Al-Fat-h: 48

  الْفَتْح
Al-Fat-h: 48

(Imeteremka Madina)


Imeanzia mwanzo wake Sura hii kwa kutaja Ushindi ulio wazi, alio msahilishia Mwenyezi Mungu Mtume wake, na imeelezea athari zake kubwa katika kueneza Uislamu na kuwatukuza Waislamu, na kuziimarisha nyoyo za Waumini ili wazidi Imani, na kuadhibiwa kwa wanaafiki na washirikina, kwa shaka shaka zao juu ya nusura ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake. Na imetaja kuwa Mtume Muhammad s.a.w. ametumwa kuwa ni mwenye kushuhudia, na mwenye kubashiria, ili ithibiti Imani ya Mwenyezi Mungu. Tena Sura ikaingia kueleza kusimulia kuungwa mkono Mtume na watu wa kweli wa kutimiza ahadi, na ikabainisha uwongo wa udhuru walio toa walio kwenda kinyume na Mtume wasitoke naye kwenda pambana na maadui, na ambao walibaki nyuma kwa kudhania kwao kuwa Mwenyezi Mungu hatampa nusura Mtume, na ikaeleza kuwa kutaka kwao kutoka naye ni kwa sababu ya kupata ngawira.
Tena Sura imebainisha kuwa watakuja takiwa kupigana na kaumu wakali na wenye nguvu, na kwamba hapana makosa kuacha kwenda vitani kwa udhuru wa kweli. Kama ilivyo weka wazi ukubwa wa kheri alizo waahidi Mwenyezi Mungu wale alio furahi nao katika kumuunga mkono Mtume s.a.w. kwa Ridhwani. Imezungumzia juu ya kukimbia kwao makafiri na kushindwa kwao walipo pigana na Waumini, ikaeleza hikima ya Mwenyezi Mungu kuwazuia makafiri wasiwapige Waumini, na kuwazuia Waumini wasiwapige makafiri wakati wa kutekwa Makka. Na mazungumzo yakamalizikia kwa kubainisha kwamba Mwenyezi Mungu ameitimiza ndoto aliyo iota Mtume wake ya kuingia katika Msikiti Mtakatifu, na kwamba Muhammad na walio amini pamoja naye ni wakali kwa makafiri lakini ni wapole, wanaoneana huruma wao kwa wao. Na ikabainisha alama za kuwajuulisha Waumini, na sifa zao katika Taurati na sifa zao katika Injili, na Mwenyezi Mungu kawaahidi walio amini na wakatenda mema msamaha mkunjufu, na ujira mkubwa.



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا﴿١﴾
1. Hakika Tumekupa ushindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم ambao ni) ushindi bayana.


لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَيَهْدِيَكَ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا﴿٢﴾
2. Ili Allaah Akughufurie yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayofuatia; na Akutimizie neema Yake juu yako na Akuongoze njia iliyonyooka.


وَيَنصُرَكَ اللَّـهُ نَصْرًا عَزِيزًا﴿٣﴾
3. Na Akunusuru Allaah nusura yenye nguvu kabisa.


هُوَ الَّذِي أَنزَلَ السَّكِينَةَ فِي قُلُوبِ الْمُؤْمِنِينَ لِيَزْدَادُوا إِيمَانًا مَّعَ إِيمَانِهِمْ ۗ وَلِلَّـهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا﴿٤﴾
4. Yeye Ndiye Aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili Awazidishie iymaan pamoja na iymaan zao. Na ni ya Allaah Pekee majeshi ya mbinguni na ardhini, na Allaah ni daima ‘Aliyman-Hakiymaa (Mjuzi wa yote - Mwenye hikmah wa yote).


لِّيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عِندَ اللَّـهِ فَوْزًا عَظِيمًا﴿٥﴾
5. (Na) Ili Awaingize Waumini wa kiume na Waumini wa kike Jannaat zipitazao chini yake mito, ni wenye kudumu humo, na Awafutie maovu yao; na limekuwa hilo mbele ya Allaah,  ni kufuzu adhimu.


وَيُعَذِّبَ الْمُنَافِقِينَ وَالْمُنَافِقَاتِ وَالْمُشْرِكِينَ وَالْمُشْرِكَاتِ الظَّانِّينَ بِاللَّـهِ ظَنَّ السَّوْءِ ۚ عَلَيْهِمْ دَائِرَةُ السَّوْءِ ۖ وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ وَلَعَنَهُمْ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا﴿٦﴾
6. Na Awaadhibu wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike na washirikina wa kiume na washirikina wa kike, wanaomdhania Allaah dhana ovu.  Utawafikia mgeuko mbaya; na Allaah Awaghadhibikie, na Awalaani, na Awaandalie (Moto wa) Jahannam, na paovu palioje mahali pa kuishia.


وَلِلَّـهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا﴿٧﴾
7. Na ni ya Allaah Pekee majeshi la mbingu na ardhi, na Allaah daima ni ‘Aziyzan-Hakiymaa (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye hikmah wa yote).


إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا﴿٨﴾
8.  Hakika Sisi Tumekutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ukiwa mwenye kushuhudia, mwenye kubashiri na mwonyaji.


لِّتُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُعَزِّرُوهُ وَتُوَقِّرُوهُ وَتُسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا﴿٩﴾
9. Ili (nyinyi watu) mumwamini Allaah na Rasuli Wake, na mumsaidie kwa taadhima na mumheshimu (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na mumsabbih (Allaah سبحانه وتعالى) asubuhi na jioni.


إِنَّ الَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ اللَّـهَ يَدُ اللَّـهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ ۚ فَمَن نَّكَثَ فَإِنَّمَا يَنكُثُ عَلَىٰ نَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِمَا عَاهَدَ عَلَيْهُ اللَّـهَ فَسَيُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا﴿١٠﴾
10. Hakika wale waliofungamana ahadi ya utiifu nawe, hakika hapana ila wanafungamana ahadi ya utiifu na Allaah, Mkono wa Allaah Uko juu ya mikono yao. Basi atakayevunja (fungamano), hakika hapana ila anavunja dhidi ya nafsi yake. Na yeyote atimizaye yale aliyomuahidi Allaah - basi Atampa ujira adhimu.


سَيَقُولُ لَكَ الْمُخَلَّفُونَ مِنَ الْأَعْرَابِ شَغَلَتْنَا أَمْوَالُنَا وَأَهْلُونَا فَاسْتَغْفِرْ لَنَا ۚ يَقُولُونَ بِأَلْسِنَتِهِم مَّا لَيْسَ فِي قُلُوبِهِمْ ۚ قُلْ فَمَن يَمْلِكُ لَكُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا إِنْ أَرَادَ بِكُمْ ضَرًّا أَوْ أَرَادَ بِكُمْ نَفْعًا ۚ بَلْ كَانَ اللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا﴿١١﴾
11. Watakuambia mabedui waliobaki nyuma: “Zimetushughulisha mali zetu na ahli zetu, basi tuombee maghfirah.” Wanasema kwa ndimi zao yasiyokuweko nyoyoni mwao. Sema: “Nani basi atayekuwa na uwezo kuzuia chochote kwa Allaah Akikusudia kukudhuruni au Akikusudia kukunufaisheni. Bali Allaah daima ni Khabiyraa (Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyofichikana) kwa yale myatendayo.


بَلْ ظَنَنتُمْ أَن لَّن يَنقَلِبَ الرَّسُولُ وَالْمُؤْمِنُونَ إِلَىٰ أَهْلِيهِمْ أَبَدًا وَزُيِّنَ ذَٰلِكَ فِي قُلُوبِكُمْ وَظَنَنتُمْ ظَنَّ السَّوْءِ وَكُنتُمْ قَوْمًا بُورًا﴿١٢﴾
12. “Bali mlidhania kwamba Rasuli na Waumini hawatorudi kwa ahli zao abadani, na likapambwa hilo katika nyoyo zenu na mkadhania dhana ovu, na mkawa watu wa kuangamia.”


وَمَن لَّمْ يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ فَإِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَعِيرًا﴿١٣﴾
13. Na yeyote asiyemuamini Allaah na Rasuli Wake basi hakika Sisi Tumewaandalia makafiri (Moto wa) Sa’iyraa (uwakao kwa nguvu).”


وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا﴿١٤﴾
14. Na ni wa Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Anamghufuria Amtakaye, na Anamuadhibu Amtakaye; na Allaah daima ni Ghafuwrar-Rahiymaa (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


سَيَقُولُ الْمُخَلَّفُونَ إِذَا انطَلَقْتُمْ إِلَىٰ مَغَانِمَ لِتَأْخُذُوهَا ذَرُونَا نَتَّبِعْكُمْ ۖ يُرِيدُونَ أَن يُبَدِّلُوا كَلَامَ اللَّـهِ ۚ قُل لَّن تَتَّبِعُونَا كَذَٰلِكُمْ قَالَ اللَّـهُ مِن قَبْلُ ۖ فَسَيَقُولُونَ بَلْ تَحْسُدُونَنَا ۚ بَلْ كَانُوا لَا يَفْقَهُونَ إِلَّا قَلِيلًا﴿١٥﴾
15. “Waliobakia nyuma pale mtakapotoka kuelekea kwenye ghanima ili mzichukue watasema: “Tuacheni tukufuateni!” Wanataka kubadilisha Maneno ya Allaah. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hamtotufuata! Hivyo kwenu (ndivyo) Alivyosema Allaah kabla.” Basi watasema: “Bali mnatuhusudu!” Bali walikuwa hawafahamu isipokuwa kidogo “


قُل لِّلْمُخَلَّفِينَ مِنَ الْأَعْرَابِ سَتُدْعَوْنَ إِلَىٰ قَوْمٍ أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ تُقَاتِلُونَهُمْ أَوْ يُسْلِمُونَ ۖ فَإِن تُطِيعُوا يُؤْتِكُمُ اللَّـهُ أَجْرًا حَسَنًا ۖ وَإِن تَتَوَلَّوْا كَمَا تَوَلَّيْتُم مِّن قَبْلُ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا﴿١٦﴾
16. Waambie (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) waliobakia nyuma miongoni mwa mabedui: “Mtaitwa (kuwakabili) watu wenye nguvu kali zaidi mpigane nao, au wasilimu amri. Lakini mkitii, Allaah Atakupeni ujira mzuri; na mkikengeuka kama mlivyokenguka kabla Atakuadhibuni adhabu iumizayo.


لَّيْسَ عَلَى الْأَعْمَىٰ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْمَرِيضِ حَرَجٌ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ وَمَن يَتَوَلَّ يُعَذِّبْهُ عَذَابًا أَلِيمًا﴿١٧﴾
17. Hakuna dhambi juu ya kipofu na wala hakuna dhambi juu ya kilema, na wala hakuna dhambi juu ya mgonjwa (wasipokwenda vitani). Na yeyote yule atakayemtii Allaah na Rasuli Wake, (Allaah) Atamuingiza Jannaat zipitazo chini yake mito. Na atakayekengeuka, Atamuadhibu adhabu iumizayo.


لَّقَدْ رَضِيَ اللَّـهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا﴿١٨﴾
18. Kwa yakini Allaah Amewawia radhi Waumini walipofungamana nawe ahadi ya utiifu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) chini ya mti, (Allaah) Alijua yale yaliyomo nyoyoni mwao; basi Akawateremshia utulivu, na Akawalipa ushindi wa karibu.


وَمَغَانِمَ كَثِيرَةً يَأْخُذُونَهَا ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا﴿١٩﴾
19. Na ghanima nyingi watakazozichukua. Na Allaah daima ni ‘Aziyzan-Hakiymaa (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye hikmah wa yote).


وَعَدَكُمُ اللَّـهُ مَغَانِمَ كَثِيرَةً تَأْخُذُونَهَا فَعَجَّلَ لَكُمْ هَـٰذِهِ وَكَفَّ أَيْدِيَ النَّاسِ عَنكُمْ وَلِتَكُونَ آيَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ وَيَهْدِيَكُمْ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا﴿٢٠﴾
20. Allaah Amekuahidini ghanima nyingi mtazichukua na Akakuharakizieni hizi na Akazuia mikono ya watu dhidi yenu na ili iwe Aayah (ishara, zingatio) kwa Waumini, na Akuongozeni njia iliyonyooka.


وَأُخْرَىٰ لَمْ تَقْدِرُوا عَلَيْهَا قَدْ أَحَاطَ اللَّـهُ بِهَا ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرًا﴿٢١﴾
21. Na (ushindi, ghanima) nyenginezo hamkuwa na uwezo nayo, Allaah Amekwishazizingia. Na Allaah daima juu ya kila kitu ni Qadiyraa (Muweza).


وَلَوْ قَاتَلَكُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوَلَّوُا الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يَجِدُونَ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا﴿٢٢﴾
22. Na kama wangelipigana nanyi wale waliokufuru basi wangeligeuza migongo yao kisha wasipate mlinzi yoyote na wala mwenye kunusuru.


سُنَّةَ اللَّـهِ الَّتِي قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلُ ۖ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّةِ اللَّـهِ تَبْدِيلًا﴿٢٣﴾
23. Desturi ya Allaah ambayo imekwishapita kabla, na wala hutapata mabadiliko katika desturi ya Allaah.


وَهُوَ الَّذِي كَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ عَنْهُم بِبَطْنِ مَكَّةَ مِن بَعْدِ أَنْ أَظْفَرَكُمْ عَلَيْهِمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا﴿٢٤﴾
24. Naye Ndiye Aliyeizuia mikono yao dhidi yenu na mikono yenu dhidi yao katikati ya Makkah baada ya kukupeni ushindi juu yao. Na Allaah daima kwa yale myatendayo ni Baswiyraa (Mwenye kuona).


هُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوكُمْ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَالْهَدْيَ مَعْكُوفًا أَن يَبْلُغَ مَحِلَّهُ ۚ وَلَوْلَا رِجَالٌ مُّؤْمِنُونَ وَنِسَاءٌ مُّؤْمِنَاتٌ لَّمْ تَعْلَمُوهُمْ أَن تَطَئُوهُمْ فَتُصِيبَكُم مِّنْهُم مَّعَرَّةٌ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۖ لِّيُدْخِلَ اللَّـهُ فِي رَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۚ لَوْ تَزَيَّلُوا لَعَذَّبْنَا الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا﴿٢٥﴾
25. Wao ndio wale waliokufuru na wakakuzuieni (kuingia) Al-Masjidil-Haraam na wanyama wa kuchinjwa wakazuiliwa kufika mahali pa kuchinjwa. Na lau kama si wanaume Waumini na wanawake Waumini msiowajua nyinyi – mngewakanyaga (kuwaua) yakakusibuni kutokana na wao dhambi (na fedheha) bila ya kujua - (mngeliruhusiwa kuingia Makkah, lakini imekuwa hivyo) ili Allaah Amuingize katika Rahmah Yake Amtakaye. Na lau kama (Waumini na makafiri) wangelitengana; bila shaka Tungeliwaadhibu wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo.


إِذْ جَعَلَ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْحَمِيَّةَ حَمِيَّةَ الْجَاهِلِيَّةِ فَأَنزَلَ اللَّـهُ سَكِينَتَهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَعَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَأَلْزَمَهُمْ كَلِمَةَ التَّقْوَىٰ وَكَانُوا أَحَقَّ بِهَا وَأَهْلَهَا ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا﴿٢٦﴾
26. Walipotia katika nyoyo zao ghadhabu na kiburi - ghadhabu na kiburi za kipindi cha ujahili Allaah Akateremshia utulivu Wake juu ya Rasuli Wake na juu ya Waumini na Akawalazimisha neno la taqwa (laa ilaaha illa-Allaah), na wakawa ndio wenye haki zaidi kwalo na wenye kustahiki. Na Allaah daima kwa kila kitu ni ‘Aliymaa (Mjuzi).


لَّقَدْ صَدَقَ اللَّـهُ رَسُولَهُ الرُّؤْيَا بِالْحَقِّ ۖ لَتَدْخُلُنَّ الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ إِن شَاءَ اللَّـهُ آمِنِينَ مُحَلِّقِينَ رُءُوسَكُمْ وَمُقَصِّرِينَ لَا تَخَافُونَ ۖ فَعَلِمَ مَا لَمْ تَعْلَمُوا فَجَعَلَ مِن دُونِ ذَٰلِكَ فَتْحًا قَرِيبًا﴿٢٧﴾
27. Kwa yakini Allaah Amemsadikisha Rasuli Wake ndoto (yake) kwa haki. Bila shaka mtaingia Al-Masjidal-Haraam Akipenda Allaah mkiwa katika amani, wenye kunyoa vichwa vyenu na wenye kupunguza, hamukhofu (chochote). Kisha Akajua ambayo hamkujua, Akajaalia kabla ya hayo ushindi wa karibu.


هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا﴿٢٨﴾
28. Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad  (صلى الله عليه وآله وسلم kwa Mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote. Na Allaah Anatosha kuwa Shahiydaa (Mwenye kushuhudia yote).



مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ ۚ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ ۗ وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا﴿٢٩﴾
29. Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri; wanahurumiana baina yao. Utawaona wakirukuu na wakisujudu wakitafuta fadhila na Radhi kutoka kwa Allaah. Alama zao dhahiri zi katika nyuso zao kutokana na athari za sujudu. Huo ni mfano wao katika Tawraat, na mfano wao katika Injiyl kama mmea umetoa chipukizi lake, likautia nguvu kisha likawa nene, kisha likasimama sawasawa juu ya shina lake, liwapendezeshe wakulima (na) ili liwatie ghaidhi makafiri. Allaah Amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema miongoni mwao maghfirah na ujira adhimu.




Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com