Al-Mursalaat (77)


سُورَةُ  الْمُرْسَلاَت
Al-Mursalaat (77)
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَالْمُرْسَلَاتِ عُرْفًا ﴿١﴾

1. Naapa kwa pepo zitumwazo moja baada ya moja.

فَالْعَاصِفَاتِ عَصْفًا ﴿٢﴾

2. Kisha (Naapa) kwa pepo zinazovuma kwa dhoruba.

وَالنَّاشِرَاتِ نَشْرًا ﴿٣﴾

3. Na (Naapa) kwa pepo zinazotawanya (mawingu na mvua) mtawanyiko.

فَالْفَارِقَاتِ فَرْقًا ﴿٤﴾

4. Na (Naapa) kwa (Malaika) wanaopambanua mpambanuo.

فَالْمُلْقِيَاتِ ذِكْرًا ﴿٥﴾

5. Kisha (Naapa) kwa (Malaika) wanaopeleka dhikri (maneno ya Allaah).

عُذْرًا أَوْ نُذْرًا ﴿٦﴾

6. Kwa udhuru au kuonya.

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَاقِعٌ ﴿٧﴾

7. Hakika yale mliyoahidiwa bila shaka yatatokea tu!

فَإِذَا النُّجُومُ طُمِسَتْ ﴿٨﴾

8. Pale nyota zitakapofutwa (mwanga wake).

وَإِذَا السَّمَاءُ فُرِجَتْ ﴿٩﴾

9. Na (pale) mbingu zitakapopasuliwa.

وَإِذَا الْجِبَالُ نُسِفَتْ ﴿١٠﴾
10. Na (pale) majabali yatakapong’olewa.

وَإِذَا الرُّسُلُ أُقِّتَتْ ﴿١١﴾

11. Na (pale) Rasuli watakapopangwa kwa ratiba (wakati wake maalumu).


لِأَيِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ ﴿١٢﴾

12. Kwa siku gani hiyo iliyokawilishwa?

لِيَوْمِ الْفَصْلِ ﴿١٣﴾

13. Kwa ajili ya siku ya hukumu.

وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الْفَصْلِ ﴿١٤﴾

14. Na nini kitakachokujulisha siku ya hukumu?

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١٥﴾

15. Ole siku hiyo (ya Qiyaamah) kwa wakadhibishaji.

أَلَمْ نُهْلِكِ الْأَوَّلِينَ ﴿١٦﴾

16. Je, kwani Hatukuangamiza (watu wa) awali?

ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ الْآخِرِينَ ﴿١٧﴾

17. Kisha Tukawafuatilishia wengineo?

كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ ﴿١٨﴾

18. Hivyo ndivyo Tutakavyowafanya wakhalifu.

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١٩﴾

19. Ole siku hiyo (ya Qiyaamah) kwa wakadhibishaji.

أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّاءٍ مَّهِينٍ ﴿٢٠﴾

20. Je, kwani Hatukukuumbeni kwa maji dhalilifu (manii)?

فَجَعَلْنَاهُ فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ ﴿٢١﴾

21. Kisha Tukayaweka katika mahali pa utulivu.

إِلَىٰ قَدَرٍ مَّعْلُومٍ ﴿٢٢﴾

22. Mpaka kadirio maalumu.

فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ الْقَادِرُونَ ﴿٢٣﴾

23. Tukakadiria, basi ni wazuri walioje (Sisi) Wakadiriaji.

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٢٤﴾

24. Ole siku hiyo (ya Qiyaamah) kwa wakadhibishaji.

أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ كِفَاتًا ﴿٢٥﴾

25. Je, kwani Hatukufanya ardhi kuwa ni chombo cha kukusanya?

أَحْيَاءً وَأَمْوَاتًا ﴿٢٦﴾

26. (Kukusanya) Vilivyo hai na wafu?

وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَاتٍ وَأَسْقَيْنَاكُم مَّاءً فُرَاتًا ﴿٢٧﴾

27. Na Tukaweka humo milima mirefu thabiti, na Tukakunywesheni maji matamu?

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٢٨﴾

28. Ole siku hiyo (ya Qiyaamah) kwa wakadhibishaji.

انطَلِقُوا إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ ﴿٢٩﴾

29. (Wataambiwa): “Nendeni kwenye yale mliyokuwa mkiyakadhibisha.


انطَلِقُوا إِلَىٰ ظِلٍّ ذِي ثَلَاثِ شُعَبٍ ﴿٣٠﴾

30.  “Nendeni kwenye kivuli chenye sehemu tatu.”

لَّا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِي مِنَ اللَّـهَبِ ﴿٣١﴾

31. (Kivuli hicho) hakiwafuniki, na wala hakiwakingi na mwako wa Moto.

إِنَّهَا تَرْمِي بِشَرَرٍ كَالْقَصْرِ ﴿٣٢﴾

32. Hakika (huo Moto) hurusha macheche (makubwa na marefu) kama makasri.

كَأَنَّهُ جِمَالَتٌ صُفْرٌ ﴿٣٣﴾

33. Kama kwamba ngamia wa rangi ya manjano.

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٣٤﴾

34. Ole siku hiyo (ya Qiyaamah) kwa wakadhibishaji.

هَـٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ ﴿٣٥﴾

35. Siku hii hawatotamka.

وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ ﴿٣٦﴾

36. Na wala hawatopewa idhini, ili watoe nyudhuru.

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٣٧﴾

37. Ole siku hiyo (ya Qiyaamah) kwa wakadhibishaji.

هَـٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ ۖ جَمَعْنَاكُمْ وَالْأَوَّلِينَ ﴿٣٨﴾

38. Hii ni siku ya hukumu. Tumekukusanyeni pamoja na (watu) wa awali.

فَإِن كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ ﴿٣٩﴾

39. Ikiwa mnayo njama yoyote ile basi Nifanyieni.

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٤٠﴾
40. Ole siku hiyo (ya Qiyaamah) kwa wakadhibishaji.


إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ ﴿٤١﴾

41. Hakika wenye taqwa wamo katika vivuli na chemchemu.

وَفَوَاكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na (kila aina ya) matunda katika yale wanayoyatamani.

كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٤٣﴾

43. (Wataambiwa): “Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda.”

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٤٤﴾

44.  Hakika hivyo ndivyo Tunavyowalipa watendao wema.

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٤٥﴾

45. Ole siku hiyo (ya Qiyaamah) kwa wakadhibishaji.


كُلُوا وَتَمَتَّعُوا قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجْرِمُونَ ﴿٤٦﴾

46. (Makafiri nao wataambiwa): “Kuleni na stareheni kidogo (hapa duniani), hakika nyinyi ni wahalifu.”


وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٤٧﴾

47. Ole siku hiyo (ya Qiyaamah) kwa wakadhibishaji.


وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ارْكَعُوا لَا يَرْكَعُونَ ﴿٤٨﴾

48. Na (walikuwa duniani) wakiambiwa “Rukuuni (Swalini),” hawakuwa wakirukuu.

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿٤٩﴾

49. Ole siku hiyo (ya Qiyaamah) kwa wakadhibishaji.

فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ ﴿٥٠﴾

50. Basi hadiyth gani baada ya hii (Qur-aan) wataiamini?

 


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com