Ar-Rahmaan (55)


سُورَةُ  الرَّحْمن
Ar-Rahmaan (55)

(Imeteremka Madina)


Sura hii imeingia kuzihisabu fadhila na neema za Mwenyezi Mungu, kwa kuanzia baada ya kumtaja Arrah'man, Mwingi wa Rehema, kwa kutaja neema yake tukufu kabisa, nayo ni Kufunza Qur'ani Tukufu. Tena Aya zikaendelea kuzieleza hizo neema kwa namna ya kuweka wazi utukufu wa Mwenye kuziumba, aliye tukuka shani yake; na inadhihirisha uweza wake na ufalme wake juu ya wanaadamu na majini katika mbingu na ardhi.
Na inaeleza adhabu za wakosefu na wanao kadhibisha katika Jahannamu, na ikafafanua neema za wachamngu Peponi.
Na Sura ikakhitimisha kwa kumtakasa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumsifu.
Na Sura imeikariri Aya isemayo "Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?" mara thalathini na moja, katika mpango wa ki- Qur'ani kukariri kunako pendeza kama inavyo wafikiana na haja. Kila moja katika hizo Aya inawagonga hao wakanushaji kwa kuzikadhibisha kwao neema za Mwenyezi Mungu katika Aya iliyo kabla yake.

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

الرَّحْمَـٰنُ ﴿١﴾

1. Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah).

عَلَّمَ الْقُرْآنَ ﴿٢﴾

2. Amefundisha Qur-aan.

خَلَقَ الْإِنسَانَ ﴿٣﴾

3. Ameumba insani.

عَلَّمَهُ الْبَيَانَ ﴿٤﴾

4. Akamfundisha ufasaha.

الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ بِحُسْبَانٍ ﴿٥﴾

5. Jua na mwezi (huenda) katika hesabu.

وَالنَّجْمُ وَالشَّجَرُ يَسْجُدَانِ ﴿٦﴾

6. Na nyota na miti vinasujudu (kwa Allaah).

وَالسَّمَاءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ الْمِيزَانَ ﴿٧﴾

7. Na mbingu Ameziinua na Akaweka mizani.

أَلَّا تَطْغَوْا فِي الْمِيزَانِ ﴿٨﴾

8. Ili msivuke mipaka (kudhulumu) katika mizani.

وَأَقِيمُوا الْوَزْنَ بِالْقِسْطِ وَلَا تُخْسِرُوا الْمِيزَانَ ﴿٩﴾

9. Na simamisheni uzani kwa uadilifu, na wala msipunguze mizani.

وَالْأَرْضَ وَضَعَهَا لِلْأَنَامِ ﴿١٠﴾

10. Na ardhi Ameiweka kwa ajili ya viumbe.

فِيهَا فَاكِهَةٌ وَالنَّخْلُ ذَاتُ الْأَكْمَامِ ﴿١١﴾

11. Humo mna matunda na mitende yenye mafumba.

وَالْحَبُّ ذُو الْعَصْفِ وَالرَّيْحَانُ ﴿١٢﴾

12. Na nafaka zenye makapi na rayhaan (mimea yenye harufu nzuri).

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿١٣﴾

13. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

خَلَقَ الْإِنسَانَ مِن صَلْصَالٍ كَالْفَخَّارِ ﴿١٤﴾

14. Amemuumba insani kutokana na udongo wa mfinyanzi unaotoa sauti kama wa vyungu uliookwa moto.


وَخَلَقَ الْجَانَّ مِن مَّارِجٍ مِّن نَّارٍ ﴿١٥﴾

15. Na Akaumba jini kutokana na mwako wa moto.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿١٦﴾

16. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ ﴿١٧﴾

17. Rabb (Mola) wa Mashariki mbili na Rabb wa Magharibi mbili.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿١٨﴾

18. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ يَلْتَقِيَانِ ﴿١٩﴾

19. Ameziachia bahari mbili zinakutana (bahari ya maji ya chumvi na ya maji matamu).

بَيْنَهُمَا بَرْزَخٌ لَّا يَبْغِيَانِ ﴿٢٠﴾

20. Baina yake (hizo bahari mbili) kuna kizuizi (hivyo) haziingiliani.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢١﴾

21. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

يَخْرُجُ مِنْهُمَا اللُّؤْلُؤُ وَالْمَرْجَانُ ﴿٢٢﴾

22. Zinatoka humo (kwenye hizo bahari mbili) lulu na marijani.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢٣﴾

23. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

وَلَهُ الْجَوَارِ الْمُنشَآتُ فِي الْبَحْرِ كَالْأَعْلَامِ ﴿٢٤﴾

24. Na ni Vyake Pekee vyombo (vinavopita) vikiinuliwa baharini kama milima.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢٥﴾

25. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ ﴿٢٦﴾

26. Kila aliyekuwa juu yake ni mwenye kutoweka.

وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ ﴿٢٧﴾

27. Na utabakia Wajihi wa Rabb (Mola) wako Dhul-Jalaali wal-Ikraam (Mwenye Utukufu na Ukarimu).

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢٨﴾

28. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

يَسْأَلُهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْنٍ ﴿٢٩﴾

29. Wanamuuliza (Yeye) kila aliyekuweko mbinguni na ardhini, kila siku Yeye Yumo katika (kuleta) jambo.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٠﴾
30. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

سَنَفْرُغُ لَكُمْ أَيُّهَ الثَّقَلَانِ ﴿٣١﴾

31. Tutakukusudieni (kukuhesabuni) enyi aina mbili ya viumbe.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٢﴾

32. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ إِنِ اسْتَطَعْتُمْ أَن تَنفُذُوا مِنْ أَقْطَارِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ فَانفُذُوا ۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلْطَانٍ ﴿٣٣﴾

33. Enyi jamii ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye zoni za mbingu na ardhi, basi penyeni. Hamtoweza kupenya isipokuwa kwa madaraka (kutoka kwa Allaah).

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٤﴾

34. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

يُرْسَلُ عَلَيْكُمَا شُوَاظٌ مِّن نَّارٍ وَنُحَاسٌ فَلَا تَنتَصِرَانِ ﴿٣٥﴾

35. Mtapelekewa mwako wa Moto juu yenu na shaba iliyoyayushwa, basi hamtoweza kushinda.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٦﴾

36. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

فَإِذَا انشَقَّتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ وَرْدَةً كَالدِّهَانِ ﴿٣٧﴾

37. Basi zitakapochanika-chanika mbingu zikawa (rangi ya) waridi kama mafuta.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٨﴾

38. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُسْأَلُ عَن ذَنبِهِ إِنسٌ وَلَا جَانٌّ ﴿٣٩﴾

39. Siku hiyo hatoulizwa kuhusu dhambi yake binadamu na wala jini.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٠﴾

40. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

يُعْرَفُ الْمُجْرِمُونَ بِسِيمَاهُمْ فَيُؤْخَذُ بِالنَّوَاصِي وَالْأَقْدَامِ ﴿٤١﴾

41. Watatambulikana wahalifu kwa alama zao, basi watachukuliwa kwa vipaji vya uso na (kwa) miguu

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٢﴾

42. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

هَـٰذِهِ جَهَنَّمُ الَّتِي يُكَذِّبُ بِهَا الْمُجْرِمُونَ ﴿٤٣﴾

43. Hii ni Jahannam ambayo wahalifu wanaikanusha.

يَطُوفُونَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ حَمِيمٍ آنٍ ﴿٤٤﴾

44. Wataizunguka baina yake na baina ya maji yachemkayo yenye kutokota.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٥﴾

45. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ ﴿٤٦﴾

46. Na kwa mwenye kukhofu kisimamo mbele ya Rabb (Mola) wake (kuna) bustani mbili.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٧﴾

47. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

ذَوَاتَا أَفْنَانٍ ﴿٤٨﴾

48. Zilizo na matawi yaliyotanda

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٩﴾

49. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

فِيهِمَا عَيْنَانِ تَجْرِيَانِ ﴿٥٠﴾

50. Humo (kwenye bustani mbili katika Jannah, kuna) chemchemu mbili zinazopita.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥١﴾

51. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

فِيهِمَا مِن كُلِّ فَاكِهَةٍ زَوْجَانِ ﴿٥٢﴾

52. Humo (kwenye bustani mbili katika Jannah kuna) kila matunda ya aina mbili.


فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٣﴾

53. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ فُرُشٍ بَطَائِنُهَا مِنْ إِسْتَبْرَقٍ ۚ وَجَنَى الْجَنَّتَيْنِ دَانٍ ﴿٥٤﴾

54. Waegemee kwenye matandiko bitana yake ni kutokana na hariri nzito nyororo, na matunda ya bustani mbili yako karibu (yananing’inia).

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٥﴾

55. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

فِيهِنَّ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ ﴿٥٦﴾
56. Humo (wako) wanawake wenye macho ya kuinamisha (mazuri, kwa staha) hajawahi kuwagusa (kuwajamii) binadamu kabla yao na wala jini.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٧﴾

57. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

كَأَنَّهُنَّ الْيَاقُوتُ وَالْمَرْجَانُ ﴿٥٨﴾

58. Kama kwamba wao (hao wanawake) ni yakuti na marijani.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٩﴾

59. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

هَلْ جَزَاءُ الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ ﴿٦٠﴾

60. Je, kuna jazaa (yeyote ile) ya wema isipokuwa (ni) wema tu?

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦١﴾

61. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ ﴿٦٢﴾

62. Na zaidi ya hizo (mbili, ziko) bustani mbili (zingine).

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٣﴾

63. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

مُدْهَامَّتَانِ ﴿٦٤﴾

64. Za (rangi ya) kijani iliyokoza.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٥﴾

65. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

فِيهِمَا عَيْنَانِ نَضَّاخَتَانِ ﴿٦٦﴾

66. Humo (kwenye bustani mbili, kuna) chemchemu mbili zenye kububujika kwa nguvu mfululizo.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٧﴾

67. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

فِيهِمَا فَاكِهَةٌ وَنَخْلٌ وَرُمَّانٌ ﴿٦٨﴾

68. Humo (kwenye bustani mbili) kuna matunda na mitende na makomamanga.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٩﴾

69. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

فِيهِنَّ خَيْرَاتٌ حِسَانٌ ﴿٧٠﴾

70. Humo (kuna) wanawake wazuri wema.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧١﴾

71. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

حُورٌ مَّقْصُورَاتٌ فِي الْخِيَامِ ﴿٧٢﴾

72. Huwrun (wanawake weupe wazuri wa Jannah) wanaotawishwa katika mahema.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧٣﴾

73.  Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ ﴿٧٤﴾

74. Hajawahi kuwagusa (kuwajamii) binadamu kabla yao na wala jini.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧٥﴾

75. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ رَفْرَفٍ خُضْرٍ وَعَبْقَرِيٍّ حِسَانٍ ﴿٧٦﴾

76. Waegemee kwenye matakia ya kijani na mazulia nyororo mazuri mno.


فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧٧﴾

77. Basi neema ipi ya Rabb (Mola) wenu (enyi majini na wanaadamu) mnaikanusha?

تَبَارَكَ اسْمُ رَبِّكَ ذِي الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ ﴿٧٨﴾

78. Limebarikika Jina la Rabb (Mola) wako Dhil-Jalaali wal-Ikraam (Mwenye Utukufu na Ukarimu)




Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com