Al-Mumtahinah (60)


سُورَةُ  الْمُمْتُحِنَة
Al-Mumtahinah (60)

(Imeteremka Madina)

Sura hii imeanza kwa kuwakataza Waumini wasiwafanye urafiki washirikina, ambao ni maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zao wao, kwa kushikilia kwao ukafiri, na kumtoa Mtume wa Mwenyezi Mungu na Waumini kwenye nyumba zao Makka. Na ikaashiria kwamba uadui wa watu hawa kwa Waumini, ulio fichikana, hauwachi kudhihiri pale wanapo wakuta na wakapata nguvu juu yao.
Kisha Sura ikaingia kubainisha ruwaza njema ya Ibrahim na walio kuwa pamoja naye katika kujitenga na washirikina, na hayo waliyo kuwa wakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, wakitangaza uadui wao kwao mpaka wamuamini Mwenyezi Mungu peke yake. Hayo yanaonyesha kuwa huo ndio mwendo wa wanao taraji kukutana na Mwenyezi Mungu, na wanaogopa adhabu yake.
Kisha ikabainisha makhusiano yepi yanafaa kuwa nayo na wasio kuwa Waislamu, na yepi hayafai. Ama wale ambao hawatupigi vita katika Dini wala hawasaidii dhidi yetu, basi ni waajibu  wetu kuwafanyia wema, na kuwafanyia haki. Ama hao wanao tupiga vita katika Dini, na wakasaidia katika kututoa kwenye nyumba zetu na miji yetu, hao, basi, ndio Mwenyezi Mungu anatukataza kuwafanyia hisani na kukhusiana nao.
Kisha Sura ikabainisha hukumu ya Waumini wanawake walio hamia kwenye mji wa Kiislamu, na wakawaacha waume zao wa kishirikina; na hukumu ya wanawake wa kishirikina ambao  waume zao Waislamu wamehama, na hao wanawake wakaachwa katika mji wa shirki.
Na ikafuatiliza kueleza kutoa ut'iifu wanawake, kwa walivyo mtolea Mtume s.a.w. Kisha Sura ikakhitimisha, kama ilivyo anza, kwa kukataza kuwafanya urafiki maadui walio kasirikiwa na Mwenyezi Mungu, ili kuthibitisha hukumu iliyo kwisha tolewa mwanzo wake, na ikaitilia nguvu katika kuthibitisha kwake.

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُم مِّنَ الْحَقِّ يُخْرِجُونَ الرَّسُولَ وَإِيَّاكُمْ ۙ أَن تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ رَبِّكُمْ إِن كُنتُمْ خَرَجْتُمْ جِهَادًا فِي سَبِيلِي وَابْتِغَاءَ مَرْضَاتِي ۚ تُسِرُّونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَأَنَا أَعْلَمُ بِمَا أَخْفَيْتُمْ وَمَا أَعْلَنتُمْ ۚ وَمَن يَفْعَلْهُ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿١﴾

1. Enyi mlioamini! Msimchukue adui Wangu na adui wenu (kuwa) marafiki wandani mkiwapelekea (siri za mikakati) kwa mapenzi, na hali wamekwishakanusha haki iliyokujieni. Wanamtoa kwa kumfukuza Rasuli (pamoja) na nyinyi kwa vile mmemuamini Allaah Rabb (Mola) wenu; ikiwa mmetoka (kwa ajili ya) jihaad katika njia Yangu na kutafuta Radhi Zangu. Mnawapa siri kwa mapenzi, na (hali) Mimi Najua zaidi yale (yote) mnayoyaficha na yale (yote) mnayoyadhihirisha. Na yeyote (yule) atakayefanya hivyo miongoni mwenu, basi kwa yakini amepotea njia ya sawa.

إِن يَثْقَفُوكُمْ يَكُونُوا لَكُمْ أَعْدَاءً وَيَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ وَأَلْسِنَتَهُم بِالسُّوءِ وَوَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ ﴿٢﴾

2. Wakikudhibitini (wakakushindeni) watakuwa ni maadui kwenu, na watakunyosheeni mikono yao na ndimi zao kwa uovu, na watatamani lau mngekufuru.

لَن تَنفَعَكُمْ أَرْحَامُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ ۚ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَفْصِلُ بَيْنَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٣﴾

3. Hawatokufaeni (kitu) jamaa zenu wa uhusiano wa damu, na wala auladi wenu Siku ya Qiyaamah (Allaah) Atapambanua baina yenu; na Allaah kwa yale myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona).

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَا أَمْلِكُ لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۖ رَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٤﴾

4. Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, walipowaambia watu wao: “Hakika sisi tumejitenga nanyi na yale (yote) mnayoyaabudu badala ya Allaah, tunakukanusheni, na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha abadi mpaka mumuamini Allaah Pekee.” Isipokuwa kauli ya Ibraahiym kwa baba yake: “Nitakuombea maghfirah, na wala sikumilikii chochote kile mbele ya Allaah. Rabb (Mola) wetu! Tumetawakali Kwako, na Kwako Tunarudia kutubia, na Kwako ni mahali pa kuishia mwishoni.

رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا وَاغْفِرْ لَنَا رَبَّنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٥﴾

5. “Rabb (Mola) wetu! Usitujaalie (kuwa) mtihani kwa wale waliokufuru, na Tughufurie Rabb wetu; hakika Wewe ni Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima   - Mwenye hikmah wa yote daima).”

لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِيهِمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ ۚ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿٦﴾

6. Kwa yakini imekuwa kwenu kigezo kizuri katika (mwenendo) wao kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho. Na yeyote atakayekengeuka, basi hakika Allaah Ndiye Al-Ghaniyyul-Hamiyd (Mkwasi - Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote daima).

عَسَى اللَّـهُ أَن يَجْعَلَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ الَّذِينَ عَادَيْتُم مِّنْهُم مَّوَدَّةً ۚ وَاللَّـهُ قَدِيرٌ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٧﴾

7. Huenda Allaah Akajaalia mapenzi baina yenu na baina ya wale mlio na uaduwi nao; na Allaah ni Qadiyr (Muweza wa yote daima), na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).

لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ ﴿٨﴾

8. Allaah Hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita katika Dini, na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu. Hakika Allaah Anapenda wafanyao uadilifu.

إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَىٰ إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٩﴾

9. Hakika Allaah Anakukatazeni tu kuhusu wale waliokupigeni vita katika Dini, na wakakutoeni kutoka majumbani mwenu, na wakasaidiana (kwenye) kukutoeni (ndio Anakataza) kufanya urafiki nao. Na yeyote atakayewafanya (hao) marafiki, basi hao ndio madhalimu.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ ۖ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ ۖ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ ۖ وَآتُوهُم مَّا أَنفَقُوا ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ أَن تَنكِحُوهُنَّ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۚ وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ وَاسْأَلُوا مَا أَنفَقْتُمْ وَلْيَسْأَلُوا مَا أَنفَقُوا ۚ ذَٰلِكُمْ حُكْمُ اللَّـهِ ۖ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿١٠﴾

10. Enyi mlioamini! Wanapokujieni Waumini wa kike Muhaajiraat basi wajaribuni. Allaah Anajua zaidi iymaan zao. Na mkiwatambua kuwa ni Waumini basi msiwarejeshe (Makkah) kwa makafiri. Wao si (wake) halaal kwao (hao makafiri), na wala wao si (waume) halaal kwao. Na wapeni (makafiri mahari) waliyotoa. Na wala si dhambi kufunga nao nikaah mkiwapa mahari yao. Na wala msiwaweke wanawake makafiri katika fungamano la ndoa; na takeni (kurudishiwa) mlichotoa (katika mahari), nao watake walichotoa. Hiyo ndio hukumu ya Allaah, Anahukumu baina yenu, na Allaah ni ‘Aliymun-Hakim (Mjuzi daima wa yote - Mwenye hikmah wa yote daima).

وَإِن فَاتَكُمْ شَيْءٌ مِّنْ أَزْوَاجِكُمْ إِلَى الْكُفَّارِ فَعَاقَبْتُمْ فَآتُوا الَّذِينَ ذَهَبَتْ أَزْوَاجُهُم مِّثْلَ مَا أَنفَقُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي أَنتُم بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿١١﴾

11. Na kama mkimpoteza yeyote kati ya wake zenu (akitoroka na) kurejea kwa makafiri (bila ya kurudisha mahari), ikatokea kuwa (mmekwenda vitani dhidi yao na mkapata ngawira), basi wapeni wale walioondokewa na wake zao mfano wa walichotoa (mahari); na mcheni Allaah Ambaye nyinyi Kwake mnamuamini.

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا جَاءَكَ الْمُؤْمِنَاتُ يُبَايِعْنَكَ عَلَىٰ أَن لَّا يُشْرِكْنَ بِاللَّـهِ شَيْئًا وَلَا يَسْرِقْنَ وَلَا يَزْنِينَ وَلَا يَقْتُلْنَ أَوْلَادَهُنَّ وَلَا يَأْتِينَ بِبُهْتَانٍ يَفْتَرِينَهُ بَيْنَ أَيْدِيهِنَّ وَأَرْجُلِهِنَّ وَلَا يَعْصِينَكَ فِي مَعْرُوفٍ ۙ فَبَايِعْهُنَّ وَاسْتَغْفِرْ لَهُنَّ اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢﴾

12. Ee Nabii! Wakikujia Waumini wa kike wanafungamana nawe ahadi kwamba hawatomshirikisha Allaah na chochote, na wala hawatoiba, na wala hawatozini, na wala hawataua auladi wao, na wala hawatoleta kashfa walioizua baina ya mikono yao na miguu yao, na wala hawatakuasi katika (jambo) jema; basi fungamana nao ahadi, na waombee maghfirah kwa Allaah. Hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ قَدْ يَئِسُوا مِنَ الْآخِرَةِ كَمَا يَئِسَ الْكُفَّارُ مِنْ أَصْحَابِ الْقُبُورِ ﴿١٣﴾

13. Enyi mlioamini! Msiwafanye marafiki watu ambao Allaah Amewaghadhibikia, wamekwishakata tamaa na Aakhirah kama walivyokwishakata tamaa makafiri kati ya watu wa makaburini.


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com