Hadiyth Ya 39 Nimewatayarishia Pepo Waja Wangu Wema




  عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَعْدَدْتُ لِعِبَادِي الصَّالِحِينَ مَا لَا عَيْنٌ رَأَتْ وَلَا أُذُنٌ سَمِعَتْ وَلَا خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ)) قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ اقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: (( فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ)) البخاري, مسلم, الترمذي وابن ماجه


Kutoka kwa Abu Hurayrahرضي الله عنه  ambaye amesema: Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: ((Allaah تَبَارَكَ وَتَعَالَى Amesema: ((Nimewatayarishia waja Wangu wema kile ambacho jicho lolote halijapata kuona na sikio lolote halijapata kusikia na wala haijapata kupita katika moyo wa binaadamu)) Akasema Abu Hurayrah: Kwa hivyo, soma ukitaka: ((Nafsi yeyote haijui waliofichiwa katika hayo yanayofurahisha macho huko Peponi)) [As-Sajdah: 32:17] [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah]