Al-Inshiqaaq (84)


سُورَةُ  الإِنْشِقَاق
Al-Inshiqaaq (84)

(Imeteremka Makka)

Sura hii imetaja baadhi ya ishara za Saa ya Kiyama, na kunyenyekea ardhi na mbingu kufuata atakavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na imefahamisha kwamba mtu anachungwa ende akakutane na Mola wake Mlezi, na kwamba vitendo vyake vimeandikwa katika daftari atakalo kuja likuta. Basi mwenye kulipokea kwa mkono wake wa kulia, hisabu yake itakuwa nyepesi. Na mwenye kulipokea kwa mkono wa kushoto atayayatika kuipata adhabu na kuingia Motoni. Tena Mwenyezi Mungu Subhanahu ameapa kwa Ishara ambazo zinashuhudia uweza wake, na ambazo zinaitia imani ya kufufuliwa. Lakini juu ya hayo walio kufuru hawaamini, wala hawaizingatii Qur'ani, wala hawazifuati hukumu zake. Kisha Sura inakhitimisha kwa kuonya kwamba Mwenyezi Mungu anayajua wanayo dhamiria, na kwamba Yeye amekwisha waandalia adhabu iliyo chungu, kama alivyo waandalia Waumini ujira wa daima usio katika.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ﴿١﴾

1. Mbingu zitakapopasuka. 

وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ﴿٢﴾

2. Na zikamsikia (na kumtii) Rabb (Mola) wake na zimepaswa (kufanya hivyo).

وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ ﴿٣﴾

3. Na ardhi itakapotandazwa.

وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ ﴿٤﴾

4. Na ikatupilia mbali vile (vyote) vilivyomo ndani yake, na ikawa tupu.

وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ﴿٥﴾

5. Na ikamsikia (na kumtii) Rabb (Mola) wake na imepaswa (kufanya hivyo).

يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدْحًا فَمُلَاقِيهِ ﴿٦﴾

6. Ee insani! Hakika wewe unasumbuka kwa tabu kubwa kuelekea kwa Rabb (Mola) wako, na ni mwenye kukutana Naye.

فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ ﴿٧﴾

7. Basi ama yule atakayepewa kitabu chake kuliani mwake.

فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا ﴿٨﴾

8. Atahesabiwa hesabu nyepesi.

وَيَنقَلِبُ إِلَىٰ أَهْلِهِ مَسْرُورًا ﴿٩﴾

9. Na atageuka kwa ahli zake (akiwa) mwenye furaha.

وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاءَ ظَهْرِهِ ﴿١٠﴾

10. Na ama yule atakayepewa kitabu chake nyuma ya mgongo wake.

فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا ﴿١١﴾

11. Ataomba maangamizi.

وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا ﴿١٢﴾

12. Na ataingia aungue (Moto wa) Sa’iyraa (uwakao kwa nguvu).”

إِنَّهُ كَانَ فِي أَهْلِهِ مَسْرُورًا ﴿١٣﴾

13. Hakika yeye alikuwa katika ahli zake (ni mwenye) furaha.

إِنَّهُ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ ﴿١٤﴾

14. Hakika yeye alidhani kwamba hatorudi (kwa Allaah).

بَلَىٰ إِنَّ رَبَّهُ كَانَ بِهِ بَصِيرًا ﴿١٥﴾

15. Hapana! Hakika Rabb (Mola) wake daima alikuwa kwa yeye Baswiyraa (Mwenye kuona).

فَلَا أُقْسِمُ بِالشَّفَقِ ﴿١٦﴾

16. Basi Naapa kwa mng’aro wa kukuchwa jua.

وَاللَّيْلِ وَمَا وَسَقَ ﴿١٧﴾

17. Na usiku na yale (yote) yanayogubika (kizani mwake).

وَالْقَمَرِ إِذَا اتَّسَقَ ﴿١٨﴾

18. Na mwezi unapokamilika.

لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ ﴿١٩﴾

19. Bila shaka mtapitia hali baada ya hali (hatua kwa hatua).

فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠﴾
20. Basi wana nini hawaamini?

وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ ۩ ﴿٢١﴾

21. Na wanaposomewa Qur-aan, hawasujudu.

بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُكَذِّبُونَ ﴿٢٢﴾

22. Bali wale waliokufuru wanakadhibisha.

وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ ﴿٢٣﴾

23. Na Allaah Anajua zaidi yale wanayoyakusanya (ya siri).

فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٢٤﴾

24. Basi wabashirie adhabu iumizayo.

إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ﴿٢٥﴾

25. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mazuri, watapata ujira usiokatika.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com