Al-A’laa (87)


سُورَةُ  الأَعْلى
Al-A’laa (87)

(Imeteremka Makka)

Sura hii imeanza kwa kumtakasa huyo aliye umba vitu vyote, na akavifanya vyote sawa kwa kuvishughulikia, na akakadiria kila kitu kwa kinavyo silihi, basi akakiongoza kifikilie hivyo. Na akaotesha malisho ya wanyama, na khalafu akayafanya makavu yaliyo ingia weusi. Kisha Aya zikatoa khabari kwamba Mwenyezi Mungu atamsomesha Mtume wake Qur'ani, naye ataihifadhi, wala hatosahau chochote katika hivyo ila apende Mwenyezi Mungu. Na atamsahilishia kwa wepesi. Kisha Sura inamuamrisha Mtume akumbushe kwa Qur'ani apate kukumbuka mwenye kuogopa, na ajitenge na ukumbusho huyo mwovu atakaye ingia kwenye Moto mkubwa. Na Aya zimetilia mkazo kwamba uwokovu ni wa mwenye kujisafisha, na akalikumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali. Na Sura imekhitimisha kwa kubaini kwamba yaliyo kuja humu yamethibiti katika Vitabu vya zamani, Vitabu vya Ibrahimu na Musa.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى ﴿١﴾

1.      Sabbih Jina la Rabb (Mola) wako Aliyetukuka.

الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ ﴿٢﴾

2. Ambaye Ameumba na Akasawazisha.

وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ ﴿٣﴾

3. Na Ambaye Amekadiria na Akaongoza.

وَالَّذِي أَخْرَجَ الْمَرْعَىٰ ﴿٤﴾

4. Na Ambaye Ametoa malisho.

فَجَعَلَهُ غُثَاءً أَحْوَىٰ ﴿٥﴾

5. Kisha Akayajaalia makavu, meusi.

سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰ ﴿٦﴾

6. Tutakusomesha (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) basi hutoisahau.

إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۚ إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ ﴿٧﴾

7. Isipokuwa yale Ayatakayo Allaah; hakika Yeye Anayajua ya jahara na yale yanayofichikana.

وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٨﴾

8. “Na Tutakuwepesishia kwa (yale yaliyo) mepesi”

فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ الذِّكْرَىٰ ﴿٩﴾

9. Basi kumbusha (waidhi) ikiwa kunafaa ukumbusho (mawaidha).

سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَىٰ ﴿١٠﴾

10. Atakumbuka (na kuwaidhika) yule anayeogopa.

وَيَتَجَنَّبُهَا الْأَشْقَى ﴿١١﴾

11. Na atajiepusha nayo fedhuli.

الَّذِي يَصْلَى النَّارَ الْكُبْرَىٰ ﴿١٢﴾

12. Ambaye atauingia Moto mkubwa na kuungua.

ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ ﴿١٣﴾

13. Kisha hatokufa humo, na wala hatokuwa hai.

قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّىٰ ﴿١٤﴾

14. Hakika Amefaulu yule anayejitakasa.

وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّىٰ ﴿١٥﴾

15. Na akadhukuru Jina la Rabb (Mola) wake na akaswali.

بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿١٦﴾

16. Bali mnafadhilisha uhai wa dunia.


وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ﴿١٧﴾

17. Na (uhai wa) Aakhirah ni bora na ni wa kubaki.

إِنَّ هَـٰذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ ﴿١٨﴾

18. Hakika haya bila shaka yamo katika swahifa za awali.

صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ ﴿١٩﴾

19. Swahifa za Ibraahiym na Muwsaa.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com