At-Takwiyr (81)

سُورَةُ  التَّكْوِير
At-Takwiyr (81)

(Imeteremka Makka)

 
Katika Sura hii yanaelezwa yatakayo tokea wakati wa Saa ya Kiyama na baada yake, na yanaelezwa ya kuonyesha dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu, na kutilia mkazo cheo cha Qur'ani tukufu, na kupinga madai ya uzushi katika Qur'ani, na kumtakasa Mtume s.a.w. na tuhuma za wazimu, na kuwatisha na kuwaonya hao wanao endelea na upotovu, na inataka yaangaliwe mazingatio yaliyomo katika Qur'ani ambayo yatawafaa watu wenye kusimama msimamo wa sawa, na inarudisha mambo yote ya watu kwenye mapenzi ya Mola Mlezi wa walimwengu wote.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ﴿١﴾

1. Jua litakapokunjwa kunjwa.

وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ ﴿٢﴾

2. Na nyota zitapoanguka na kupuputika.

وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ ﴿٣﴾

3. Na majabali yatakapoendeshwa.

وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ ﴿٤﴾

4. Na ngamia wenye mimba pevu watakapopuuzwa.

وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ ﴿٥﴾

5. Na wanyama mwitu watakapokusanywa.

وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ ﴿٦﴾

6. Na bahari zitakapowashwa moto.

وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ ﴿٧﴾

7. Na nafsi zitakapounganishwa (na miili yake).


وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ ﴿٨﴾

8. Na mtoto wa kike aliyezikwa akiwa hai atakapoulizwa.

بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ ﴿٩﴾

9. Kwa dhambi gani aliuliwa?

وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ ﴿١٠﴾

10. Na swahifa zitakapotandazwa.

وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ ﴿١١﴾

11. Na mbingu zitakapotanduliwa.

وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ ﴿١٢﴾

12. Na (Moto wa) Al-Jahiym utakapochochewa.

وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ ﴿١٣﴾

13. Na Jannah itakaposogezwa (karibu).

عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا أَحْضَرَتْ ﴿١٤﴾

14. (Hapo kila) Nafsi itajua yale iliyoyahudhurisha (ya ‘amali njema au ovu).

فَلَا أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ ﴿١٥﴾

15. Basi Naapa kwa (sayari) zinazorudi nyuma (zinapotea mchana na zinadhihirika usiku).

الْجَوَارِ الْكُنَّسِ ﴿١٦﴾
16. Zinazotembea na kujificha.

وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ ﴿١٧﴾

17. Na usiku unapoondoka.

وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ ﴿١٨﴾

18. Na asubuhi inapopumua.

إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ﴿١٩﴾

19. Hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni kauli (aliyokuja nayo) Mjumbe mtukufu (Jibriyl).

ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ ﴿٢٠﴾

20. Mwenye nguvu na cheo kitukufu kwa (Allaah) Mwenye ‘Arsh.

مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ ﴿٢١﴾

21. Anayetiiwa (na Malaika wenziwe huko mbinguni), tena (ni) mwaminifu.

وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ ﴿٢٢﴾

22. Na hakuwa swahibu yenu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) majnuni.

وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ ﴿٢٣﴾

23. Na kwa yakini alimuona (Jibriyl) katika upeo wa macho bayana.

وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِينٍ ﴿٢٤﴾

24. Naye si mzuiaji wa (kuelezea mambo ya) ghayb.


وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ ﴿٢٥﴾

25. Na hii (Qur-aan) si kauli ya shaytwaan aliyefukuzwa (kuwekwa mbali na Rahmah ya Allaah).

فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ ﴿٢٦﴾

26. Basi mnakwenda wapi?

إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ ﴿٢٧﴾

27. Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa ni dhikri (ukumbusho, mawaidha na kumbukumbu) kwa walimwengu.

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ ﴿٢٨﴾

28. Kwa yule atakaye miongoni mwenu anyooke (katika njia ya haki).

وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٩﴾

29. Na hamtotaka isipokuwa Atake Allaah Rabb (Mola) wa walimwengu.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com