Al-Qadr (97)


سُورَةُ  الْقَدْر
Al-Qadr (97) 

(Imeteremka Makka)


Katika Sura hii upo wito wa kusoma na kujifunza, na kwamba aliye weza kumuumba mtu kutokana na asli nyonge ni Mweza wa kumfunza kuandika kwa kudhibitia ilimu na kutimizia kufahamu, na amfunze aliyo kuwa hayajui. Kwani Yeye Subhanahu ndiye Mwenye kummiminia ilimu mwanaadamu. Na Sura  inanabihisha kwamba utajiri na nguvu huenda zikampelekea mtu kupindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu, lakini marejeo ya wote ni kwa Mwenyezi Mungu mwishoni. Na mazungumzo yanamwelekea kila mwenye kusilihi kusemezwa kuwaonya hao majeuri wanao pinga kheri, kuwaonya kuwa watakuja kushikwa kwa nywele zao za utosi wakibururwa Motoni; na hawatofaliwa na wasaidizi wowote. Na Sura inakhitimisha kwa kuwataka wasikivu wende kinyume na hao wenye inda wanao kadhibisha, na wajijongeze kwa ut'iifu kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ ﴿١﴾

1. Hakika Sisi Tumeiteremsha (Qur-aan) katika Laylatil-Qadr (usiku wa cheo).

وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ ﴿٢﴾

2. Na nini kitakachokujulisha ni nini huo (usiku wa) Laylatul-Qadr?

لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ ﴿٣﴾

3.  (Usiku wa) Laylatul-Qadr ni (usiku) mbora kuliko miezi elfu.

تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ ﴿٤﴾

4. Wanateremka humo Malaika na Ruwh (Jibriyl) kwa idhini ya Rabb (Mola) wao kwa kila amri (jambo).

سَلَامٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ ﴿٥﴾

5. (Usiku huo ni) Amani mpaka kuchomoza Alfajiri.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com