113. Falaq


سُورَةُ  الْفَلَقْ
Al-Falaq (113)

(Imeteremka Makka)

Sura hii inamtaka Nabii s.a.w. amwendee Mola wake Mlezi atake ulinzi kwake kujilinda na shari ya kila mwenye shari, ya viumbe vyake, na shari za usiku linapo ingia giza, yanayo yasibu nafsi katika hali ya upweke, na madhara ambayo mtu hawezi kujikinga nayo, na shari za mafisadi wanao pita kuharibu makhusiano na mawasiliano yalio baina ya watu, na shari za hasidi anaye tamani kuondoa neema alizo wapa Mwenyezi Mungu waja wake.

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾

1. Sema: “Najikinga na Rabb (Mola) wa mapambazuko.

مِن شَرِّ مَا خَلَقَ ﴿٢﴾

2. “Kutokana na shari ya Alivyoviumba.

وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ ﴿٣﴾

3. “Na kutokana na shari ya giza linapoingia.

وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ ﴿٤﴾

4. “Na kutokana na shari ya wanaopuliza mafundoni.

وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ ﴿٥﴾

5. Na kutokana na shari ya hasidi anapohusudu.



Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com