An-Naswir


سُورَةُ  النَّصْر
An-Naswr (110)

(Imeteremka Madina)




Sura hii imemtaka Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. ukija msaada wa Mwenyezi Mungu na ushindi, na akaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi kwa kutua mambo yake na kutukuka neno lake na kumkamilishia Mwenyezi Mungu, basi amtakase Mola wake Mlezi kwa kumsifu, na amtakase na kila lisio mwelekea, na amwombe msamaha kwa nafsi yake na kwa Waumini, kwa sababu hakika Yeye ni Mwingi wa kukubali toba za waja wake, na anasamehe makosa.

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّـهِ وَالْفَتْحُ ﴿١﴾

1. Itakapokuja Nusura ya Allaah na ushindi.

وَرَأَيْتَ النَّاسَ يَدْخُلُونَ فِي دِينِ اللَّـهِ أَفْوَاجًا ﴿٢﴾

2. Na utawaona watu wanaingia katika Dini ya Allaah makundi makundi.

فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُ ۚ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا ﴿٣﴾

3. Basi sabbih kwa Sifa njema za Rabb (Mola) wako na muombe maghfirah; hakika Yeye daima ni Tawwaabaa (Mwingi wa kupokea tawbah).





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com