Ash-Sharh (94)


سُورَةُ  الشَّرْح
Ash-Sharh (94)

(Imeteremka Makka)


Inathibitisha Sura hii kwamba Mwenyezi Mungu ameukunjua moyo wa Nabii wake, na akaufanya ndipo pahala pa kuteremkia siri na ilimu, na akaondoa matatizo yaliyo kuwa yakimthakilisha mgongo wake, nayo ni katika mizigo ya kazi ya Da'wa, yaani Wito. Na akalikutanisha jina lake Mwenyezi Mungu na jina lake Mtume katika asli ya Imani na alama za Dini. Kisha Aya hizi zikataja sunna ya Mwenyezi Mungu ya kuambatisha mepesi na mazito, dhiki na faraji, na zikamtaka Mtume kila anapo pata nafasi kutokana na kutenda kheri, atende kheri nyengine, na afanye lengo lake ni Mola wake Mlezi, kwani Yeye ni Muweza wa kumsaidia. 


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ ﴿١﴾

1. Je, kwani Hatukukupanulia kifua chako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)?

وَوَضَعْنَا عَنكَ وِزْرَكَ ﴿٢﴾

2. Na Tukakuondolea mzigo wako (wa dhambi)?

الَّذِي أَنقَضَ ظَهْرَكَ ﴿٣﴾

3. Ambao ulithakilisha mgongo wako?

وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ ﴿٤﴾

4. Na Tukanyanyulia juu utajo wako (ukawa mwenye kusifika mno)?

فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٥﴾

5. Basi hakika pamoja na ugumu (dhiki), kuna mepesi (faraja).


إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٦﴾

6. Hakika pamoja na ugumu (dhiki), kuna mepesi (faraja).

فَإِذَا فَرَغْتَ فَانصَبْ ﴿٧﴾

7. Basi utakapokuwa faragha (umemaliza shughuli za wajibu), jishughulishe (na ‘ibaadah).

وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَارْغَب ﴿٨﴾

8. Na kwa Rabb (Mola) wako elemeza raghba (zako).





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com