الحديث
السادس والثلاثون
"من نفس عن مسلم
كربة"
عن أبي هُرَيْرَة رضي اللهُ عنه، عن النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم
قال: (( مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنْيا نَفَّسَ اللهُ
عَنْهُ كُرْبَةً من كُرَبِ يوْمِ القيامَةِ، ومَنْ يَسَّرَ على مُعْسِرٍ يَسَّرَ
اللهُ عليه في الدنْيا والآخِرَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِماً سَتَرَهُ الله في
الدُّنْيا والآخِرَةِ واللهُ في عَوْنِ الْعَبْدِ
ما كانَ الْعَبْدُ في عَونِ أخيهِ. ومَنْ سلك طَريقاً يَلْتَمِسُ فِيهِ عِلْماً
سَهَّلَ اللهُ له بِهِ طَرِيقاً إلى الجنَّةِ.
وَمَا اجتَمَعَ قَوْمٌ في بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللهِ يَتْلُونَ
كِتَابَ اللهِ ويَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ، إلا نَزَلَتْ عليهمُ السَّكِينَةُ،
وغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ، وحَفَّتهُمُ المَلائِكَةُ، وذَكَرَهُمُ اللهُ فيمَنْ
عِنْدَه . وَمَنْ بَطَّأ بِه عَمَلُهُ لمْ يُسْرِعْ به نَسَبُهُ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ بهذا اللفظ.
HADITHI YA 36
ATAKAYEMUONDOSHEA SHIDA MUISLAMU MWENZAKE,
ALLAH ATAMUONDOSHEA SHIDA ZAKE
Kutoka kwa Abu
Hurayra رضي الله عنه ambaye
amesema kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم
kasema:
Yeyote
atakaemuondoshea shida ya kidunia Muislamu mwenzake, Allaah Atamuondoshea
moja katika shida za siku ya Kiyama.
Yeyote yule
anaemsaidia muhitaji (maskini) Allaah Atamsaidia haja zake hapa duniani
na akhera. Yeyote yule anayemsitiri Muislamu, Allaah
Atamsitiri hapa duniani na akhera.
Mwenyeezi Mungu
humsaidia mja wake wakati wote mja anapomsaidia nduguye (Muislamu).
Yeyote yule anayekamata njia kutafuta elimu, Allaah Atamrahisishia njia
ya peponi. Hawakutaniki watu katika nyumba ya Mwenyeezi Mungu wakisoma
kitabu cha Mwenyeezi Mungu na wakasomeshana pamoja ila watashukiwa na utulivu
(sakina) na kheri. Rehema (za Allah) huwafunika na Malaika huwazunguka na Allaah
Huwakumbuka kwa wale walioko pamoja Nae. Yeyote yule anayeakhirishwa
(anayecheleweshwa) na vitendo vyake (kwenda peponi) hatoharakishwa na Nasab
yake.
Imesimuiwa na
Muslim