114.An-Naas



114. SURAT ANNAS
(Imeteremka Makka)

Katika Sura hii Mwenyezi Mungu anamuamrisha Nabii wake s.a.w. amwendee Yeye amwombe ulinzi kumkinga na shari kubwa zinazo washinda watu wengi kuzitambua kwa sababu zinatokana na matamanio yao, na pumbao lao, basi wakatumbukia katika yale yale wanayo katazwa.
Hiyo ndiyo shari ya wasiwasi wa Shetani, anaye jificha machoni, au hujidhihirisha kwa kificho;  wasiwasi wake ni kwa hila na khadaa.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEM
An-Naas (114)

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾

1. Sema: “Najikinga na Rabb (Mola) wa watu.

مَلِكِ النَّاسِ ﴿٢﴾

2. “Maliki (Mfalme) wa watu.

إِلَـٰهِ النَّاسِ ﴿٣﴾

3. Ilaah (Muabudiwa wa haki) na watu.

مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ ﴿٤﴾

4. “Kutokana na shari za anayetia wasiwasi Al-Khannaas (mwenye kurejea nyuma akinyemelea).

الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ ﴿٥﴾

5. “Ambaye anayetia wasiwasi vifuani mwa watu.

مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ ﴿٦﴾

6. “Miongoni mwa majini na watu.”


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com