HADITHI YA 33

الحديث الثالث والثلاثون
"البينة على المدعي واليمين على من أنكر "
عن ابن عَبَّاسٍ رضي اللُه عنهما: أن رسولَ الله صلى الله عليه وسلم قال: ((لَو يُعْطَى النَّاسُ بِدَعْوَاهُمْ لادَّعَى رِجَالٌ أموالَ قَوْمٍ ودِماءَهُمْ لَكِنِ البَيِّنَةُ على المُدَّعِى والْيَمينُ على من أَنْكَرَ)).

حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ الْبَيْهَقِيّ     وَغَيْرُهُ هَكَذَا، وَبَعْضُهُ فِي "الصَّحِيحَيْنِ". 
 
 HADITHI  YA  33
JUKUMU LA USHAHIDI LIKO KWA YULE ANAYEDAI
NA KULA KIAPO KUNAMUWAJIBIKIA YULE ANAYEKANA

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas رضي الله عنه  ambaye amesema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم   alisema:
Kama watu wangelipewa kwa mujibu  wa madai yao, watu wangelidai mali na damu za wenzao (uhai) lakini jukumu la ushahidi liko kwa yule anayedai na kula kiapo kunawajibika kwa yule anayekana (kuwa hajatenda).

Imesimuliwa na Al-Bayhaqi na wengineo. Ni Hadithi Hasan.