Al-Muddathir (74)


سُورَةُ  الْمُدَّثِّر
Al-Muddathir (74)
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ ﴿١﴾

1. Ee uliyejigubika.

قُمْ فَأَنذِرْ ﴿٢﴾
2. Simama na uonye

وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ ﴿٣﴾

3. Na Rabb (Mola) wako mtukuze (kwa takbira).

وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ ﴿٤﴾

4. Na nguo zako zitwaharishe.

وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ ﴿٥﴾

5. Na Ar-Rujz (masanamu) epukana nayo.


وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ ﴿٦﴾

6. Na wala usifanye ihsani kwa ajili ya kutaraji kukithirishiwa (manufaa ya kidunia).

وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ ﴿٧﴾

7. Na kwa ajili ya Rabb (Mola) wako subiri.

فَإِذَا نُقِرَ فِي النَّاقُورِ ﴿٨﴾

8. Itakapopulizwa katika baragumu.

فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ ﴿٩﴾

9. Basi hiyo itakuwa ni Siku ngumu.

عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ ﴿١٠﴾

10. Kwa makafiri (siku hiyo haitokuwa) nyepesi.

ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا ﴿١١﴾

11. Niache Mimi na yule Niliyemuumba Pekee (bila mali wala watoto).

وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَّمْدُودًا ﴿١٢﴾

12. Na Nikamjaalia mali tele.

وَبَنِينَ شُهُودًا ﴿١٣﴾

13. Na watoto wanaoonekana.

وَمَهَّدتُّ لَهُ تَمْهِيدًا ﴿١٤﴾

14. Na Nikamtandazia (kila kitu) maandalizi mazuri.

ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ ﴿١٥﴾

15. Kisha anatumaini Nimuongezee.

كَلَّا ۖ إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا ﴿١٦﴾

16. Hasha!  Hakika yeye amekuwa anidi kwa Aayaat Zetu.

سَأُرْهِقُهُ صَعُودًا ﴿١٧﴾

17. Nitamshurutisha adhabu ya kumgandamiza.

إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ ﴿١٨﴾

18. Hakika yeye ametafakari na akakadiria.

فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ ﴿١٩﴾

19. Na akaangamia namna vile alivyokadiria.

ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ ﴿٢٠﴾

20. Kisha akaangamia namna alivyokadiria.

ثُمَّ نَظَرَ ﴿٢١﴾

21. Kisha akatazama.

ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ ﴿٢٢﴾

22. Kisha akakunja kipaji na akafinya uso kwa ghadhabu.

ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ ﴿٢٣﴾
23. Kisha akaipa mgongo (haki) na akatakabari.

فَقَالَ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ ﴿٢٤﴾

24. Akasema: “Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa ni sihiri inayonukuliwa (na watu).

إِنْ هَـٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ ﴿٢٥﴾

25. “Hii si chochote isipokuwa ni kauli ya mtu.

سَأُصْلِيهِ سَقَرَ ﴿٢٦﴾

26. Nitamuingiza kwenye (Moto wa) Saqar.

وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ ﴿٢٧﴾

27. Na nini kitakachokujulisha huo (Moto wa) Saqar.

لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ ﴿٢٨﴾

28.  Haubakishi na wala hauachi.

لَوَّاحَةٌ لِّلْبَشَرِ ﴿٢٩﴾

29. Unababua ngozi.

عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ ﴿٣٠﴾

30. Juu yake wako (walinzi) kumi na tisa.

وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلَّا مَلَائِكَةً ۙ وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا ۙ وَلَا يَرْتَابَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ ۙ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ ۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ ﴿٣١﴾

31. Na Hatukuweka walinzi wa Moto isipokuwa ni Malaika, na Hatukuifanya idadi yao (hiyo ya kumi na tisa) isipokuwa iwe (ni) jaribio kwa wale waliokufuru; ili wayakinishe wale waliopewa Kitabu, na iwazidishie iymaan wale walioamini; na wala wasitie shaka wale waliopewa Kitabu na Waumini; na ili wale waliokuwa na maradhi nyoyoni mwao (ya unafiki) na makafiri waseme: “Allaah Ametaka nini kwa mfano huu?” Hivyo ndivyo Allaah Anavyompotoa Amtakaye (kwa vile ametaka mwenyewe kupotoka), na Anamuongoa Amtakaye. Na hakuna ajuaye majeshi ya Rabb (Mola) wako isipokuwa Yeye Pekee, na huu (Moto) haukuwa isipokuwa ni ukumbusho kwa mtu.  

كَلَّا وَالْقَمَرِ ﴿٣٢﴾

32. Hasha! Naapa kwa mwezi.

وَاللَّيْلِ إِذْ أَدْبَرَ ﴿٣٣﴾

33. Na usiku unapogeuka.

وَالصُّبْحِ إِذَا أَسْفَرَ ﴿٣٤﴾

34. Na asubuhi inapopambazuka.

إِنَّهَا لَإِحْدَى الْكُبَرِ ﴿٣٥﴾
35. Hakika huo (Moto) bila shaka ni moja kati ya (balaa) kubwa kabisa.

نَذِيرًا لِّلْبَشَرِ ﴿٣٦﴾

36. Ni onyo kwa mtu.

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ ﴿٣٧﴾

37. Kwa atakaye miongoni mwenu kutakadamu (mbele kutenda ‘amali njema), au kuchelewa (nyuma kwa kutenda madhambi).

كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ ﴿٣٨﴾

38. Kila nafsi iko katika rehani kwa yale iliyoyachuma.

إِلَّا أَصْحَابَ الْيَمِينِ ﴿٣٩﴾

39. Isipokuwa watu wa kuliani.

فِي جَنَّاتٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٤٠﴾

40. Katika Jannaat wanaulizana.


عَنِ الْمُجْرِمِينَ ﴿٤١﴾

41. Kuhusu wahalifu.

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ ﴿٤٢﴾

42. (Watawauliza): “Nini kilichokuingizeni katika (Moto wa) Saqar?”


قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ ﴿٤٣﴾

43. Watasema: “Hatukuwa miongoni mwa wanaoswali.

وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ ﴿٤٤﴾

44. “Na wala hatukulisha masikini.

وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ ﴿٤٥﴾

45. “Na tulikuwa tunatumbukia kwenye upuuzi pamoja na wanaotumbukia upuuzini.

وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ ﴿٤٦﴾

46. “Na tulikuwa tunaikadhibisha Siku ya Malipo.

حَتَّىٰ أَتَانَا الْيَقِينُ ﴿٤٧﴾

47. “Mpaka yakini (mauti) ikatujia.”

فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ ﴿٤٨﴾

48. Basi hautowafaa uombezi wowote (ule) wa waombezi.

فَمَا لَهُمْ عَنِ التَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ ﴿٤٩﴾

49. Basi wana nini (hata wakawa) ni wenye kupuuza tadhkiratin (ukumbusho)!


كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُّسْتَنفِرَةٌ ﴿٥٠﴾

50. Kama kwamba ni punda wanaotishwa.

فَرَّتْ مِن قَسْوَرَةٍ ﴿٥١﴾
51. Wanaokimbia simba.


بَلْ يُرِيدُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُّنَشَّرَةً ﴿٥٢﴾

52. Bali anataka kila mmoja wao apewe sahifa zilizofunuliwa.

كَلَّا ۖ بَل لَّا يَخَافُونَ الْآخِرَةَ ﴿٥٣﴾

53. Sivyo katu! Bali hawaiogopi Aakhirah.

كَلَّا إِنَّهُ تَذْكِرَةٌ ﴿٥٤﴾

54. Hapana! Bali hiyo ni tadhkirah (ukumbusho).


فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ ﴿٥٥﴾
55. Basi anayetaka atakumbuka.

وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ هُوَ أَهْلُ التَّقْوَىٰ وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ ﴿٥٦﴾

56. Na hawatokumbuka (na kuwaidhika) isipokuwa Akitaka Allaah; Yeye Ndiye Anayepasa kuogopwa, na Mwenye (kutoa) maghfirah.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com