ni katika Mayahudi wa Madina. Walikuwa hao walisuluhiana na Mtume s.a.w. baada ya kuhamia Madina kwamba wasiwe dhidi yake wala upande wake. Walipo shindwa Waislamu katika vita vya Uhud, walivunja agano lao wakaungana na Maqureshi dhidi ya Mtume s.a.w. Hapo ndipo akenda akwazunguka katika ngome zao ambazo walidhani wenyewe kuwa zitawalinda, na zisiweze kuwalinda. Tena ndio akawafukuza kutoka Madina. Kisha Sura inaeleza hukumu ya mali yaliyo patikana kwa maadui bila ya kupigana vita wala kukimbilia kwa farasi na kadhaalika. Ikataja kuwa hayo ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, na mafakiri katika wakimbizi walio tolewa kwenye nyumba zao na mali yao. Kisha Sura ikasimulia khabari za Ansari, Waislamu wa Madina, na fadhila yao, na jinsi walivyo kuwa wanawafadhilisha Wahajiri, wakimbizi, kuliko nafsi zao, ijapo kuwa wao wenyewe wana haja ya hivyo wanavyo toa. Na Sura inataka macho yaangalie zile ahadi za wanaafiki kwa Bani Nnadhiiri, na kauli yao waliyo sema: Pindi mkitolewa, nasi tutatoka pamoja nanyi! Na mkipigwa vita tutakusaidieni! Basi Sura imeufedhehi uwongo wao huo, udanganyifu wao katika hayo.
Kisha Sura ikamalizikia kwa kuwakumbusha Waumini kwa yatakikanayo wawe nayo, nayo ni kumcha Mwenyezi Mungu, na kujiwekea akiba kwa siku zijazo za karibuni na za mbali. Na wala wasiwe kama wale walio mpuuza Mwenyezi Mungu, naye akawasahaulisha nafsi zao.
Na ikakhitimisha Sura kwa kubainisha hadhi ya Qur'ani na ubora wa taathira yake. Hayo ni hivyo kwa sababu aliye iteremsha ni Yeye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye Mwenye Asmau-l-H'usna, Majina Mazuri kabisa.

 


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١﴾

1. Kinamsabbih Allaah Pekee (kila) kilichokuweko katika mbingu na ardhi Naye ndiye Al-’Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).

هُوَ الَّذِي أَخْرَجَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِن دِيَارِهِمْ لِأَوَّلِ الْحَشْرِ ۚ مَا ظَنَنتُمْ أَن يَخْرُجُوا ۖ وَظَنُّوا أَنَّهُم مَّانِعَتُهُمْ حُصُونُهُم مِّنَ اللَّـهِ فَأَتَاهُمُ اللَّـهُ مِنْ حَيْثُ لَمْ يَحْتَسِبُوا ۖ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ ۚ يُخْرِبُونَ بُيُوتَهُم بِأَيْدِيهِمْ وَأَيْدِي الْمُؤْمِنِينَ فَاعْتَبِرُوا يَا أُولِي الْأَبْصَارِ ﴿٢﴾

2. Yeye Ndiye Aliyewatoa wale waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu (Mayahudi wa Banu An-Nadhwiyr) kutoka majumbani mwao katika mkusanyiko wa kwanza. Hamkudhania kwamba watatoka, nao wakadhani kwamba ngome zao zitawakinga dhidi ya Allaah. (Lakini)  Allaah Akawafikia (kwa adhabu Yake) kutoka (mahali) wasipotazamia, na Akatia kiwewe katika nyoyo zao. Wanaziharibu nyumba zao kwa mikono yao na (kwa) mikono ya Waumini, basi zingatieni, enyi wenye uoni.  

وَلَوْلَا أَن كَتَبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمُ الْجَلَاءَ لَعَذَّبَهُمْ فِي الدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابُ النَّارِ ﴿٣﴾

3. Na lau kama Allaah Asingeliwaandikia kufukuzwa nchi, bila shaka Angeliwaadhibu duniani, na Aakhirah watapata adhabu ya Moto.

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ شَاقُّوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۖ وَمَن يُشَاقِّ اللَّـهَ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٤﴾

4. Hivyo kwa kuwa wao wamempinga Allaah na Rasuli Wake. Na yeyote (yule) anayempinga Allaah, basi hakika Allaah ni Mkali wa kuakibu.

مَا قَطَعْتُم مِّن لِّينَةٍ أَوْ تَرَكْتُمُوهَا قَائِمَةً عَلَىٰ أُصُولِهَا فَبِإِذْنِ اللَّـهِ وَلِيُخْزِيَ الْفَاسِقِينَ ﴿٥﴾

5. Hamkukata mtende wowote (ule, katika mitende yao mliyoikata) au mliouacha umesimama juu ya shina lake, basi ni kwa idhini ya Allaah na ili Awahizi mafasiki.

وَمَا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ مِنْهُمْ فَمَا أَوْجَفْتُمْ عَلَيْهِ مِنْ خَيْلٍ وَلَا رِكَابٍ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يُسَلِّطُ رُسُلَهُ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٦﴾

6. Na ngawira yeyote ile Aliyoleta Allaah kwa Rasuli Wake kutoka kwao; basi hamkuyaendea mbio kwa farasi na wala ngamia (vitani), lakini Allaah Huwasalitishia Rasuli Wake kwa Amtakaye. Na Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Mweza).

مَّا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ مِنْ أَهْلِ الْقُرَىٰ فَلِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنكُمْ ۚ وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٧﴾

7. Ngawira Aliyoyatoa Allaah kwa Rasuli Wake kutoka kwa watu wa vijiji, basi ni za Allaah na Rasuli na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na msafiri aliyeharibikiwa, ili yasiwe yanarudiarudia (kinyang’anyiro) baina ya matajiri miongoni mwenu. Na lolote (lile) analokupeni Rasuli (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) basi lichukueni, na (lolote lile) analokukatazeni, basi acheni. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuakibu.


لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ ﴿٨﴾

8. (Na pia liweko fungu la ngawira) Kwa mafuqara Muhaajiriyn ambao wametolewa kutoka majumbani mwao na (zikataifishwa) mali zao wanatafuta fadhila na Radhi kutoka kwa Allaah na wanamnusuru Allaah (kwa kuinusuru Dini Yake) na Rasuli Wake (kwa kumuunga mkono); hao ndio wakweli.

وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٩﴾

9. Na wale waliokuwa na makazi (Madiynah) na wakawa na iymaan kabla yao, wanawapenda wale waliohajiri kwao, na wala hawapati kuhisi haja yoyote (choyo, wivu, husda) vifuani mwao kwa yale waliyopewa (Muhaajiriyn), na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wana ufukara. Na yeyote (yule) anayeepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٠﴾

10. Na wale waliokuja baada yao (wenye) kusema: “Rabb (Mola) wetu! Tughufurie na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo (ya chuki, uadui, uhasidi, n.k.) kwa wale walioamini; Rabb wetu! Hakika Wewe ni Rauwfur-Rahiym (Mwenye huruma mno - Mwenye kurehemu).


أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ نَافَقُوا يَقُولُونَ لِإِخْوَانِهِمُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَئِنْ أُخْرِجْتُمْ لَنَخْرُجَنَّ مَعَكُمْ وَلَا نُطِيعُ فِيكُمْ أَحَدًا أَبَدًا وَإِن قُوتِلْتُمْ لَنَنصُرَنَّكُمْ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿١١﴾

11. Je, huwaoni wale walionafiki wanawaambia ndugu zao waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu (Mayahudi): “Mkitolewa (mkifukuzwa kutoka Madiynah), bila shaka nasi tutatoka pamoja nanyi, na wala hatutomtii yeyote abadani dhidi yenu. Na mkipigwa vita, bila shaka tutakunusuruni.” Na Allaah Anashuhudia kwamba wao bila shaka ni waongo.

لَئِنْ أُخْرِجُوا لَا يَخْرُجُونَ مَعَهُمْ وَلَئِن قُوتِلُوا لَا يَنصُرُونَهُمْ وَلَئِن نَّصَرُوهُمْ لَيُوَلُّنَّ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ ﴿١٢﴾

12. Wakitolewa, hawatotoka pamoja nao, na wakipigwa vita, hawatowanusuru, na hata wakiwanusuru, bila shaka watageukia mbali migongo (wakimbie), kisha hawatonusuriwa.

لَأَنتُمْ أَشَدُّ رَهْبَةً فِي صُدُورِهِم مِّنَ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ ﴿١٣﴾

13. Bila shaka nyinyi (Waumini) ni tisho kubwa katika vifua vyao kuliko (wanavyomuogopa) Allaah. Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasiofahamu.

لَا يُقَاتِلُونَكُمْ جَمِيعًا إِلَّا فِي قُرًى مُّحَصَّنَةٍ أَوْ مِن وَرَاءِ جُدُرٍ ۚ بَأْسُهُم بَيْنَهُمْ شَدِيدٌ ۚ تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ ﴿١٤﴾

14. Hawatopigana nanyi wote (kwa mkusanyiko) isipokuwa katika miji iliyohifadhiwa kwa ngome, au kutoka nyuma ya kuta. Vita vyao baina yao ni vikali. Utawadhania wako pamoja, kumbe nyoyo zao ziko mbalimbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasiotia akilini.

كَمَثَلِ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ قَرِيبًا ۖ ذَاقُوا وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٥﴾

15. (Hali yao hawa Mayahudi wa Banu Nadhwiyr) Ni kama mfano wa wale (Mayahudi wa Banu Qaynuqaa) walio kabla yao hivi karibuni tu walionja matokeo ya ubaya wa mambo yao, na watapata adhabu iumizayo.

كَمَثَلِ الشَّيْطَانِ إِذْ قَالَ لِلْإِنسَانِ اكْفُرْ فَلَمَّا كَفَرَ قَالَ إِنِّي بَرِيءٌ مِّنكَ إِنِّي أَخَافُ اللَّـهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦﴾

16. (Wanafiki ni) Kama mfano wa shaytwaan anapomwambia insani: “Kufuru!” Alipokufuru; (shaytwaan) husema: “Hakika mimi siko pamoja nawe! Mimi namuogopa Allaah Rabb (Mola) wa walimwengu.”

فَكَانَ عَاقِبَتَهُمَا أَنَّهُمَا فِي النَّارِ خَالِدَيْنِ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الظَّالِمِينَ ﴿١٧﴾

17. Basi yakawa matokeo yao wote wawili ni kwamba watakuwa Motoni wote wawili ni wenye kudumu humo. Na hiyo ndio jazaa ya madhalimu.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَلْتَنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ لِغَدٍ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١٨﴾

18. Enyi mlioamini! Mcheni Allaah, na nafsi itazame imetanguliza nini kwa ajili ya kesho (Siku ya Qiyaamah), na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Khabiyr (Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana) kwa myatendayo.

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ نَسُوا اللَّـهَ فَأَنسَاهُمْ أَنفُسَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١٩﴾

19. Na wala msiwe kama wale waliomsahau Allaah, Naye (Allaah) Akawasahaulisha nafsi zao, hao ndio mafasiki.

لَا يَسْتَوِي أَصْحَابُ النَّارِ وَأَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۚ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمُ الْفَائِزُونَ ﴿٢٠﴾

20. Hawalingani sawa watu wa Motoni na watu wa Jannah, watu wa Jannah ndio wenye kufuzu.

لَوْ أَنزَلْنَا هَـٰذَا الْقُرْآنَ عَلَىٰ جَبَلٍ لَّرَأَيْتَهُ خَاشِعًا مُّتَصَدِّعًا مِّنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ ۚ وَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١﴾

21. Lau Tungeliiteremsha hii Qur-aan juu ya jabali, ungeliliona linanyenyekea (na) lenye kupasukapasuka kutokana na khofu ya Allaah. Na hiyo ni mifano Tunawapigia watu ili wapate kutafakari.

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿٢٢﴾

22. Yeye ni Allaah, Ambaye hakuna ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye. ‘Aalimu (Mjuzi) wa ghayb na dhahiri, Yeye Ndiye Ar-Rahmaanur-Rahiym (Mwingi wa Rahmah - Mwenye kurehemu).

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٢٣﴾

23. Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye, Al-Malik (Mfalme), Al-Qudduws (Mtakatifu), As-Salaam (Mwenye amani), Al-Muumin (Mwenye kusadikisha), Al-Muhaymin (Mwenye kutawala na kuendesha), Al-‘Aziyz (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima), Al-Jabbaar (Asiyeshindwa kufanya Atakalo), Al-Mutakabbir (Mwenye kustahiki kiburi), Subhaana Allaah! (Utakasifu ni wa Allaah!) kwa yale yote wanayomshirikisha (nayo).

هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٤﴾

24. Yeye Ndiye Allaah, Al-Khaaliq (Muumbaji), Al-Baariu (Mwanzishi viumbe bila kasoro), Al-Muswawwir (Mtengeneza sura), Ana Majina Mazuri kabisa, kinamsabbih Pekee (kila) kilichokuweko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com