Al-‘Aswr (103)

سُورَةُ  الْعَصْر
Al-‘Aswr (103)

(Imeteremka Makka)

 
Katika Sura hii anaapa Subhanahu kwa Zama, kwa zilivyo kusanya chungu ya ajabu, na mazingatio yenye kujuulisha uweza wa Mwenyezi Mungu na hikima yake, ya kwamba mtu haachi kuwa na upungufu katika vitendo vyake na hali zake ila Waumini wanao tenda mema, na wakausiana kushika Haki. Na hiyo ndiyo kheri yote. Na wakausiana kusubiri na kuvumilia juu ya walio amrishwa na walio katazwa.

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَالْعَصْرِ ﴿١﴾

1. Naapa kwa Al-‘Aswr (zama).


إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ ﴿٢﴾

2. Hakika insani bila shaka yumo katika khasara.

إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ ﴿٣﴾

3. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mazuri na wakausiana kwa (kufuata) haki na wakausiana (kuwa na) subira.




Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com