112. SURAT AL-IKHLAS'


سُورَةُ  الإِخْلاَص
Al-Ikhlaasw (112)

(Imeteremka Makka)

Nabii s.a.w. aliulizwa khabari za Mola wake Mlezi, akaamrishwa katika Sura hii ajibu kwamba Yeye ni Mwenye kukusanya sifa zote za ukamilifu, ni Mmoja, wa Pekee, Mwenye kukusudiwa daima katika haja, Mwenye kujitosha hamhitajii yeyote mwenginewe, ametakasika na kuwa na mfano, hakuzaa wala hakuzaliwa, wala hana  mwenzie katika viumbe vyake.



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾
1. Sema: “Yeye ni Allaahu Ahad (Mmoja Pekee).

اللَّـهُ الصَّمَدُ ﴿٢﴾

2. “Allaah ni Asw-Swamad (Aliyekamilika sifa za kila aina ya utukufu Wake, Mwenye kukusudiwa kwa haja zote).

لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ ﴿٣﴾

3. “Hakuzaa na wala Hakuzaliwa.


وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ ﴿٤﴾

4. “Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana (au kulingana) Naye.”

waliopotea.


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com