Hadiyth Ya 26 - Allah Ana Haki Ya Kuogopwa Zaidi Ya Watu

  
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لَا يَحْقِرَنَّ أَحَدُكُمْ نَفْسَهُ إِذَا رَأَى أَمْرًا لِلَّهِ فِيهِ مَقَالٌ أَنْ يَقُولَ فِيهِ فَيُقَالُ لَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَا مَنَعَكَ أَنْ تَقُولَ فِيهِ فَيَقُولُ رَبِّ خَشِيتُ النَّاسَ قَالَ فَأَنَا أَحَقُّ أَنْ تَخْشَى)) مسند أحمد

Kutoka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriyy ambaye amesema: Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: ((Asijidhalilishe mmoja wenu atakapoona jambo la Allaah ambalo angalisema kitu juu yake na asiseme, kwa hivyo Allaah  سبحانه وتعالىHumwambia siku ya Qiyaamah: Kipi kilichokuzuia usiseme kitu kuhusu jambo kadhaa wa kadhaa? Husema: Nikiogopa watu. Kisha Mola Atasema: Ni mimi Ndiye ninayepaswa kuogopwa)) [Musnad Ahmad]