Hadiyth Ya 09 - Subira Katika Msiba Wa Kwanza Jaza Yake Pepo

 

عَنْ أَبِي أُمَامَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((يَقُولُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ يَا ابْنَ آدَمَ: إن  َصَبَرْتَ وَاحْتَسَبْتَ عِنْدَ الصَّدْمَةِ الْأُولَى لَمْ أَرْضَ لَكَ ثَوابا دون الْجَنَّةِ)) ابن ماجه

Kutoka kwa Abu Umaamah ambaye amesema: Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: ((Allaah  عَزَّ وَجَلَّ Anasema: Ewe Mwana wa Aadam, utakaposubiri na ukategemea (thawabu) katika  msiba wa mwanzo, sitoridhia kwako ujira chini (ila) ya Pepo)) [Ibn Maajah]