005 - Hadiyth Ya 5: Kuvunjia Kiapo Kitendo Kiovu Kwa Kilicho Chema


عَنْ أبي طريفٍ عَدِيَّ بْنَ حَاتِمٍ  الطَّائي (رضي الله عنه) قال: سَمِعْتُ رسول اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم) يَقُولُ: ((مَنْ حَلَفَ عَلَى يَمِينٍ ثُمَّ رَأَى أَتْقَى لِلَّهِ مِنْهَا فَلْيَأْتِ التَّقْوَى))  رواه مسلم  
 
Imepokelewa kutoka kwa Abu Twariyf ‘Adiyy bin Haatim (رضي الله عنه) amesema: “Nimemsikia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Atakayeapa yamini [kufanya jambo] kisha akaona linalomridhisha zaidi Allaah kuliko aliloliapia, basi amche Allaah kwa kufanya linalomridhisha Allaah)).[1]
 
Mafunzo Na Hidaaya:
 
  1. Aayah na Hadiyth nyingi zimesisitiza kuwajibika kuwa na taqwa, [Al-Ahzaab 33: 70, At-Tawbah 9: 119, Al-Maidah 5: 35].
 
  1. Mwenye kuazimia kufanya maasi asiyatende japokuwa ameyaapia kutenda.
 
  1. Kuruhusika kuvunja kiapo na kafara zake. [Rejea Hadiyth namba 92, 102, 124].
 
 لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٨٩﴾
 
Allaah Hatokuhisabuni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakuhisabuni kwa (kuvunja) viapo mlivyoapa kwa niyyah mlioifunga thabiti. Basi kafara yake (ya kuvunja viapo hivi) ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu, au kuwavisha nguo, au kuacha huru mtumwa. Lakini asiyeweza kupata (moja katika hayo), basi afunge Swawm siku tatu. Hiyo ndio kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na hifadhini viapo vyenu (msiape kisha hamtimizi). Hivyo ndivyo Allaah Anavokubainishieni Aayah Zake mpate kushukuru[2]
 
  1. Umuhimu wa kupata radhi za Allaah (سبحانه وتعالى) kuliko jambo jengine lolote lile.
 
 
 



[1]  Muslim.
[2]  Al-Maaidah (5: 89).