Al-Kaafiruwn (109)

سُورَةُ  الْكَافِرُون
 Al-Kaafiruwn (109)

(Imeteremka Makka)

 
Katika Sura hii Mwenyezi Mungu anamuamrisha Mtume wake s.a.w. awakatishe tamaa makafiri katika juhudi zao za kutaka kusikilizana na Mtume katika wito wake wa Haki, kwa kuwa yeye ni mwenye kubakia vile vile juu ya ibada ya Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu ila Yeye, na wao wabakie kuiabudu miungu yao ambayo haifidi chochote katika Haki, wao wawe na dini yao walio ifuata baba zao, na yeye na Dini yake aliyo mridhia Mwenyezi Mungu aifuate.

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ ﴿١﴾

1. Sema: “Enyi makafiri!

لَا أَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَ ﴿٢﴾

2. “Siabudu yale mnayoyaabudu.

وَلَا أَنتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ ﴿٣﴾

3. “Na wala nyinyi si wenye kuabudu Yule Ninayemwabudu.

وَلَا أَنَا عَابِدٌ مَّا عَبَدتُّمْ ﴿٤﴾

4. “Na mimi si mwenye kuabudu yale mnayoabudu.

وَلَا أَنتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ ﴿٥﴾

5. “Na wala nyinyi si wenye kuabudu Yule Ninayemwabudu.

لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ ﴿٦﴾

6. “Nyinyi mna dini yenu; nami nina Dini yangu.”

 


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com