Al-Jaathiyah: 45

الْجاثِيَة
Al-Jaathiyah: 45

(Imeteremka Makka)


Imeanzia Sura hii kwa harufi mbili katika harufi za Alifbete, na ikafuatiliza kwa kubainisha kuwa kuteremshwa Qur'ani kumetokana na Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu Mwenye hikima. Kisha ikazitaja dalili za uumbaji na za kiakili kuthibitisha itikadi ya Imani na kuitia watu waifuate. Hali kadhaalika imekusanya wito kwa wenye kukadhibisha Ishara. Kisha ikaingia kuzihisabu neema za Mwenyezi Mungu na fadhila zake kwa waja wake; na ikawataka Waumini wawasamehe makafiri wanao kanya. Kwani Mwenyezi Mungu peke yake ndiye wa kumlipa kila mtu kwa alilo litenda. Kisha Sura baada ya hayo ikazungumzia vipi Mwenyezi Mungu alivyo wafadhili Wana wa Israili kwa kuwapa neema nyingi, na khitilafu zilizo zuka baina yao ambazo Mwenyezi Mungu atazitolea hukumu Siku ya Kiyama. Kisha ikaingia kufarikisha baina ya walio fuata Haki na walio fuata matamanio, wakakanya kufufuliwa, na wakapinga Ishara  za uweza kwa kutaka wafufuliwe baba zao! Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuhuisha, na ndiye Mwenye kufisha. Yeye ana ufalme wa kila kitu. Na siku watakapo kusanywa wapotovu kila nafsi itaitwa ikapokee kitabu chake. Hapo watafuzu Waumini na watakemewa walio takabari. Sura tena inarejea hadithi ya kule kuikataa kwao Saa ya Kiyama, na kuzikadhibisha Ishara zinazo ionyesha; na vile Mwenyezi Mungu atavyo wasahau wao kama wao walivyo isahau hii Siku. Na ikabainisha kuwa makaazi yao ni Motoni kwa kule kuzikejeli kwao Ishara za Mwenyezi Mungu na kudanganyika kwao na dunia. Na Sura imekhitimisha kwa kumsifu Muumba mbingu na ardhi, Mwenye utukufu kote humo, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
حم﴿١﴾
1. Haa Miym.


تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ﴿٢﴾
2. Ni uteremsho wa Kitabu (Qur-aan) kutoka kwa Allaah Al-’Aziyul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye hikmah wa yote).


إِنَّ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّلْمُؤْمِنِينَ﴿٣﴾
3. Hakika katika mbingu na ardhi bila shaka (ziko) Aayaat (ishara, dalili, zingatio) kwa Waumini.


وَفِي خَلْقِكُمْ وَمَا يَبُثُّ مِن دَابَّةٍ آيَاتٌ لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ﴿٤﴾
4. Na katika kuumbwa kwenu, na Anaoyatawanya (ulimwenguni) kati ya viumbe vinavyotembea ni Aayaat (hoja, dalili) kwa watu wenye yakini.


وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن رِّزْقٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ آيَاتٌ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴿٥﴾
5. Na mapishano ya usiku na mchana, na Anayoteremsha Allaah kutoka mbinguni katika riziki, Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake, na kugeukageuka pepo (za Rahmah) ni Aayaat (hoja, dalili) kwa watu wanaotia akilini.


تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۖ فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَ اللَّـهِ وَآيَاتِهِ يُؤْمِنُونَ﴿٦﴾
6. Hizo ni Aayaat za Allaah Tunakusomea kwa haki. Basi hadiyth gani wataziamini baada ya (kupuuza hadiyth za) Allaah na Aayaat Zake?


وَيْلٌ لِّكُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ﴿٧﴾
7.  Ole kwa kila mzushi muongo, mtendaji mno dhambi.


يَسْمَعُ آيَاتِ اللَّـهِ تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ثُمَّ يُصِرُّ مُسْتَكْبِرًا كَأَن لَّمْ يَسْمَعْهَا ۖ فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٨﴾
8. Anazisikia Aayaat za Allaah akisomewa, kisha anang’ang’ana kuwa mwenye kutakabari kama kwamba hakuzisikia. Basi mbashirie adhabu iumizayo.


وَإِذَا عَلِمَ مِنْ آيَاتِنَا شَيْئًا اتَّخَذَهَا هُزُوًا ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ﴿٩﴾
9. Na anapojua chochote katika Aayaat Zetu huzichukulia mzaha. Hao watapata adhabu ya kudhalilisha.


مِّن وَرَائِهِمْ جَهَنَّمُ ۖ وَلَا يُغْنِي عَنْهُم مَّا كَسَبُوا شَيْئًا وَلَا مَا اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْلِيَاءَ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿١٠﴾
10. Nyuma yao (Moto wa) Jahannam, na wala hayatowafaa kitu yale waliyoyachuma na wala wale waliowafanya (kama) watawalia badala ya Allaah, na watapata adhabu kuu.


هَـٰذَا هُدًى ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ لَهُمْ عَذَابٌ مِّن رِّجْزٍ أَلِيمٌ﴿١١﴾
11. Hii (Qur-aan) ni Mwongozo Na wale waliokanusha Aayaat za Rabb (Mola) wao watapata adhabu ya kufadhaika iumizayo.


اللَّـهُ الَّذِي سَخَّرَ لَكُمُ الْبَحْرَ لِتَجْرِيَ الْفُلْكُ فِيهِ بِأَمْرِهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴿١٢﴾
12. Allaah Ambaye Amekutiishieni bahari ili zipite merikebu humo kwa amri Yake, na ili mtafute katika fadhila Zake na ili mpate kushukuru.


وَسَخَّرَ لَكُم مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مِّنْهُ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿١٣﴾
13. Na Amekutiishieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini vyote humo. Hakika katika hayo bila shaka (kuna) Aayaat (hoja, dalili, ishara) kwa watu wanaotafakari.


قُل لِّلَّذِينَ آمَنُوا يَغْفِرُوا لِلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ أَيَّامَ اللَّـهِ لِيَجْزِيَ قَوْمًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿١٤﴾
14. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa wale walioamini wawasamehe wale wasiozitaraji Siku za Allaah ili Awalipe watu kutokana na yale waliyokuwa wakiyachuma.


مَنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا ۖ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ﴿١٥﴾
15. Yeyote atendaye jema, basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kufanya uovu, basi ni dhidi yake, kisha kwa Rabb (Mola) wenu mtarejeshwa.


وَلَقَدْ آتَيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ﴿١٦﴾
16. Na kwa yakini Tuliwapa wana wa Israaiyl Kitabu na hukumu na unabii, na Tukawaruzuku katika vizuri, na Tukawafadhilisha juu ya walimwengu.


وَآتَيْنَاهُم بَيِّنَاتٍ مِّنَ الْأَمْرِ ۖ فَمَا اخْتَلَفُوا إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿١٧﴾
17. Na Tukawapa hoja bayana ya mambo (ya Dini). Basi hawakukhitilafiana isipokuwa baada ya kuwajia elimu kwa uhusuda baina yao. Hakika Rabb (Mola) wako Atahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale waliyokuwa wakikhitilafiana nayo.


ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٍ مِّنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ﴿١٨﴾
18. Kisha Tukakuweka (wewe ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya shariy’ah ya mambo (ya Dini), basi ifuate, na wala usifuate hawaa za wale wasiojua.


إِنَّهُمْ لَن يُغْنُوا عَنكَ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۚ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۖ وَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُتَّقِينَ﴿١٩﴾
19. Hakika wao hawatokufaa chochote mbele ya Allaah. Na hakika madhalimu ni marafiki wandani na wasaidizi wao kwa wao. Na Allaah ni Waliyyu (Mlinzi, Msaidizi) wa wenye taqwa.


هَـٰذَا بَصَائِرُ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ﴿٢٠﴾
20. Hii (Qur-aan) ni utambuzi kwa watu na ni Mwongozo na Rahmah kwa watu wenye yakini.


أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ اجْتَرَحُوا السَّيِّئَاتِ أَن نَّجْعَلَهُمْ كَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَوَاءً مَّحْيَاهُمْ وَمَمَاتُهُمْ ۚ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ﴿٢١﴾
21. Je, wanadhania wale waliochuma maovu kwamba Tutawafanya sawa na wale walioamini na wakatenda mema (na pia) sawasawa uhai wao na kufa kwao? Uovu ulioje wanaouhukumu.


وَخَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَلِتُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿٢٢﴾
22. Na Allaah Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, na ili ilipwe kila nafsi kwa yale iliyoyachuma, nao hawatodhulumiwa.


أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ وَأَضَلَّهُ اللَّـهُ عَلَىٰ عِلْمٍ وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمْعِهِ وَقَلْبِهِ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِ غِشَاوَةً فَمَن يَهْدِيهِ مِن بَعْدِ اللَّـهِ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿٢٣﴾
23. Je, umemuona yule aliyejichukulia hawaa zake kuwa ndio ilaah (muabudiwa) wake, na Allaah Akampotoa juu ya kuwa na elimu na Akapiga mhuri juu ya masikio yake na moyo wake; na Akaweka kifuniko juu ya macho yake? Basi nani atamuongoa baada ya Allaah? Je, basi hamkumbuki?


وَقَالُوا مَا هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا يُهْلِكُنَا إِلَّا الدَّهْرُ ۚ وَمَا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ﴿٢٤﴾
24. Na wakasema: “Huu si chochote isipokuwa ni uhai wetu wa dunia, tunakufa na tunahuika, na hakuna cha kutuangamiza isipokuwa dahari.” Na wala hawana kwayo ujuzi wowote, ila wao wanadhania tu.


وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ مَّا كَانَ حُجَّتَهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا ائْتُوا بِآبَائِنَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٢٥﴾
25. Na wanaposomewa Aayaat Zetu bayana haikuwa hoja yao isipokuwa kusema: “Tuleteeni mababu zetu mkiwa nyinyi ni wakweli.”


قُلِ اللَّـهُ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يَجْمَعُكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٢٦﴾
26. Sema: “Allaah Anakuhuisheni, kisha Atakufisheni, kisha Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah isiyo na shaka ndani yake, lakini watu wengi hawajui.


وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يَوْمَئِذٍ يَخْسَرُ الْمُبْطِلُونَ﴿٢٧﴾
27. Na ni wa Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Na Siku itakayosimama Saa (Qiyaamah), watakhasirika Siku hiyo wabatilifu.


وَتَرَىٰ كُلَّ أُمَّةٍ جَاثِيَةً ۚ كُلُّ أُمَّةٍ تُدْعَىٰ إِلَىٰ كِتَابِهَا الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٨﴾
28. Na utaona kila ummah wenye kupiga magoti (kwa kunyenyekea). Kila ummah utaitwa kwenye rekodi yake (ya matendo): “Leo mtalipwa yale mliyokuwa mkiyatenda.”


هَـٰذَا كِتَابُنَا يَنطِقُ عَلَيْكُم بِالْحَقِّ ۚ إِنَّا كُنَّا نَسْتَنسِخُ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٩﴾
29. “Hii rekodi Yetu inatamka (kushuhudia) juu yenu kwa haki. Hakika Sisi Tulikuwa Tunaamuru yaandikwe yale mliyokuwa mkiyatenda.”


فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُدْخِلُهُمْ رَبُّهُمْ فِي رَحْمَتِهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ﴿٣٠﴾
30. Basi wale walioamini na wakatenda mema, Rabb (Mola) wao Atawaingiza katika Rahmah Yake. Huko ndiko kufuzu bayana.


وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا أَفَلَمْ تَكُنْ آيَاتِي تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَاسْتَكْبَرْتُمْ وَكُنتُمْ قَوْمًا مُّجْرِمِينَ﴿٣١﴾
31. Ama wale waliokufuru (wataambiwa): “Je, kwani hazikuwa Aayaat Zangu zikisomwa kwenu, mkatakabari na mkawa watu wahalifu?”


وَإِذَا قِيلَ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَالسَّاعَةُ لَا رَيْبَ فِيهَا قُلْتُم مَّا نَدْرِي مَا السَّاعَةُ إِن نَّظُنُّ إِلَّا ظَنًّا وَمَا نَحْنُ بِمُسْتَيْقِنِينَ﴿٣٢﴾
32. Na inaposemwa: “Hakika ahadi ya Allaah ni haki, na Saa (Qiyaamah kinakuja) haina shaka ndani yake” Mlisema: “Hatujui Saa ni nini! Hatudhanii isipokuwa ni dhana tupu, nasi sio wenye kuyakinika kikweli.”


وَبَدَا لَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا عَمِلُوا وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٣٣﴾
33. Na yatawafichukia maovu waliyoyatenda, na yatawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.


وَقِيلَ الْيَوْمَ نَنسَاكُمْ كَمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا وَمَأْوَاكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّاصِرِينَ﴿٣٤﴾
34. Na itasemwa: “Leo Tunakusahauni kama mlivyosahau kukutana na Siku yenu hii, na makazi yenu ni Motoni na wala hamna yeyote mwenye kunusuru.


ذَٰلِكُم بِأَنَّكُمُ اتَّخَذْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ هُزُوًا وَغَرَّتْكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۚ فَالْيَوْمَ لَا يُخْرَجُونَ مِنْهَا وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ﴿٣٥﴾
35. Hivyo ni kwa sababu nyinyi mlizichukulia mzaha Aayaat za Allaah, na ukakudanganyeni uhai wa dunia.” Basi leo hawatotolewa humo, na wala hawataachiliwa kuomba kuridhisha (kwa Allaah).


فَلِلَّـهِ الْحَمْدُ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَرَبِّ الْأَرْضِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٣٦﴾
36. Basi Himidi zote Anastahiki Allaah Rabb (Mola) wa mbingu na Rabb wa ardhi, Rabb wa walimwengu.


وَلَهُ الْكِبْرِيَاءُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٣٧﴾
37. Na Al-Kibriyaau (Adhama, Utukufu, Ujalali) ni Wake Pekee mbinguni na ardhini; Naye Ndiye Al-’Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye hikmah wa yote).




Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com