024 - Hadiyth Ya 24: Uongo Unaruhusiwa Katika Kupatanisha Waliogombana Na Vitani

024 - Hadiyth Ya 24: Uongo Unaruhusiwa Katika Kupatanisha Waliogombana Na Vitani


 
 عَنْ أُمَّ كُلْثُومٍ بِنْتَ عُقْبَةَ (رضي الله عنها) قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم) يَقُولُ: ((لَيْسَ الْكَذَّابُ الَّذِي يُصْلِحُ بَيْنَ النَّاسِ فَيَنْمِي خَيْرًا)) متفق عليه. وفي رواية مسلم زيادة  َقَالَتْ: وَلَمْ أَسْمَعْهُ يُرَخِّصُ فِي شَيْءٍ مِمَّا يَقُولُ النَّاسُ إلاَّ فِي ثَلاَثٍ: تَعْنِي الْحَرْبَ, والإصْلاَحَ بَيْنَ النَّاس, وَحَدِيثَ الرَّجُلِ امْرَأَتَهُ وَحَدِيث الْمَرْأَةِ زَوْجَهَا
 
Imepokelewa kutoka kwa Ummu Kulthuum bint ‘Uqbah (رضي الله عنها) amesema: Nilimsikia Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Hajasema uongo yule mwenye kusuluhisha baina ya watu akawa anasambaza [habari ya] kheri, au anasema kheri)).[1] Na katika riwaya ya Muslim kuna ziada inayosema: Akasema “wala sikumsikia akiruhusu chochote katika uongo wanaosema watu isipokuwa katika mambo matatu”. Yaani katika vita, kusuluhisha baina ya watu, mwanamume kuzungumza na mkewe na mke kuzungumza na mumewe.”
 
Mafunzo Na Hidaaya
 
  1. Uislamu umeharamisha kusema uongo isipokuwa katika hali tatu zilizotajwa.
 
  1. Umuhimu wa kuweko amani baina ya jamii ya Kiislamu kiasi kwamba kusema uongo ambao ni dhambi kubwa umehalalishwa kwayo. [Rejea Hadiyth namba 94].
 
  1. Fadhila za kusuluhisha waliokhasimikiana ni kubwa mno.
 
 
لَّا خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَاحٍ بَيْنَ النَّاسِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١١٤﴾
 
Hakuna kheri katika minong’ono yao mingi isipokuwa anayeamrisha swadaqah, au (kumarisha) ma’aruwf (mema), au kupatanisha baina ya watu. Na atakayefanya hivyo kutaka Radhi za Allaah, basi Tutampa ujira mkubwa[2]
 
  1. Umuhimu wa mapatano na amani baina ya mke na mume na jamii kwa ujumla [An-Nisaa 4: 128, Al-Anfaal 8: 1, Al-Hujuraat 49: 10].
 
  1. Uislamu ni Dini ya amani, na kuamkiana kwa maamkizi ya Kiislamu ni sababu mojawapo ya kuleta amani na kumwingiza Muislamu Peponi. [Rejea Hadiyth namba 42, 73].
 
 



[1]  Al-Bukhaariy na Muslim.
[2]  An-Nisaa (4: 114).