Al-Balad (90)


سُورَةُ الْبَلَد
Al-Balad (90)

(Imeteremka Makka)


Mwenyezi Mungu anaapa kwa mji mtakatifu wa Makka, mji wa kuzaliwa Muhammad s.a.w. na ndipo alipo kulia na akapapenda, na pia anaapa kwa mzazi na anacho kizaa, kwani kwa hao ndio jinsi inahifadhika na maamrisho yanabakia, na ya kwamba mtu ameumbwa kwa mashaka na shida na taabu. Tena anabainisha kwamba mtu anadanganyika kwa kudhani kuwa uweza wake haushindiki, na kwamba yeye ana mali mengi anayo yatumia kuridhisha matamanio yake na pumbao lake. Kisha Subhanahu akazitaja neema alizo mneemesha mwanaadamu na kumsahilishia njia za uwongofu na za kupitia milimani, ili awe katika watu wa Peponi, watu wa mkono wa kulia, na aikimbie njia ya kumpelekea kuwa katika watu wa kushoto ambako itawatumbukiza Motoni na kufungiwa milango.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

لَا أُقْسِمُ بِهَـٰذَا الْبَلَدِ ﴿١﴾

1. Naapa kwa mji huu (wa Makkah).

وَأَنتَ حِلٌّ بِهَـٰذَا الْبَلَدِ ﴿٢﴾

2. Nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uko huru na vikwazo vya mji huu.

وَوَالِدٍ وَمَا وَلَدَ ﴿٣﴾

3. Na (Naapa kwa) mzazi na alichokizaa.

لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي كَبَدٍ ﴿٤﴾

4. Kwa yakini Tumemuumba insani katika tabu.

أَيَحْسَبُ أَن لَّن يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَدٌ ﴿٥﴾

5. Je, anadhani kwamba hakuna yeyote atakayemweza?

يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالًا لُّبَدًا ﴿٦﴾

6. Anasema (kwa kujigamba): “Nimeangamiza mali tele.”

أَيَحْسَبُ أَن لَّمْ يَرَهُ أَحَدٌ ﴿٧﴾

7. Anadhani kwamba hakuna yeyote anayemuona?

أَلَمْ نَجْعَل لَّهُ عَيْنَيْنِ ﴿٨﴾

8. Je, kwani Hatukumjaalia macho mawili?

وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ ﴿٩﴾

9. Na lisani na midomo miwili?

وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ ﴿١٠﴾

10. Na Tukamuongoza (kumbainishia) njia mbili (ya haki ya upotofu)?

فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ ﴿١١﴾

11. Basi hakujaribu kukata njia ya mnyanyuko mkali (mashaka).


وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ ﴿١٢﴾

12. Na nini kitakachokujulisha nini hiyo njia ya mnyanyuko mkali (mashaka).

فَكُّ رَقَبَةٍ ﴿١٣﴾

13. (Ni) Kuacha huru mtumwa.

أَوْ إِطْعَامٌ فِي يَوْمٍ ذِي مَسْغَبَةٍ ﴿١٤﴾

14. Au kulisha katika siku ya ukame.

يَتِيمًا ذَا مَقْرَبَةٍ ﴿١٥﴾

15. Yatima aliyekuwa jamaa wa karibu.

أَوْ مِسْكِينًا ذَا مَتْرَبَةٍ ﴿١٦﴾

16. Au maskini aliye na shida mno (hohe hahe).

ثُمَّ كَانَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا بِالْمَرْحَمَةِ ﴿١٧﴾

17. Kisha akawa miongoni mwa wale walioamini, na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.

أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ ﴿١٨﴾

18. Hao ndio watu wa kuliani..

وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا هُمْ أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ ﴿١٩﴾

19. Na wale waliozikanusha Aayaat Zetu wao ndio watu wa kushotoni.


20. Juu yao ni Moto uliofungiwa (kila upande).





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com