141.
Huo ni ummah kwa yakini umeshapita, utapta uliyoyachuma nanyi mtapata
mliyoyachuma, na wala hamtoulizwa waliyokuwa wakitenda.
سَيَقُولُ السُّفَهَاءُ مِنَ النَّاسِ مَا وَلَّاهُمْ عَن قِبْلَتِهِمُ الَّتِي كَانُوا عَلَيْهَا ۚ قُل لِّلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٤٢﴾
|
142. Watasema masafihi miongoni mwa watu: “Nini kilichowageuza kutoka Qiblah chao ambacho walikuwa wakikielekea!” Sema: “Mashariki na Magharibi ni ya Allaah, Anamwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.” |
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ
وَمَا جَعَلْنَا الْقِبْلَةَ الَّتِي كُنتَ عَلَيْهَا إِلَّا لِنَعْلَمَ
مَن يَتَّبِعُ الرَّسُولَ مِمَّن يَنقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ ۚ وَإِن كَانَتْ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤٣﴾
|
143. Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah waswatwaa (bora na adilifu) ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu. Na Hatukukifanya Qiblah ambacho ulikuwa ukikielekea (cha Baytul-Maqdis
kuwa bora) isipokuwa Tupate kumpambanulisha yule anayemfuata Rasuli
miongoni mwa mwenye kugeuka akarudi nyuma. Na hakika ilikuwa ni jambo
gumu isipokuwa kwa wale ambao Allaah Amewaongoza. Na Allaah Hakuwa
Mwenye kupoteza iymaan yenu, hakika Allaah kwa watu ni Rauwfur-Rahiym (Mwenye huruma mno - Mwenye kurehemu). |
قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاءِ ۖ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا ۚ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ ۗ وَإِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٤٤﴾
|
144. Kwa yakini Tumeona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuzageuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia. Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam. Na popote mtakapokuwepo (mkataka kuswali), basi elekezeni nyuso zenu upande wake. Na hakika wale waliopewa Kitabu bila shaka wanajua kwamba hivyo ni haki kutoka kwa Rabb (Mola) wao. Na Allaah si Mwenye kughafilika kwa wayatendayo.
|
وَلَئِنْ أَتَيْتَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ بِكُلِّ آيَةٍ مَّا تَبِعُوا قِبْلَتَكَ ۚ وَمَا أَنتَ بِتَابِعٍ قِبْلَتَهُمْ ۚ وَمَا بَعْضُهُم بِتَابِعٍ قِبْلَةَ بَعْضٍ ۚ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ إِنَّكَ إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٥﴾
|
145. Na hata ukiwaletea wale waliopewa Kitabu kila Aayah
(ishara, hoja, ushahidi n.k) basi hawatofuata Qiblah chako. Na wewe
hutofuata Qiblah chao. Na wala baadhi yao hawatofuata Qiblah cha baadhi
ya wengineo. Na kama ukiyafuata matamanio yao baada ya kukufikia elimu;
hakika hapo utakuwa miongoni mwa madhalimu.
|
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمْ ۖ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنْهُمْ لَيَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٤٦﴾
|
146. Wale Tulioewapa Kitabu wanatambua (Uislamu na Tawhiyd na Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama wanavyotambua watoto; na hakika kundi miongoni mwao wanaficha haki na hali wao wanajua.
|
الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿١٤٧﴾
|
147. Haki kutoka kwa Rabb (Mola) wako basi kamwe usiwe miongoni mwa wenye shaka.
|
وَلِكُلٍّ وِجْهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَا ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ أَيْنَ مَا تَكُونُوا يَأْتِ بِكُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٤٨﴾
|
148. Na
kila (mmoja ana) upande wa kuuelekea. Basi harakieni (kutenda) mambo ya
kheri. Popote mtakapokuwa Allaah Atakuleteni nyote pamoja (Siku ya
Qiyaamah); hakika Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).
|
وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۖ وَإِنَّهُ لَلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿١٤٩﴾
|
149. Na popote utokako (kwa ajili ya kuswali) basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam. Na hiyo ni haki kutoka kwa Rabb (Mola) wako. Na Allaah si Mwenye kughafilika kwa muyatendayo.
|
وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ
وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ لِئَلَّا يَكُونَ
لِلنَّاسِ عَلَيْكُمْ حُجَّةٌ إِلَّا الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ فَلَا
تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِي وَلِأُتِمَّ نِعْمَتِي عَلَيْكُمْ وَلَعَلَّكُمْ
تَهْتَدُونَ ﴿١٥٠﴾
|
150. Na popote utokako (kwa ajili ya kuswali) basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam.
Na popote mtakapokuwa (mkataka kuswali) basi elekezeni nyuso zenu
upande wake, ili watu wasiwe na hoja juu yenu isipokuwa wale
waliodhulumu miongoni mwao. Basi msiwaogope bali Niogopeni na ili
Nitimize neema Yangu juu yenu na mpate mwongoke.
|
كَمَا
أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِّنكُمْ يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِنَا
وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُم
مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ﴿١٥١﴾
|
151. Kama Tulivyomtuma kwenu Rasuli anayetokana na nyinyi, anawasomea Aayaat Zetu na anakutakaseni na anakufunzeni Kitabu na Hikmah, na anakufundisheni mambo ambayo hamkuwa mkiyajua.
|
فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ ﴿١٥٢﴾
|
152. Basi nidhukuruni na Mimi Nitakukumbukeni; na nishukuruni wala msinikufuru.
|
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٣﴾
|
153. Enyi mlioamini! Tafuteni msaada kwa subira na Swalaah; hakika Allaah Yu pamoja na wanaosubiri.
|
وَلَا تَقُولُوا لِمَن يُقْتَلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتٌ ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ وَلَـٰكِن لَّا تَشْعُرُونَ ﴿١٥٤﴾
|
154. Wala msiseme kwa waliouawa katika njia ya Allaah kuwa ni wafu, bali wahai lakini hamhisi.
|
وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٥﴾
|
155. Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri.
|
الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ﴿١٥٦﴾
|
156. Wale ambao unapowafika msiba husema: “Innaa liLLaahi wa Innaa Ilayhi Raaji’uwn” (Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea).
|
أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ ﴿١٥٧﴾
|
157. Hao juu yao zitakuwa Barakah kutoka kwa Rabb (Mola) wao na Rahmah, na hao ndio wenye kuongoka.
|
إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّـهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٥٨﴾
|
158. Hakika Swafaa na Mar-wah ni katika sha’aair (alama za Dini) Allaah.
Basi yeyote anayehiji kwenye Nyumba (hiyo) au akatekeleza ‘Umrah basi
hakuna lawama kwake kuvizunguka kwayo (vilima viwili hivyo). Na
atakayejitolea kufanya kheri basi hakika Allaah ni Shaakirun-‘Aliym (Mwenye kupokea shukurani - Mjuzi wa yote daima).
|
إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَـٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّـهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ ﴿١٥٩﴾
|
159. Hakika
wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja bayana na mwongozo
baada ya kuwa Tumeyabainisha kwa watu katika Kitabu, hao Anawalaani
Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani.
|
إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَبَيَّنُوا فَأُولَـٰئِكَ أَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنَا التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٠﴾
|
160. Isipokuwa wale waliotubu na wakatengenea na wakabainisha (waliyoyaficha); basi hao Napokea tawbah zao, Na Mimi ni At-Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah - Mwenye kurehemu).
|
إِنَّ
الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ
لَعْنَةُ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿١٦١﴾
|
161. Hakika wale waliokufuru na wakafa hali ya kuwa ni makafiri; hao iko juu yao laana ya Allaah na Malaika na watu wote.
|
خَالِدِينَ فِيهَا ۖ لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿١٦٢﴾
|
162. Wenye kudumu humo, hawatopunguziwa adhabu na wala wao hawatopewa muhula wa kupumzika.
|
وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾
|
163. “Na Ilaah wenu (Muabudiwa wa haki) ni Ilaah Mmoja (Pekee) hakuna ilaaha ila Yeye. (Ar-Rahmaanur-Rahiym (Mwingi wa Rahmah - Mwenye kurehemu).”
|
إِنَّ
فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ
وَالنَّهَارِ وَالْفُلْكِ الَّتِي تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِمَا يَنفَعُ
النَّاسَ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن مَّاءٍ فَأَحْيَا
بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَابَّةٍ
وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخَّرِ بَيْنَ السَّمَاءِ
وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿١٦٤﴾
|
164. Hakika
katika kuumbwa mbingu na ardhi na mabadiliko ya usiku na mchana na
merikebu zipitazo katika bahari viwafaavyo watu na Aliyoteremsha Allaah
kutoka mbinguni katika maji Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake na
Akaeneza humo kila aina ya mnyama na mgeuko wa pepo na mawingu
yanayotiishwa baina ya mbingu na ardhi ni Ayaat kwa watu wenye akili.
|
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ
وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُوا إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ
الْقُوَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا وَأَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ ﴿١٦٥﴾
|
165. Na
miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah kuwa ni
wanaolingana (na Allaah) wanawapenda kama mapenzi (yapasavyo) ya
kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. Na
lau wangelitambua wale waliodhulumu (yatayowakuta) watakapoona adhabu
(wataelewa) kwamba Nguvu zote ni za Allaah; na kwamba hakika Allaah ni
Mkali wa kuadhibu.
|
إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ ﴿١٦٦﴾
|
166.
(Watambue kwamba) Wale waliofuatwa watakapowakana wale waliowafuata
wakiwa wameshaiona adhabu; na yatawakatikia mafungamano yao (ya
uhusiano).
|
وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا ۗ كَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ اللَّـهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ ۖ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ ﴿١٦٧﴾
|
167. Na
watasema wale waliofuata: “Lau tungekuwa tunamiliki kurudi (duniani)
tungewakana kama walivyotukana.” Hivyo ndivyo Allaah Atakavyowaonyesha
‘amali zao kuwa ni majuto juu yao. Na wala hawatokuwa wenye kutoka
Motoni.
|
يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُلُوا مِمَّا فِي الْأَرْضِ حَلَالًا طَيِّبًا وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿١٦٨﴾
|
168. Enyi
watu! Kuleni katika vilivyomo ardhini vya halaal, vizuri; na wala
msifuate hatua za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui bayana.
|
إِنَّمَا يَأْمُرُكُم بِالسُّوءِ وَالْفَحْشَاءِ وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿١٦٩﴾
|
169. Hakika hakuna isipokuwa anakuamrisheni maovu na machafu (na ubakhili) na mseme dhidi ya Allaah msiyoyajua.
|
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۗ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ ﴿١٧٠﴾
|
170. Na
wanapoambiwa: “Fuateni Aliyoyateremsha Allaah” Husema: “Bali tunafuata
tuliyowakuta nayo baba zetu.” Je, japokuwa baba zao walikuwa hawaelewi
kitu chochote na wala hawakuongoka?
|
وَمَثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا كَمَثَلِ الَّذِي يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَاءً وَنِدَاءً ۚ صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿١٧١﴾
|
171. Na
mfano wa wale waliokufuru ni kama mfano wa yule ambaye anapiga kelele
kwa asiyesikia ila wito na kelele tu (za wanyama anaowachunga); viziwi,
mabubu, vipofu kwa hiyo hawaelewi. |
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّـهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ ﴿١٧٢﴾
|
172. Enyi mlioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni na mshukuruni Allaah mkiwa mnamwabudu Yeye Pekee.
|
إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٧٣﴾
|
173. Hakika
Allaah Amekuharamishieni mzoga na damu na nyama ya nguruwe na
kilichotajiwa kwacho (katika kuchinjwa) asiyekuwa Allaah. Lakini
aliyefikwa na dharura bila ya kutamani wala kupindukia mpaka; basi si
dhambi juu yake. Hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).
|
إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ الْكِتَابِ وَيَشْتَرُونَ بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۙ
أُولَـٰئِكَ مَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ إِلَّا النَّارَ وَلَا
يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ
عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٤﴾
|
174. Hakika
wale wanaoficha yale Aliyoyateremsha Allaah katika Kitabu na
wakabadilisha kwacho kwa thamani ndogo; hao hawali katika matumbo yao
isipokuwa moto, na wala Allaah Hatowasemesha Siku ya Qiyaamah na wala
Hatowatakasa nao watapata adhabu iumizayo.
|
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَىٰ وَالْعَذَابَ بِالْمَغْفِرَةِ ۚ فَمَا أَصْبَرَهُمْ عَلَى النَّارِ ﴿١٧٥﴾
|
175. Hao ndio wale waliobadilisha upotofu kwa uongofu na adhabu kwa maghfirah. Basi kuvumilia gani huko kwao ndani ya Moto?
|
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ نَزَّلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ ۗ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِي الْكِتَابِ لَفِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ ﴿١٧٦﴾
|
176. Hivyo
(wanastahiki) kwa sababu Allaah Amekiteremsha Kitabu kwa haki. Na
hakika wale waliokhitilafiana katika Kitabu wamo katika upinzani wa
mbali (na haki).
|
لَّيْسَ
الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ
وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ
وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ وَآتَى الْمَالَ عَلَىٰ
حُبِّهِ ذَوِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينَ وَابْنَ
السَّبِيلِ وَالسَّائِلِينَ وَفِي الرِّقَابِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى
الزَّكَاةَ وَالْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَاهَدُوا ۖ وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ ﴿١٧٧﴾
|
177. Si
wema (pekee) kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na
Magharibi lakini wema (khasa) ni mwenye kuamini Allaah na Siku ya Mwisho
na Malaika na Kitabu na Nabiy, na akawapa mali juu ya kuipenda kwake
jamaa wa karibu na mayatima na masikini na msafiri (aliyeharibikiwa) na
waombao (msaada) na katika kukomboa watumwa na akasimamisha Swalaah, na
akatoa Zakaah na watimizao ahadi zao wanapoahidi, na wanaosubiri katika mashaka (ufukara, dhiki ya maisha) na madhara (magonjwa, misiba n.k) na katika vita. Hao ndio waliosadikisha na hao ndio wenye taqwa.
|
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِصَاصُ فِي الْقَتْلَى ۖ الْحُرُّ بِالْحُرِّ وَالْعَبْدُ بِالْعَبْدِ وَالْأُنثَىٰ بِالْأُنثَىٰ ۚ فَمَنْ عُفِيَ لَهُ مِنْ أَخِيهِ شَيْءٌ فَاتِّبَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ وَأَدَاءٌ إِلَيْهِ بِإِحْسَانٍ ۗ ذَٰلِكَ تَخْفِيفٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَرَحْمَةٌ ۗ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٨﴾
|
178. Enyi mlioamini! Mmeandikiwa (shariy’ah
ya kulipiza) kisasi waliouawa. Muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa
mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke, na anayesamehewa na nduguye kwa lolote
basi kufuatilizwa kwake kuwe kwa wema na kumlipa kwake iwe kwa ihsaan. Hiyo ni takhafifu kutoka kwa Rabb (Mola) wenu na Rahmah. Na atakayeruka mipaka baada ya hapo basi atapata adhabu iumizayo. |
وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٧٩﴾
|
179. Na mtapata katika (kulipiza) kisasi (kuokoa) uhai enyi wenye akili mpate kuwa na taqwa.
|
كُتِبَ
عَلَيْكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ إِن تَرَكَ خَيْرًا
الْوَصِيَّةُ لِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُتَّقِينَ ﴿١٨٠﴾
|
180. Mmeandikiwa (shariy’ah) kuwa anapofikiwa mmoja wenu na mauti kama ameacha mali, kufanya wasia kwa wazazi wawili, na jamaa wa karibu kwa maaruwf (namna inayoeleweka katika shariy’ah). Haya ni wajibu kwa wenye taqwa.
|
فَمَن بَدَّلَهُ بَعْدَ مَا سَمِعَهُ فَإِنَّمَا إِثْمُهُ عَلَى الَّذِينَ يُبَدِّلُونَهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿١٨١﴾
|
181. Atakayeubadilisha (huo wasia) baada ya kuusikia; basi hakika dhambi yake ni juu ya wale watakaoubadilisha. Hakika Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote daima - Mjuzi wa yote daima).
|
فَمَنْ خَافَ مِن مُّوصٍ جَنَفًا أَوْ إِثْمًا فَأَصْلَحَ بَيْنَهُمْ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٨٢﴾
|
182. Basi
mwenye kukhofu kwamba muusiaji kakosea au kapata dhambi (kwa kufanya
makosa makusudi) akasuluhisha baina yao; basi haitokuwa dhambi juu yake.
Hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).
|
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٨٣﴾
|
183. Enyi mlioamini! Mmeandikiwa (fardhi ya) Swiyaam kama ilivyoandikwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa.
|
أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ ۖ فَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ ۚ وَأَن تَصُومُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٨٤﴾
|
184. (Kufunga Swiyaam
kwenyewe ni) Siku za kuhesabika. Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni
mwenu, au yuko safarini (akafunga baadhi ya siku); basi (akamilishe)
idadi (ya siku anazotakiwa kufunga) katika siku nyinginezo. Na ni juu ya
wale wanaoiweza (kufunga Swiyaam) lakini kwa tabu (kama wazee) watoe
fidia; kulisha masikini (kila siku). Na atakayejitolea kwa jema lolote
lile basi ni bora kwake. Na mkifunga Swiyaam ni bora kwenu mkiwa mnajua.
|
شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ
يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ
وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ
وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٨٥﴾
|
185. Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na al-furqaan (pambanuo la haki na ubatilifu). Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi (mpya) na afunge Swiyaam.
Na atakayekuwa mgonjwa au safarini basi (atimize) idadi katika siku
nyinginezo. Allaah Anakutakieni mepesi na wala Hakutakieni magumu; na
ili mkamilishe idadi na ili mumkabbiri Allaah (mseme: Allaahu Akbar) kwa kuwa Amekuongozeni na mpate kushukuru.
|
وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴿١٨٦﴾
|
186. Na watakapokuuliza waja Wangu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Mimi, basi Mimi ni Qariyb
(Yu karibu daima kwa ujuzi Wake); Naitikia du’aa ya muombaji
anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka.
|
أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتَانُونَ أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿١٨٧﴾
|
187. Mmehalalishiwa usiku wa Swiyaam
kujamiiana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao.
Allaah Anajua kwamba nyinyi mlikuwa mkizihini nafsi zenu hivyo Akapokea tawbah
yenu na Akakusameheni. Basi sasa changanyikeni nao (waingilieni) na
tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu. Na kuleni na kunyweni mpaka
ibainike kwenu weupe (wa Afajiri) kutokana na weusi (wa usiku). Kisha
timizeni Swiyaam mpaka usiku. Na wala msichanganyike nao hali ya kuwa nyinyi wenye kukaa i’tikaaf Misikitini. Hiyo ni mipaka ya Allaah basi msiikaribie. Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat (na hukmu) Zake kwa watu wapate kuwa na taqwa.
|
وَلَا
تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ وَتُدْلُوا بِهَا إِلَى
الْحُكَّامِ لِتَأْكُلُوا فَرِيقًا مِّنْ أَمْوَالِ النَّاسِ بِالْإِثْمِ
وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٨٨﴾
|
188. Na
wala msiliane mali zenu kwa ubatilifu na kuzipeleka (rushwa) kwa
mahakimu ili mle sehemu katika mali ya watu kwa dhambi nanyi mnajua
(kwamba ni haraam).
|
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ ۗ وَلَيْسَ الْبِرُّ بِأَن تَأْتُوا الْبُيُوتَ مِن ظُهُورِهَا وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ أَبْوَابِهَا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٨٩﴾
|
189. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu
miezi (inapoandama). Sema: “Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa watu na
Hajj.” Na si wema kuingia nyumba kwa nyuma yake, lakini wema ni kuwa na
taqwa. Na ingieni nyumba (zenu) kupitia milango yake. Na mcheni Allaah
mpate kufaulu.
|
وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿١٩٠﴾
|
190. Na
piganeni katika njia ya Allaah (dhidi ya) wale wanaokupigeni, wala
msivuke mipaka. Hakika Allaah Hapendi wanaopindukia mipaka.
|
وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ الْقَتْلِ ۚ وَلَا تُقَاتِلُوهُمْ عِندَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَاتِلُوكُمْ فِيهِ ۖ فَإِن قَاتَلُوكُمْ فَاقْتُلُوهُمْ ۗ كَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ ﴿١٩١﴾
|
191. Na wauweni popote muwakutapo, na watoeni popote walipokutoeni na fitnah ni mbaya zaidi kuliko kuua. Na wala msipigane nao kwenye Al-Masjidil-Haraam mpaka wakupigeni humo, watakapokupigeni basi (nanyi pia) wapigeni. Namna hivi ndivyo (inavyokuwa) jazaa ya makafiri.
|
فَإِنِ انتَهَوْا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٩٢﴾
|
192. Wakikoma, basi Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).
|
وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلَّـهِ ۖ فَإِنِ انتَهَوْا فَلَا عُدْوَانَ إِلَّا عَلَى الظَّالِمِينَ ﴿١٩٣﴾
|
193. Na piganeni nao mpaka kusiweko fitnah (shirki, kufru), na Dini iwe kwa ajili ya Allaah Pekee, wakikoma basi kusiweko na uadui ila kwa madhalimu.
|
الشَّهْرُ الْحَرَامُ بِالشَّهْرِ الْحَرَامِ وَالْحُرُمَاتُ قِصَاصٌ ۚ فَمَنِ اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ ﴿١٩٤﴾
|
194. (Kupigana katika) Mwezi
mtukufu kwa (ajili ya ushari katika) mwezi mtukufu, na vitukufu
vimewekewa kisasi. Basi atakayekufanyieni uadui, nanyi mfanyieni uadui
kwa kadiri alivyokufanyieni uadui. Na mcheni Allaah, na jueni kwamba
Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.
|
وَأَنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ۛ وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٩٥﴾
|
195. Na
toeni katika njia ya Allaah wala msijitupe kwa mikono yenu katika
maangamizi. Na fanyeni ihsaan Hakika Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.
|
وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ ۚ فَإِنْ أُحْصِرْتُمْ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۖ وَلَا تَحْلِقُوا رُءُوسَكُمْ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْهَدْيُ مَحِلَّهُ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ بِهِ أَذًى مِّن رَّأْسِهِ فَفِدْيَةٌ مِّن صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ ۚ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَمَن تَمَتَّعَ بِالْعُمْرَةِ إِلَى الْحَجِّ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۚ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ فِي الْحَجِّ وَسَبْعَةٍ إِذَا رَجَعْتُمْ ۗ تِلْكَ عَشَرَةٌ كَامِلَةٌ ۗ ذَٰلِكَ لِمَن لَّمْ يَكُنْ أَهْلُهُ حَاضِرِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿١٩٦﴾
|
196. Na timizeni Hajj na ‘Umrah
kwa ajili ya Allaah. Na kama mkizuilika basi (chinjeni) wanyama walio
wepesi kupatikana. Na wala msinyoe vichwa vyenu mpaka mnyama afikie
machinjoni pake. Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au ana vya
kumuudhi kichwani mwake (ikambidi anyoe); basi atoe fidia kwa kufunga Swiyaam (siku tatu) au
kutoa sadaka au kuchinja mnyama. Na mtakapopata amani, basi mwenye
kutekeleza ‘Umrah (katika miezi ya Hajj) kisha Hajj, basi achinje mnyama
aliye mwepesi. Na asiyepata (mnyama), afunge Swiyaam siku tatu
katika Hajj na (siku) saba mtakaporejea. Hizo ni (siku) kumi timilifu.
Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawaishi karibu na Al-Masjidil-Haraam. Na mcheni Allaah, na jueni kwamba Allaah ni Mkali wa kuakibu
|
الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ ۚ وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٧﴾
|
197. Hajj
ni miezi maalumu. Na atakayekusudia kuhiji (akaingia katika Ihraam),
basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika Hajj. Na
lolote mlifanyalo katika ya kheri Allaah Analijua. Na chukueni masurufu.
Na hakika bora ya masurufu ni taqwa. Na nicheni Mimi enyi wenye akili!
|
لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَبْتَغُوا فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ ۚ فَإِذَا أَفَضْتُم مِّنْ عَرَفَاتٍ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ عِندَ الْمَشْعَرِ الْحَرَامِ ۖ وَاذْكُرُوهُ كَمَا هَدَاكُمْ وَإِن كُنتُم مِّن قَبْلِهِ لَمِنَ الضَّالِّينَ ﴿١٩٨﴾
|
198. Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Rabb (Mola) wenu. Basi mtakapomiminika kutoka ‘Arafaat mdhukuruni Allaah kwenye Mash’aril- Haraam (Muzdalifah) na mdhukuruni Yeye kama Alivyokuongozeni kwani hakika mlikuwa kabla ya hapo miongoni mwa waliopotea.
|
ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٩٩﴾
|
199. Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu; na ombeni maghfirah kwa Allaah. Hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).
|
فَإِذَا قَضَيْتُم مَّنَاسِكَكُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَذِكْرِكُمْ آبَاءَكُمْ أَوْ أَشَدَّ ذِكْرًا ۗ فَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ﴿٢٠٠﴾
|
200. Mtakapomaliza kutekeleza manaasik zenu (‘ibaadah za Hajj), basi mdhukuruni Allaah kama mnavyowadhukuru baba zenu au (mdhukuruni) dhikri[1] zaidi. Kwani kuna baadhi ya watu wasemao: “Rabb (Mola) wetu Tupe katika dunia;” naye katika Aakhirah hana sehemu yoyote.
|
وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿٢٠١﴾
|
201. Na miongoni mwao (wako) wasemao: “Rabb (Mola) wetu Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah (pia Tupe) mazuri na Tukinge na adhabu ya Moto.”
|
أُولَـٰئِكَ لَهُمْ نَصِيبٌ مِّمَّا كَسَبُوا ۚ وَاللَّـهُ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٢٠٢﴾
|
202. Hao watapata pato lao kutokana na waliyoyachuma, na Allaah ni Mwepesi wa kuhesabu.
|
وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٢٠٣﴾
|
203. Na
mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika. Atakayeharakisha
(akaondoka Minaa na kurudi Makkah) katika siku mbili, basi hakuna dhambi
juu yake; na atakayechelewesha (akabakia Minaa mpaka siku ya tatu) basi hakuna dhambi juu yake; kwa mwenye kuwa na taqwa. Na mcheni Allaah na jueni kwamba Kwake mtakusanywa.
|
وَمِنَ
النَّاسِ مَن يُعْجِبُكَ قَوْلُهُ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيُشْهِدُ
اللَّـهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلْبِهِ وَهُوَ أَلَدُّ الْخِصَامِ ﴿٢٠٤﴾
|
204. Na
katika watu yupo mwenye kukuvutia kauli yake katika uhai wa dunia na
humshuhudisha Allaah kwa yale yaliyomo katika moyo wake na hali yeye
ndiye khasimu mbaya zaidi.
|
وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ ﴿٢٠٥﴾
|
205. Na
anapoondoka hufanya bidii (kufanya akitakacho) katika ardhi ili afisidi
humo na aangamize mimea na vizazi. Na Allaah Hapendi ufisadi.
|
|
وَإِذَا قِيلَ لَهُ اتَّقِ اللَّـهَ أَخَذَتْهُ الْعِزَّةُ بِالْإِثْمِ ۚ فَحَسْبُهُ جَهَنَّمُ ۚ وَلَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿٢٠٦﴾
|
206. Na anapoambiwa: “Muogope Allaah!” Hupandwa na mori kwa (kutenda) dhambi. Basi (Moto wa) Jahannam unamtosheleza na ni pabaya palioje mahali pa kupumzika.
|
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْرِي نَفْسَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴿٢٠٧﴾
|
207. Na miongoni mwa watu yuko anayeiuza nafsi yake kutafuta Radhi za Allaah. Na Allaah ni Rauwfun (Mwenye huruma mno) kwa waja.
|
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٢٠٨﴾
|
208. Enyi mlioamini! Ingieni katika Uislamu kikamilifu, na wala msifuate hatua za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.
|
فَإِن زَلَلْتُم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْكُمُ الْبَيِّنَاتُ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٠٩﴾
|
209. Lakini mkiteleza (mkakengeuka) baada ya kukujieni hoja bayana, jueni kwamba hakika Allaah ni ‘Aziyzun-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).
|
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٢١٠﴾
|
210. Je,
wanangojea (nini) isipokuwa Allaah Awajie katika vivuli vya mawingu
(pamoja) na Malaika, na itolewe hukumu? Na kwa Allaah hurudishwa mambo.
|
سَلْ بَنِي إِسْرَائِيلَ كَمْ آتَيْنَاهُم مِّنْ آيَةٍ بَيِّنَةٍ ۗ وَمَن يُبَدِّلْ نِعْمَةَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٢١١﴾
|
211. Waulize wana wa Israaiyl, Aayah
(miujiza, ishara, hoja) ngapi Tumewapa zilizo bayana? Na
atakayebadilisha neema ya Allaah (kwa kufru) baada ya kumjia, (basi
hakika Allaah ni Mkali wa kuakibu.
|
زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَيَسْخَرُونَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا ۘ وَالَّذِينَ اتَّقَوْا فَوْقَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَاللَّـهُ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٢١٢﴾
|
212. Wamepambiwa
wale waliokufuru uhai wa dunia na wanawakejeli wale walioamini. Na wale
walio na taqwa watakuwa juu yao Siku ya Qiyaamah. Na Allaah Humruzuku
Amtakaye bila ya hesabu.
|
كَانَ
النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّـهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ
وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ
النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ ۚ وَمَا اخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا الَّذِينَ أُوتُوهُ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۖ فَهَدَى اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ ۗ وَاللَّـهُ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٢١٣﴾
|
213. Watu walikuwa ummah
mmoja (kabla kupotoka kwao) kisha Allaah Akatuma Nabiy wabashiriaji na
waonyaji na Akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki ili kihukumu baina ya
watu katika waliyokhitilafiana kwayo. Na hawakukhitilafiana katika hayo
isipokuwa wale waliopewa hicho (Kitabu) baada ya kuwajia hoja bayana,
kwa sababu ya chuki baina yao. Allaah Akawaongoza wale walioamini
kuendea haki katika yale waliyokhitilafiana, kwa idhini Yake. Na Allaah
Humwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.
|
أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِكُم ۖ
مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّىٰ يَقُولَ
الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَىٰ نَصْرُ اللَّـهِ ۗ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّـهِ قَرِيبٌ ﴿٢١٤﴾
|
214. Je, mnadhani kwamba mtaingia Jannah
na hali bado haijakufikieni (mitihani) kama ya wale waliopita kabla
yenu? Iliwagusa (shida za) ufukara na dhara za (maafa, magonjwa) na
wakatetemeshwa mpaka Rasuli na wale walioamini pamoja naye wanasema:
“Lini itafika nusura ya Allaah?” Tanabahi! Hakika nusura ya Allaah iko
karibu.
|
يَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ ۖ قُلْ مَا أَنفَقْتُم مِّنْ خَيْرٍ فَلِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢١٥﴾
|
215. Wanakuuliza
nini watoe? Sema: “Mnachotoa chochote katika kheri basi ni kwa ajili
ya wazazi wawili, na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini, na
msafiri”. Na lolote mlifanyalo katika kheri basi hakika Allaah kwa hilo
ni ‘Aliym (Mjuzi).
|
كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢١٦﴾
|
216. Mmeandikiwa
kupigana (vita) nako ni chukizo kwenu. Na huenda mkachukia jambo na
hali lenyewe ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda jambo na hali lenyewe ni
la shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui.
|
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ ۖ قُلْ قِتَالٌ فِيهِ كَبِيرٌ ۖ وَصَدٌّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَكُفْرٌ بِهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَإِخْرَاجُ أَهْلِهِ مِنْهُ أَكْبَرُ عِندَ اللَّـهِ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَكْبَرُ مِنَ الْقَتْلِ ۗ وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّىٰ يَرُدُّوكُمْ عَن دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا ۚ وَمَن يَرْتَدِدْ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢١٧﴾
|
217. Wanakuuliza
kuhusu miezi mitukufu (kama inafaa) kupigana humo. Sema: “Kupigana humo
ni (dhambi) kubwa. Na kuzuia (watu kufuata) njia ya Allaah na
kumkanusha Yeye na (kuzuia watu wasiende) Al-Masjidil-Haraam na kuwatoa watu wake humo ni (dhambi) kubwa zaidi mbele ya Allaah. Na fitnah
ni mbaya zaidi kuliko kuua”. Na wala hawatoacha kukupigeni vita mpaka
wakutoeni katika Dini yenu wakiweza. Na atakayeritadi miongoni mwenu
kutoka Dini yake, akafariki hali ya kuwa ni kafiri, basi hao
zimeporomoka ‘amali zao katika dunia na Aakhirah. Na hao ni watu wa
Motoni, wao humo ni wenye kudumu.
|
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَتَ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢١٨﴾
|
218. Hakika wale walioamini na wale waliohajiri na wakapigana jihaad katika njia ya Allaah, hao wanataraji Rahmah ya Allaah, na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).
|
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١٩﴾
|
219. Wanakuuliza
kuhusu ulevi na kamari. Sema: “Humo (katika viwili vyote) mna dhambi
kubwa na (pia mna baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake (vitu
viwili hivyo) ni kubwa kuliko manufaa yake.” Na wanakuuliza nini watoe.
Sema: “Al-’Afwa (yaliyokuzidieni).” Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na hukmu za shariy’ah) mpate kutafakari.
|
فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۗ وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَىٰ ۖ قُلْ إِصْلَاحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ ۖ وَإِن تُخَالِطُوهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ الْمُفْسِدَ مِنَ الْمُصْلِحِ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَأَعْنَتَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٠﴾
|
220. Katika
dunia na Aakhirah. Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: “Kuwatengeneza
ni kheri. Na Allaah Anamjua fisadi na mtengenezaji. Na lau Angetaka
Allaah Angelikutieni katika shida.” Hakika Allaah ni ‘Aziyzun Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).
|
وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٢١﴾
|
221. Na
wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni
bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Na wala msiwaozeshe wanaume
washirikina (wanawake wa Kiislamu) mpaka waamini. Na mtumwa Muumini ni
bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Hao (washirikina) wanaita
katika Moto na Allaah Anaita katika Al-Jannah na maghfirah kwa Idhini Yake. Na Anabainisha Aayaat (na hukmu) Zake wapate kukumbuka.
|
وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ ﴿٢٢٢﴾
|
222. Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni adhaa
(dhara); basi waepukeni wanawake (wanapokuwa) katika hedhi. Wala
msiwakaribie (kujimai nao) mpaka watwaharike. Watapotwaharika basi
waendeeni kupitia pale Alipokuamrisheni Allaah (kunapotoka kizazi)”.
Hakika Allaah Anapenda wenye kutubia na Anapenda wenye kujitwaharisha.
|
نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُم مُّلَاقُوهُ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٢٣﴾
|
223. Wake
zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi)
vyovyote mpendavyo. Na tangulizeni (kujikurubisha kwa Allaah) kwa ajili
ya nafsi zenu. Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika nyinyi ni wenye
kukutana Naye. Na wabashirie Waumini.
|
وَلَا تَجْعَلُوا اللَّـهَ عُرْضَةً لِّأَيْمَانِكُمْ أَن تَبَرُّوا وَتَتَّقُوا وَتُصْلِحُوا بَيْنَ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٢٤﴾
|
224. Wala
msifanye (kuapa kwa Jina la) Allaah kuwa ni nyudhuru ya viapo vyenu
(kukuzuieni) katika kutenda wema na kuwa na taqwa na kusuluhisha baina
ya watu. Na Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote daima - Mjuzi wa yote daima).
|
لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿٢٢٥﴾
|
225. Allaah Hatokuchukulieni (kukuadhibuni) kwa viapo vyenu vya upuuzi lakini Atakuchukulieni kwa yaliyochuma nyoyo zenu. Na Allaah ni Ghafuwrun-Haliym (Mwingi wa kughufuria - Mpole wa kuwavumilia waja).
|
لِّلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِن نِّسَائِهِمْ تَرَبُّصُ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ ۖ فَإِن فَاءُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٢٦﴾
|
226. Kwa wale walioapa kujitenga na wake zao (kutokujamiiana) wangojee miezi minne. Wakirejea; basi hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).
|
وَإِنْ عَزَمُوا الطَّلَاقَ فَإِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٢٧﴾
|
227. Na wakiazimia talaka, basi hakika Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote daima - Mjuzi wa yote daima).
|
وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ ۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَن يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللَّـهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ إِن كُنَّ يُؤْمِنَّ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَٰلِكَ إِنْ أَرَادُوا إِصْلَاحًا ۚ وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٨﴾
|
228. Na wanawake waliotalakiwa wabakie kungojea (wasiolewe) quruu
(twahara au hedhi) tatu. Na wala si halaal kwao kuficha Aliyoumba
Allaah katika matumbo yao ikiwa wao ni wenye kumwamini Allaah na Siku ya
Mwisho. Na waume zao wana haki kuwarejea katika (muda) huo ikiwa
wakitaka suluhu. Nao (wanawake) wana (haki) kama ambayo (ya waume zao)
iliyo juu yao kwa ma’aruwf (mujibu wa shariy’ah). Na wanaume wana daraja zaidi (la jukumu) juu yao (hao wanawake). Na Allaah ni ‘Aziyzun-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).
|
الطَّلَاقُ مَرَّتَانِ ۖ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ ۗ وَلَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَأْخُذُوا مِمَّا آتَيْتُمُوهُنَّ شَيْئًا إِلَّا أَن يَخَافَا أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا فِيمَا افْتَدَتْ بِهِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَعْتَدُوهَا ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٢٩﴾
|
229. Talaka ni mara mbili. Hivyo kuzuia kwa ma’aruwf (mujibu wa shariy’ah)
au kuachia kwa ihsaan. Wala si halaal kwenu kuchukua chochote katika
mlivyowapa (hao wanawake), isipokuwa wote wawili (mume na mke) wakikhofu
kuwa hawatoweza kusimamisha mipaka ya Allaah. Mtakapokhofu kuwa wote
wawili hawatoweza kusimamisha mipaka ya Allaah; basi hakuna lawama juu
yao katika (kupokea au kutoa) (mahari – khul’u)
atakayojikombolea kwayo (mke). Hiyo ni mipaka ya Allaah basi msiivuke.
Na atakayevuka mipaka ya Allaah basi hao ndio madhalimu. |
فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُ مِن بَعْدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوْجًا غَيْرَهُ ۗ فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يَتَرَاجَعَا إِن ظَنَّا أَن يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ ۗ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٢٣٠﴾
|
230. Na
akimtalaki (mara ya tatu) basi hatokuwa halaal kwake baada ya hapo
mpaka aolewe na mume mwengine. Akimtalaki (huyo mume mwengine, au
akifariki) hapatokuwa dhambi juu yao wawili (mwanamke na mumewe wa
kwanza) kurejeana wakidhani kwamba watasimamisha mipaka ya Allaah. Na
hiyo ni mipaka ya Allaah Anaibainisha kwa watu wanaojua.
|
وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ سَرِّحُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ ۚ وَلَا تُمْسِكُوهُنَّ ضِرَارًا لِّتَعْتَدُوا ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ ۚ وَلَا تَتَّخِذُوا آيَاتِ اللَّـهِ هُزُوًا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَمَا أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّنَ الْكِتَابِ وَالْحِكْمَةِ يَعِظُكُم بِهِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٣١﴾
|
231. Na mtakapowatalaki wanawake wakafikia muda wao (wa kukaribia kumaliza eda); basi wazuieni (warejeeni) kwa ma’aruwf (wema) au waacheni (talaka) kwa ma’aruwf (mujibu wa shariy’ah).
Na wala msiwazuie kuwakusudia dhara mkaruka mipaka. Na atakayefanya
hiyvo basi kwa yakini amejidhulumu nafsi yake. Na wala msizifanyie mzaha
Aayaat (na hukmu) za Allaah. Na kumbukeni neema za Allaah juu
yenu na Aliyokuteremshieni katika Kitabu na Hikmah Anakuwaidhini kwayo.
Na mcheni Allaah na jueni kwamba Allaah kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi).
|
وَإِذَا
طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعْضُلُوهُنَّ أَن
يَنكِحْنَ أَزْوَاجَهُنَّ إِذَا تَرَاضَوْا بَيْنَهُم بِالْمَعْرُوفِ ۗ ذَٰلِكَ يُوعَظُ بِهِ مَن كَانَ مِنكُمْ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۗ ذَٰلِكُمْ أَزْكَىٰ لَكُمْ وَأَطْهَرُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢٣٢﴾
|
232. Na
mtakapowatalaki wanawake kisha wakafikia muda wao; basi msiwazuie
kuolewa na waume zao (wa awali) ikiwa wameridhiana baina yao kwa ma’aruwf
(mujibu wa ada). Hayo anawaidhiwa kwayo yeyote miongoni mwenu mwenye
kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo kwenu ni wema zaidi na safi
kabisa. Na Allaah Anajua nanyi hamjui.
|
وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ ۖ لِمَنْ أَرَادَ أَن يُتِمَّ الرَّضَاعَةَ ۚ وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ لَا تُكَلَّفُ نَفْسٌ إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَا تُضَارَّ وَالِدَةٌ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوْلُودٌ لَّهُ بِوَلَدِهِ ۚ وَعَلَى الْوَارِثِ مِثْلُ ذَٰلِكَ ۗ فَإِنْ أَرَادَا فِصَالًا عَن تَرَاضٍ مِّنْهُمَا وَتَشَاوُرٍ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا ۗ وَإِنْ أَرَدتُّمْ أَن تَسْتَرْضِعُوا أَوْلَادَكُمْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِذَا سَلَّمْتُم مَّا آتَيْتُم بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٣٣﴾
|
233. Na
wazazi wa kike wanyonyeshe waladi wao miaka miwili kamili, kwa mwenye
kutaka kutimiza kunyonyesha. Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia
chakula chao na nguo kwa ma’aruwf (mujibu wa ada).
Hailazimishwi nafsi ila kwa liliwezalo. Asidhuriwe mzazi wa kike kwa
ajili ya waladi wake, na wala mzazi wa kiume (pia) kwa ajili ya waladi
wake. Na juu ya mrithi (wa baba) mfano wa hivyo. Watakapotaka (wote
wawili) kumwachisha (kunyonya) kwa maridhiano baina yao (wawili) na
mashauriano basi hapana dhambi juu ya wawili hao. Na mtakapotaka
kutafuta wa kuwayonyesha waladi wenu, basi si dhambi kwenu ikiwa mtatoa
(kuwalipa) mlichoahidi kwa ma’aruwf. Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona).
|
وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا ۖ فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا فَعَلْنَ فِي أَنفُسِهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٣٤﴾
|
234.
Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, (hao wake) wangojee
nafsi zao miezi minne na (siku) kumi (eda ya mfiwa). Watakapofikia muda
wao, si dhambi kwao katika yale waliyoyafanya katika nafsi zao kwa
ma’aruwf. Na Allaah kwa myatendayo ni Khabiyr (Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana).
|
وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُم بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ أَوْ أَكْنَنتُمْ فِي أَنفُسِكُمْ ۚ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ سَتَذْكُرُونَهُنَّ وَلَـٰكِن لَّا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّا أَن تَقُولُوا قَوْلًا مَّعْرُوفًا ۚ وَلَا تَعْزِمُوا عُقْدَةَ النِّكَاحِ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْكِتَابُ أَجَلَهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي أَنفُسِكُمْ فَاحْذَرُوهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿٢٣٥﴾
|
235. Wala
si dhambi juu yenu katika mliyotolea ishara kwayo ya kuposa wanawake
(walio katika eda) au mliyoficha katika nafsi zenu. Allaah Anajua kwamba
nyinyi mtawakumbuka lakini msifunge nao ahadi kisiri isipokuwa mseme
kauli ma’aruwf (inayoeleweka kawaida). Na wala msiazimie
kufunga ndoa mpaka muda ulioandikwa (katika eda) ufike mwisho wake. Na
jueni kwamba Allaah Anajua yaliyomo katika nafsi zenu basi jihadharini
Naye. Na jueni kwamba hakika Allaah ni Ghafuwrun-Haliym (Mwingi wa kughufuria - Mpole wa kuwavumilia waja).
|
لَّا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ مَا لَمْ تَمَسُّوهُنَّ أَوْ تَفْرِضُوا لَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَمَتِّعُوهُنَّ عَلَى الْمُوسِعِ قَدَرُهُ وَعَلَى الْمُقْتِرِ قَدَرُهُ مَتَاعًا بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُحْسِنِينَ ﴿٢٣٦﴾
|
236. Hakuna
dhambi kwenu mkiwatalaki wanawake ambao hamkuwagusa (hamkuwaingilia) au
kuwabainishia kwao mahari. Wapeni kiliwazo (kitoka nyumba) kwa mwenye
wasaa kadiri ya uwezo wake na mwenye dhiki kadiri ya uwezo wake.
Maliwaza kwa ma’aruwf (mujibu wa ada), ni haki kwa wafanyao ihsaan.
|
وَإِن
طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ وَقَدْ فَرَضْتُمْ
لَهُنَّ فَرِيضَةً فَنِصْفُ مَا فَرَضْتُمْ إِلَّا أَن يَعْفُونَ أَوْ
يَعْفُوَ الَّذِي بِيَدِهِ عُقْدَةُ النِّكَاحِ ۚ وَأَن تَعْفُوا أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۚ وَلَا تَنسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٣٧﴾
|
237. Na
mkiwatalaki kabla ya kuwagusa (kuwaingilia) na mkawa mmeshawabainishia
kwao mahari, basi (wapeni) nusu ya hayo mliyobainisha isipokuwa
wakisamehe (wanawake wenyewe) au asamehe yule ambaye fungamano ya ndoa
liko mikononi mwake. Na mkisamehe ni ukaribu zaidi ya taqwa. Na wala
msisahau fadhila baina yenu. Hakika Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona).
|
حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ ﴿٢٣٨﴾
|
238. Shikamaneni na Swalaah na (khasa) Swalaah ya katikati, na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu.
|
فَإِنْ خِفْتُمْ فَرِجَالًا أَوْ رُكْبَانًا ۖ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ﴿٢٣٩﴾
|
239. Mkikhofu
(adui basi swalini) hali mnakwenda au mmepanda (kipando). Mtakapokuwa
katika amani mdhukuruni Allaah (Swalini) kama Alivyokufunzeni yale
mliyokuwa hamuyajui.
|
وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا وَصِيَّةً لِّأَزْوَاجِهِم مَّتَاعًا إِلَى الْحَوْلِ غَيْرَ إِخْرَاجٍ ۚ فَإِنْ خَرَجْنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِي مَا فَعَلْنَ فِي أَنفُسِهِنَّ مِن مَّعْرُوفٍ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٤٠﴾
|
240. Na
wale waliofishwa miongoni mwenu wakaacha wake, wawausie kwa ajili ya
wake zao masurufu kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa. Watakapotoka wanawake
(wenyewe) basi hakuna dhambi juu yenu katika yale waliyofanya katika
nafsi zao katika ma’aruwf (yanayokubalika na shariy’ah). Na Allaah ni ‘Aziyzun-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).
|
وَلِلْمُطَلَّقَاتِ مَتَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُتَّقِينَ ﴿٢٤١﴾
|
241. Na wanawake waliotalakiwa wapewe kiliwazo (kitoka nyumba) kwa ma’aruwf (mujibu wa shariy’ah), ni haki juu ya wenye taqwa.
|
كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٢٤٢﴾
|
242. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na hukmu) Zake mpate kutia akilini.
|
أَلَمْ
تَرَ إِلَى الَّذِينَ خَرَجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَهُمْ أُلُوفٌ حَذَرَ
الْمَوْتِ فَقَالَ لَهُمُ اللَّـهُ مُوتُوا ثُمَّ أَحْيَاهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ ﴿٢٤٣﴾
|
243. Je,
hukuwaona wale walitoka kutoka majumbani mwao nao wakiwa ni maelfu
wakikhofu mauti, Allaah Akawaambia: “Kufeni” kisha Akawahuisha? Hakika
Allaah ni Mwenye fadhila juu ya watu lakini watu wengi hawashukuru.
|
وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٤٤﴾
|
244. Na piganeni katika njia ya Allaah, na jueni kwamba Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote daima - Mjuzi wa yote daima).
|
مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ أَضْعَافًا كَثِيرَةً ۚ وَاللَّـهُ يَقْبِضُ وَيَبْسُطُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٤٥﴾
|
245. Ni
nani atakayemkopesha Allaah mkopo mzuri kisha (Allaah) Amzidishie
mzidisho mwingi. Na Allaah Anakunja na Anakunjua, na Kwake mtarejeshwa.
|
أَلَمْ
تَرَ إِلَى الْمَلَإِ مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ مِن بَعْدِ مُوسَىٰ إِذْ
قَالُوا لِنَبِيٍّ لَّهُمُ ابْعَثْ لَنَا مَلِكًا نُّقَاتِلْ فِي سَبِيلِ
اللَّـهِ ۖ قَالَ هَلْ عَسَيْتُمْ إِن كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ أَلَّا تُقَاتِلُوا ۖ قَالُوا وَمَا لَنَا أَلَّا نُقَاتِلَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَقَدْ أُخْرِجْنَا مِن دِيَارِنَا وَأَبْنَائِنَا ۖ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ تَوَلَّوْا إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٢٤٦﴾
|
246. Je,
hukuwazingatia wakuu katika wana wa Israaiyl baada ya Muwsaa
walipomwambia Nabiy kwao: “Tutumie mfalme tupigane katika njia ya
Allaah.” (Nabiy) Akasema: “Huenda kuwa hamtapigana ikiwa mtaandikiwa
kupigana?” Wakasema: “Tuna nini hata tusipigane katika njia ya Allaah na
hali tumekwishatolewa kutoka majumbani mwetu na watoto wetu?”
Walipoandikiwa kupigana walikengeuka isipokuwa wachache miongoni mwao.
Na Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi) wa madhalimu.
|
وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ اللَّـهَ قَدْ بَعَثَ لَكُمْ طَالُوتَ مَلِكًا ۚ قَالُوا أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ الْمُلْكُ عَلَيْنَا وَنَحْنُ أَحَقُّ بِالْمُلْكِ مِنْهُ وَلَمْ يُؤْتَ سَعَةً مِّنَ الْمَالِ ۚ قَالَ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَاهُ عَلَيْكُمْ وَزَادَهُ بَسْطَةً فِي الْعِلْمِ وَالْجِسْمِ ۖ وَاللَّـهُ يُؤْتِي مُلْكَهُ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٤٧﴾
|
247. Na
Nabiy wao akawaambia: “Hakika Allaah Amekutumieni Twaaluwt kuwa ni
mfalme”. Wakasema: “Vipi yeye atakuwa na ufalme juu yetu, na hali sisi
tunastahiki zaidi ufalme kuliko yeye, na wala hakupewa wasaa katika
mali?” (Nabiy) Akasema: “Hakika Allaah Amemchagua juu yenu na
Akamuongezea ukunjufu katika elimu na kiwiliwili, na Allaah Humpa
Amtakaye ufalme Wake”. Na Allaah ni Waasi’un-‘Aliym (Mwenye wasaa - Mjuzi wa yote daima).
|
وَقَالَ
لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ آيَةَ مُلْكِهِ أَن يَأْتِيَكُمُ التَّابُوتُ
فِيهِ سَكِينَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَبَقِيَّةٌ مِّمَّا تَرَكَ آلُ مُوسَىٰ
وَآلُ هَارُونَ تَحْمِلُهُ الْمَلَائِكَةُ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٤٨﴾
|
248. Na Nabiy wao akawaambia: “Hakika ishara ya ufalme wake ni kwamba litakujieni sanduku ndani yake mna sakiynah (kituliza nyoyo) kutoka Rabb
(Mola) wenu na mabaki katika yale waliyoacha watu wa Muwsaa na watu wa
Haaruwn, (sanduku hilo) watalibeba Malaika.” Hakika katika hayo mna Aayah (ishara, dalili, buruhani) kwenu mkiwa ni Waumini.
|
فَلَمَّا
فَصَلَ طَالُوتُ بِالْجُنُودِ قَالَ إِنَّ اللَّـهَ مُبْتَلِيكُم بِنَهَرٍ
فَمَن شَرِبَ مِنْهُ فَلَيْسَ مِنِّي وَمَن لَّمْ يَطْعَمْهُ فَإِنَّهُ
مِنِّي إِلَّا مَنِ اغْتَرَفَ غُرْفَةً بِيَدِهِ ۚ فَشَرِبُوا مِنْهُ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۚ فَلَمَّا جَاوَزَهُ هُوَ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ قَالُوا لَا طَاقَةَ لَنَا الْيَوْمَ بِجَالُوتَ وَجُنُودِهِ ۚ قَالَ الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَاقُو اللَّـهِ كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿٢٤٩﴾
|
249. Alipoondoka
Twaaluwt na jeshi akasema: “Hakika Allaah Atakujaribuni kwa mto;
atakayekunywa humo, hatokuwa pamoja nami; na asiyekula hakika huyu yu
pamoja nami, isipokuwa atakayeteka mteko (mmoja) kwa mkono wake.” Basi
wakanywa kutoka humo isipokuwa wachache miongoni mwao. Alipouvuka yeye
na wale walioamini pamoja naye; wakasema: “Leo hatuna nguvu kabisa dhidi
ya Jaaluwt na jeshi lake.” Wakasema wale walio na yakini kwamba wao ni
wenye kukutana na Allaah: “Makundi mangapi machache yameshinda makundi
mengi kwa idhini ya Allaah? Na Allaah Yu pamoja na wenye kusubiri.”
|
وَلَمَّا
بَرَزُوا لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِ قَالُوا رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا
صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٥٠﴾
|
250. Na walipojitokeza kupambana na Jaaluwt na jeshi lake wakasema: “Rabb (Mola) wetu Tumiminie subira na ithibitishe miguu yetu na Tunusuru dhidi ya watu makafiri.
|
فَهَزَمُوهُم بِإِذْنِ اللَّـهِ وَقَتَلَ دَاوُودُ جَالُوتَ وَآتَاهُ اللَّـهُ الْمُلْكَ وَالْحِكْمَةَ وَعَلَّمَهُ مِمَّا يَشَاءُ ۗ
وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّـهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّفَسَدَتِ
الْأَرْضُ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ ذُو فَضْلٍ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٢٥١﴾
|
251. Wakawashinda
kwa idhini ya Allaah na Daawuwd akamuua Jaaluwt; na Allaah Akampa
(Daawuwd) ufalme na hikmah, na Akamfunza katika Aliyoyataka. Na lau
Allaah Asingelizuia watu baadhi yao kwa wengine, basi ingelifisidika
ardhi lakini Allaah ni Mwenye fadhila juu ya walimwengu.
|
تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۚ وَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٢٥٢﴾
|
252. Hizo ni Aayaat za Allaah Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki. Na hakika wewe ni miongoni mwa Rasuli. |
تِلْكَ الرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۘ مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ اللَّـهُ ۖ وَرَفَعَ بَعْضَهُمْ دَرَجَاتٍ ۚ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ
وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلَ الَّذِينَ مِن بَعْدِهِم مِّن بَعْدِ
مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَلَـٰكِنِ اخْتَلَفُوا فَمِنْهُم مَّنْ
آمَنَ وَمِنْهُم مَّن كَفَرَ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلُوا وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ ﴿٢٥٣﴾
|
253. Hao
ni Rasuli, Tumewafadhilisha baadhi yao juu ya baadhi. Miongoni mwao
(yuko) aliyesemeshwa na Allaah, na Akawapandisha baadhi yao vyeo. Na
Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام.
Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana wale (waliokuja) baada yao,
baada ya kuwajia hoja bayana. Lakini walikhitalifiana, basi miongoni
mwao (kuna) walioamini na miongoni mwao waliokufuru. Na lau Angelitaka
Allaah wasingelipigana lakini Allaah Anafanya Ayatakayo. |
يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِمَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ
أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خُلَّةٌ وَلَا شَفَاعَةٌ ۗ وَالْكَافِرُونَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٥٤﴾
|
254. Enyi mlioamini! Toeni katika Tulivyokuruzukuni kabla haijafika Siku (ambayo) hakutakuweko mapatano (ya fidya) humo wala urafiki wala shafaa’ah (uombezi wa aina yoyote ule). Na makafiri wao ndio madhalimu. |
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾
|
255. Allaah, hakuna ilaaha (muabudiwa) ila Yeye, Al-Hayyul-Qayyuwm (Aliyehai daima, Msimamizi wa kila kitu). Haumchukuwi usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai (anayeombea) mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kuzunguka chochote katika elimu Yake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Al-‘Aliyyul-‘Adhwiym (Mwenye Uluwa - Mwenye taadhima).
|
لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٥٦﴾
|
256. Hapana kulazimisha katika (kuingia) Dini, kwani imekwishabainika kati ya uongofu na upotofu. Basi atakayemkanusha twaaghuwt (miungu ya uongo) na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, na Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote daima - Mjuzi wa yote daima). |
اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ ۗ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥٧﴾
|
257. Allaah ni Waliyyu (Mlinzi, Msaidizi) wa wale walioamini, Anawatoa kutoka katika viza na kuwaingiza katika Nuru. Na wale waliokufuru awliyaa (marafiki, wasaidizi) wao ni twaaghuwt (miungu ya uongo) huwatoa kutoka katika Nuru na kuwaingiza katika viza. Hao ni watu wa Motoni wao humo ni wenye kudumu. |
أَلَمْ
تَرَ إِلَى الَّذِي حَاجَّ إِبْرَاهِيمَ فِي رَبِّهِ أَنْ آتَاهُ اللَّـهُ
الْمُلْكَ إِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّيَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ
قَالَ أَنَا أُحْيِي وَأُمِيتُ ۖ قَالَ إِبْرَاهِيمُ فَإِنَّ اللَّـهَ يَأْتِي بِالشَّمْسِ مِنَ الْمَشْرِقِ فَأْتِ بِهَا مِنَ الْمَغْرِبِ فَبُهِتَ الَّذِي كَفَرَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٢٥٨﴾
|
258. Je, hukumzingatia yule ambaye alimuhoji Ibraahiym kuhusu Rabb (Mola) wake kwa vile Allaah Alimpa ufalme; aliposema Ibraahiym: “Rabb
wangu ni Ambaye Anahuisha na Anafisha.” Akasema: “Mimi (pia) nahuisha
na nafisha.” Ibraahiym akasema: “Hakika Allaah Analileta jua (lichomoze)
kutoka Mashariki basi wewe lilete kutoka Magharibi.” Akapigwa na butwaa (na kufedheheka) yule aliyekufuru. Na Allaah Haongoi watu madhalimu. |
أَوْ كَالَّذِي مَرَّ عَلَىٰ قَرْيَةٍ وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا قَالَ أَنَّىٰ يُحْيِي هَـٰذِهِ اللَّـهُ بَعْدَ مَوْتِهَا ۖ فَأَمَاتَهُ اللَّـهُ مِائَةَ عَامٍ ثُمَّ بَعَثَهُ ۖ قَالَ كَمْ لَبِثْتَ ۖ قَالَ لَبِثْتُ يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ ۖ قَالَ بَل لَّبِثْتَ مِائَةَ عَامٍ فَانظُرْ إِلَىٰ طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمْ يَتَسَنَّهْ ۖ وَانظُرْ إِلَىٰ حِمَارِكَ وَلِنَجْعَلَكَ آيَةً لِّلنَّاسِ ۖ وَانظُرْ إِلَى الْعِظَامِ كَيْفَ نُنشِزُهَا ثُمَّ نَكْسُوهَا لَحْمًا ۚ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ قَالَ أَعْلَمُ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٥٩﴾
|
259. Au (zingatia mfano wa) kama yule aliyepita katika kijiji nacho ni kilichoporomoka kabisa juu ya mapaa yake (kuwa gofu); akasema (kwa mshangao): “Vipi Allaah Atahuisha hiki (kijiji) baada ya kufa kwake?” Basi Allaah Alimfisha miaka mia; kisha Akamfufua. Akasema:
(kwa kumuuliza) “Umekaa muda gani?” Akasema: “Nimekaa siku (moja) au
sehemu ya siku”. (Allaah) Akasema: “Bali umekaa miaka mia; basi kitazame
chakula chako na kinywaji chako hakikuharibika. Na mtazame punda wako;
na Tutakufanya (uwe) Aayah (dalili dhahiri, ishara) kwa watu.
Na itazame mifupa (ya punda) jinsi Tunavyoinyanyua, kisha Tunaivisha
nyama”. Basi ilipombainikia alisema: “Najua kwamba hakika Allaah juu ya
kila kitu ni Qadiyr (Muweza).”
|
وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ أَرِنِي كَيْفَ تُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِن ۖ قَالَ بَلَىٰ وَلَـٰكِن لِّيَطْمَئِنَّ قَلْبِي ۖ
قَالَ فَخُذْ أَرْبَعَةً مِّنَ الطَّيْرِ فَصُرْهُنَّ إِلَيْكَ ثُمَّ
اجْعَلْ عَلَىٰ كُلِّ جَبَلٍ مِّنْهُنَّ جُزْءًا ثُمَّ ادْعُهُنَّ
يَأْتِينَكَ سَعْيًا ۚ وَاعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٦٠﴾
|
260. Na (taja) aliposema Ibraahiym: “Rabb
(Mola) wangu nionyeshe vipi Unahuisha wafu?” (Allaah) Akasema: “Je
kwani huamini?” Akasema: “La! (Naamini) lakini (kwayo) moyo wangu upate
kutulia.” (Allaah) Akasema: “Basi chukua ndege wanne wazoeshe kwako,
(kisha uwachinje), kisha weka juu ya kila jabali katika hao (ndege)
sehemu yao; kisha waite watakujia mbio (wakiwa wameumbika upya nawe huku
unawaona wanavyojiunga viungo vyao kila mmoja); na jua kwamba hakika
Allaah ni ‘Aziyzun-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).
|
مَّثَلُ
الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ كَمَثَلِ
حَبَّةٍ أَنبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنبُلَةٍ مِّائَةُ حَبَّةٍ ۗ وَاللَّـهُ يُضَاعِفُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦١﴾
|
261. Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allaah ni kama mfano wa punje moja (ya mbegu) iliyotoa mashuke saba, katika kila shuke kuna punje mia. Na Allaah Humzidishia Amtakaye; na Allaah ni Waasi’un-‘Aliym (Mwenye wasaa - Mjuzi wa yote daima).
|
الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ لَا يُتْبِعُونَ مَا أَنفَقُوا مَنًّا وَلَا أَذًى ۙ لَّهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٢٦٢﴾
|
262. Wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allaah kisha hawafuatishii kwa waliyoyatoa masimbulizi wala udhia watapa ujira wao kwa Rabb (Mola) wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika. |
قَوْلٌ مَّعْرُوفٌ وَمَغْفِرَةٌ خَيْرٌ مِّن صَدَقَةٍ يَتْبَعُهَا أَذًى ۗ وَاللَّـهُ غَنِيٌّ حَلِيمٌ ﴿٢٦٣﴾
|
263. Kauli njema na msamaha ni bora kuliko swadaqah inayoifuata udhia. Na Allaah ni Ghaniyyun-Haliym (Mkwasi - Mpole wa kuwavumilia waja).
|
يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ
وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ
بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّمَّا كَسَبُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٢٦٤﴾
|
264. Enyi mlioamini! Msibatilishe swadaqah
zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali yake kwa
kujionyesha kwa watu, wala hamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Basi
mfano wake ni kama jabali juu yake pana udongo, kisha likapigwa (hilo jabali) na mvua kubwa ikaliacha tupu. Hawana uwezo juu ya lolote katika waliyoyachuma. Na Allaah Haongoi watu makafiri. |
وَمَثَلُ
الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ
وَتَثْبِيتًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ كَمَثَلِ جَنَّةٍ بِرَبْوَةٍ أَصَابَهَا
وَابِلٌ فَآتَتْ أُكُلَهَا ضِعْفَيْنِ فَإِن لَّمْ يُصِبْهَا وَابِلٌ
فَطَلٌّ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٦٥﴾
|
265. Na
mfano wa wale wanaotoa mali zao kutafuta Radhi za Allaah na
kujithibitisha nafsi zao ni kama mfano wa bustani iliyoko pahala
paliponyanyuka; ikafikiwa hiyo bustani na mvua kubwa, ikatoa mazao yake
maradufu, na (hata) kama haikufikiwa na mvua kubwa basi mvua ndogo (huitosheleza kutoa mazao). Na Allaah kwa muyatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona). |
أَيَوَدُّ
أَحَدُكُمْ أَن تَكُونَ لَهُ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ تَجْرِي
مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ لَهُ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ
وَأَصَابَهُ الْكِبَرُ وَلَهُ ذُرِّيَّةٌ ضُعَفَاءُ فَأَصَابَهَا إِعْصَارٌ
فِيهِ نَارٌ فَاحْتَرَقَتْ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢٦٦﴾
|
266. Je! Anapenda mmoja wenu kuwa na (kumiliki) bustani ya mitende na mizabibu ipitayo chini yake mito; anayo humo kila aina ya mazao; ukamfikia uzee, naye ana kizazi dhaifu; kisha ikapigwa (hiyo bustani) na kimbunga cha moto kikaiteketeza? Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat (ishara, hoja, zingatio n.k) kwenu mpate kutafakari. |
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِآخِذِيهِ إِلَّا أَن تُغْمِضُوا فِيهِ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿٢٦٧﴾
|
267. Enyi
mlioamini! Toeni katika vizuri mlivyochuma na katika ambayo
Tumekutoleeni kutoka katika ardhi. Na wala msikusudie vibaya kutoka humo
mkavitoa na hali nyinyi (wenyewe) si wenye kuvichukuwa isipokuwa kuvifumbia macho. Na jueni kwamba hakika Allaah ni Ghaniyyun-Hamiyd (Mkwasi - Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote daima). |
الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُم بِالْفَحْشَاءِ ۖ وَاللَّـهُ يَعِدُكُم مَّغْفِرَةً مِّنْهُ وَفَضْلًا ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦٨﴾
|
268. Shaytwaan anakutishieni ufukara na anakuamrisheni al-fahshaa (ubakhili, machafu n.k), na Allaah Anakuahidini maghfirah kutoka Kwake na fadhila. Na Allaah ni Waasi’un-‘Aliym (Mwenye wasaa - Mjuzi wa yote daima). |
يُؤْتِي الْحِكْمَةَ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُؤْتَ الْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٦٩﴾
|
269. Humpa hikmah Amtakaye. Na anayepewa hikmah basi kwa yakini huwa amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki (na kuwaidhika) isipokuwa wenye akili. |
وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ ۗ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿٢٧٠﴾
|
270. Na chochote mtoacho (katika njia ya Allaah) au mkiwekacho nadhiri, basi Allaah Anakijua. Na madhalimu hawana wa kuwanusuru. |
إِن تُبْدُوا الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِيَ ۖ وَإِن تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاءَ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّئَاتِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٧١﴾
|
271. Mkidhihirisha swadaqah basi ni vizuri hivyo,
na mkizificha na kuwapa mafakiri, basi hilo ni kheri kwenu. Na
Atakufutieni katika maovu yenu. Na Allaah kwa myatendayo ni Khabiyr (Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana) |
لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ اللَّـهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٢﴾
|
272. Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)
kuwaongoa, lakini Allaah Humwongoa Amtakaye. Na chochote cha kheri
mtoacho basi ni kwa ajili ya nafsi zenu. Na hamtoi ila kutaka Wajhi wa Allaah. Na chochote mtoacho katika kheri mtalipwa kamilifu nanyi hamtodhulumiwa. |
لِلْفُقَرَاءِ
الَّذِينَ أُحْصِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ ضَرْبًا
فِي الْأَرْضِ يَحْسَبُهُمُ الْجَاهِلُ أَغْنِيَاءَ مِنَ التَّعَفُّفِ
تَعْرِفُهُم بِسِيمَاهُمْ لَا يَسْأَلُونَ النَّاسَ إِلْحَافًا ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢٧٣﴾
|
273. (Swadaqah
ni) Kwa ajili ya mafakiri waliozuilika katika njia ya Allaah hawawezi
kwenda huku na kule katika ardhi (kutafuta rizki); asiyewajua huwadhania
kuwa ni matajiri kutokana na staha ya kujizua (kwao kuomba) unawatambua kwa alama zao, hawaombi watu kwa ung’ang’anizi. Na chochote mtoacho katika kheri basi Allaah kwacho ni ‘Aliym (Mjuzi). |
الَّذِينَ
يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ سِرًّا وَعَلَانِيَةً
فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ
يَحْزَنُونَ ﴿٢٧٤﴾
|
274. Wale wanaotoa mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri; watapata ujira wao kwa Rabb (Mola) wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika. |
الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا ۗ وَأَحَلَّ اللَّـهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا ۚ فَمَن جَاءَهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىٰ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَنْ عَادَ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٧٥﴾
|
275. Wale wanaokula ribaa
hawatosimama (Siku ya Qiyaamah) ila kama anavyosimama yule aliyezugwa
na shaytwaan kwa kuguswa. Hivyo kwa sababu wao wamesema: “Hakika
biashara (kuuza na kununua) ni kama ribaa.” Na Allaah Amehalalisha biashara na Ameharamisha ribaa. Basi atakayefikiwa na mawaidha kutoka kwa Rabb (Mola) wake akakoma (kula ribaa); basi ni yake yale yaliyopita, na hukumu yake iko kwa Allaah. Na atakayerudia (ribaa) basi hao ni watu wa Motoni, wao humo ni wenye kudumu. |
يَمْحَقُ اللَّـهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ ﴿٢٧٦﴾
|
276. Allaah Huifuta (baraka mali ya) ribaa na Huzibariki swadaqah. Na Allaah Hapendi kila kafiri apapiae madhambi. |
إِنَّ
الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ
وَآتَوُا الزَّكَاةَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ
عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٢٧٧﴾
|
277. Hakika wale walioamini na wakatenda mazuri na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah; watapata ujira kutoka kwa Rabb (Mola) wao na wala hakuna khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika. |
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٧٨﴾
|
278. Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na acheni yaliyobakia katika ribaa ikiwa nyinyi ni Waumini. |
فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٩﴾
|
279. Na
msipofanya basi tangazeni vita kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake. Na
mkitubu basi mtapata rasilmali zenu msidhulumu na wala msidhulumiwe.
|
وَإِن كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيْسَرَةٍ ۚ وَأَن تَصَدَّقُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٨٠﴾
|
280. Na ikiwa (mdaiwa) ni mwenye hali ngumu, basi (mdai) angoje muda wa kufarijika (anayemdai). Na mkitoa swadaqah (deni mnalodai) basi ni kheri kwenu mkiwa mnajua. |
وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّـهِ ۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٨١﴾
|
281. Na iogopeni Siku mtayorejeshwa humo kwa Allaah, kisha kila nafsi italipwa kamilifu iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa. |
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيْنٍ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَاكْتُبُوهُ ۚ وَلْيَكْتُب بَّيْنَكُمْ كَاتِبٌ بِالْعَدْلِ ۚ وَلَا يَأْبَ كَاتِبٌ أَن يَكْتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ اللَّـهُ ۚ فَلْيَكْتُبْ وَلْيُمْلِلِ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ وَلَا يَبْخَسْ مِنْهُ شَيْئًا ۚ
فَإِن كَانَ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ سَفِيهًا أَوْ ضَعِيفًا أَوْ لَا
يَسْتَطِيعُ أَن يُمِلَّ هُوَ فَلْيُمْلِلْ وَلِيُّهُ بِالْعَدْلِ ۚ وَاسْتَشْهِدُوا شَهِيدَيْنِ مِن رِّجَالِكُمْ ۖ
فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَأَتَانِ مِمَّن
تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاءِ أَن تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ
إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَىٰ ۚ وَلَا يَأْبَ الشُّهَدَاءُ إِذَا مَا دُعُوا ۚ وَلَا تَسْأَمُوا أَن تَكْتُبُوهُ صَغِيرًا أَوْ كَبِيرًا إِلَىٰ أَجَلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ وَأَقْوَمُ لِلشَّهَادَةِ وَأَدْنَىٰ أَلَّا تَرْتَابُوا ۖ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً حَاضِرَةً تُدِيرُونَهَا بَيْنَكُمْ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَلَّا تَكْتُبُوهَا ۗ وَأَشْهِدُوا إِذَا تَبَايَعْتُمْ ۚ وَلَا يُضَارَّ كَاتِبٌ وَلَا شَهِيدٌ ۚ وَإِن تَفْعَلُوا فَإِنَّهُ فُسُوقٌ بِكُمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّـهُ ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٨٢﴾
|
282. Enyi
mlioamini! Mtakapokopeshana deni kwa muda maalumu basi liandikeni. Na
aandike baina yenu mwandishi kwa uadilifu. Na wala asikatae mwandishi
kuandika kama Allaah Alivyomfunza. Basi aandike na atamke (maneno
yanayoandikwa) yule ambaye ana haki (mdai) na amuogope Allaah, Rabb (Mola)
wake, na wala asipunguze humo kitu chochote. Basi ikiwa yule ambaye ana
haki amepumbaa (hajakomaa kiakili) au dhaifu (mnyonge), au hawezi
kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe msimamizi wake kwa uadilifu. Na
mshuhudishe mashahidi wawili wanaume miongoni mwenu. Na ikiwa hakuna
wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika wale
mnaowaridhia miongoni mwa mashahidi, ili kama mmoja wao (hao wanawake
wawili) akipotea,
basi mmoja wao atamkumbusha mwengine. Na mashahidi wasikatae
watapoitwa. Na wala msichukie kuliandika (deni likiwa) dogo au kubwa
mpaka muda wake. Hivyo kwenu ndiyo aqswatw (uadilifu upasavyo) mbele ya Allaah na ndio imara (unyoofu) zaidi kwa ushahidi; na ni karibu zaidi ili
msiwe na shaka; isipokuwa itakapokuwa biashara taslimu
(mkono-kwa-mkono) mnayoiendesha baina yenu, basi si dhambi kwenu
msipoiandika. Na shuhudisheni mnapouziana. Na wala asidhuriwe mwandishi
wala shahidi; na mkifanya basi hakika huo ni ufasiki kwenu. Na mcheni
Allaah, na Allaah Anakufunzeni, na Allaah kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi). |
وَإِن كُنتُمْ عَلَىٰ سَفَرٍ وَلَمْ تَجِدُوا كَاتِبًا فَرِهَانٌ مَّقْبُوضَةٌ ۖ فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ ۗ وَلَا تَكْتُمُوا الشَّهَادَةَ ۚ وَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ ﴿٢٨٣﴾
|
283. Na
mkiwa safarini na hamkumpata mwandishi, basi (mdai) akabidhiwe rahani.
Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule
ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake; na amche Allaah, Rabb (Mola) wake; na wala msifiche ushahidi; na mwenye kuuficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Allaah kwa mnayoyatenda ni ‘Aliym (Mjuzi). |
لِّلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَإِن تُبْدُوا مَا فِي أَنفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُم بِهِ اللَّـهُ ۖ فَيَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٨٤﴾
|
284. Ni
vya Allaah Pekee vyote viliomo mbinguni na viliomo ardhini. Na
mkidhihirisha yale yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkiyaficha; basi
Allaah Atakuhesabuni kwayo. Humghufuria Amtakaye na Humuadhibu Amtakaye.
Na Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza). |
آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾
|
285. Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb (Mola) wake na Waumini (pia wameamini). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rasuli Wake. (Nao husema): “Hatutafautishi baina ya yeyote kati ya Rasuli Wake”. Na wakasema: “Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu na Kwako ni mahali pa kuishia.” |
لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٨٦﴾
|
286. Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata (malipo ya mazuri) iliyoyachuma, na ni dhidi yake (kwa maovu) iliyojichumia. “Rabb (Mola) wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Rabb wetu, Usitubebeshe mzigo kama Ulivyoubebesha juu ya wale waliokuwa kabla yetu. Rabb wetu, Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe ni Mawlaa (Mlezi, Mlinzi, Msimamizi) wetu, basi Tunusuru dhidi ya watu makafiri.
|
|