Al-Hadiyd (57)


سُورَةُ  الْحَدِيد
Al-Hadiyd (57)

(Imeteremka Madina)

Sura hii imeanzia kwa kueleza kwamba wote walioko mbinguni na katika ardhi wamemsabihi na kumtakasa Mwenyezi Mungu Mtukufu  na kila kisicho kuwa laiki naye. Kisha ikafuatiliza hayo kwa kuelekeana na kusabihi huko ufalme wa mbingu na ardhi, na kuvizunguka vyote hivyo na kuviendesha. Kisha Sura ikaamrisha Imani ya Mwenyezi Mungu, na kutoa katika njia yake, na ikabainisha khitilafu za daraja za kutoa kwa mujibu wa kukhtalifiana haja ziliopo na dharura zake. Kisha ikaeleza sura ya Waumini Siku ya Kiyama, inavyo tangulia nuru yao mbele yao na pembezoni mwao; na sura ya wanafiki wanavyo waomba Waumini wawangojee ili nao wapate mwangaza kutokana na nuru yao. Na baina yao umesimamishwa ukuta wenye mlango. Ndani yake ipo rehema, na nje yake upande wa mbele yake ni adhabu.
Na Sura ikaingia baada ya hayo kuwahimiza Waumini wanyenyekee kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na Haki aliyo iteremsha. Na inawaonyesha vyeo vya wanao sadiki wanaume na wanawake mbele ya Mola wao Mlezi; na mwisho wa Makafiri wanao kadhibisha ni katika Jahannamu. Na inapiga mifano ya udhalili wa dunia na hizo starehe zake, na ukubwa wa Akhera na neema na adhabu zilioko huko. Na Sura inataka watu wawanie kushindania maghfira kwa Mwenyezi Mungu, na inazituza nafsi kwamba kila kinacho msibu mtu ikiwa kheri au shari kimeandikwa katika Kitabu kilichoko kwa Mwenyezi Mungu, ili nyoyo zinyenyekee kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu. Kisha ikasimulia khabari za kuwatuma Mitume na kuwafuatiliza mmoja baada ya mmoja wakipewa nguvu kwa hoja na Vitabu, na njia za nguvu na vitendo, ili watu wasimamishe uadilifu. Kisha Aya ikakhitimisha kwa kuwaita Waumini wamche Mungu, na ikawaahidi kuwa watapewa rehema maradufu na watafanyiwa hisani ya kufadhiliwa, ambayo hapana mwenye kuiweza hata kidogo ila Mwenyezi Mungu. Kwani hakika fadhila zote zimo katika mkono wa Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kuu.

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١﴾

1. Kinamsabbih Allaah Pekee (kila) kilichokuweko katika mbingu na ardhi Naye Ndiye Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).

لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢﴾

2. Ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, Anahuisha na Anafisha, Naye juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).

هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٣﴾

3. Yeye Ndiye Al-Awwal (wa Awali hakuna kitu kabla Yake) na Al-Aakhir (wa Mwisho hakuna kitu baada Yake) na Adhw-Dhwaahir (Aliye juu hakuna kitu juu Yake), na Al-Baatwin (Aliye karibu, hakuna kitu kilichokaribu kuliko Yeye), Naye kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi).

هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۖ وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٤﴾

4. “Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arsh (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah), Anajua yale (yote) yanayoingia ardhini, na yale (yote) yatokayo humo, na yale (yote) yanayoteremka kutoka mbinguni, na yale (yote) yanayopanda humo, Naye Yu Pamoja nanyi (kwa ujuzi Wake) popote mlipo. Na Allaah kwa yote myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuyaona).”

لَّهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٥﴾

5. Ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, kwa Allaah Pekee yanarejeshwa mambo (yote).

يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ ۚ وَهُوَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٦﴾

6. Anauingiza usiku katika mchana, na Anaingiza mchana katika usiku, Naye ni ‘Aliym (Mjuzi) wa yaliyomo vifuani.

آمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَأَنفِقُوا مِمَّا جَعَلَكُم مُّسْتَخْلَفِينَ فِيهِ ۖ فَالَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَأَنفَقُوا لَهُمْ أَجْرٌ كَبِيرٌ ﴿٧﴾

7. Muaminini Allaah na Rasuli Wake, na toeni kutokana na yale Aliyokufanyieni kuwa warithi kwayo. Basi wale walioamini miongoni mwenu, na wakatao, watapata ujira mkubwa.

وَمَا لَكُمْ لَا تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۙ وَالرَّسُولُ يَدْعُوكُمْ لِتُؤْمِنُوا بِرَبِّكُمْ وَقَدْ أَخَذَ مِيثَاقَكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٨﴾

8. Na mna nini nyinyi (hata mkafikia kuwa) hamumuamini Allaah, na hali Rasuli (Wake) anakuiteni ili mumuamini Rabb (Mola) wenu, na hali Amekwishachukua fungamano lenu mkiwa ni Waumini.

هُوَ الَّذِي يُنَزِّلُ عَلَىٰ عَبْدِهِ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ لِّيُخْرِجَكُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ بِكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿٩﴾

9. Yeye Ndiye Yule Anayemteremshia mja Wake Aayaat bayana ili Akutoeni katika viza na kukuingizeni kwenye Nuru. Na hakika Allaah kwenu ni Rauwfur-Rahiym (Mwenye huruma mno - Mwenye kurehemu).

وَمَا لَكُمْ أَلَّا تُنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلِلَّـهِ مِيرَاثُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا يَسْتَوِي مِنكُم مَّنْ أَنفَقَ مِن قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِّنَ الَّذِينَ أَنفَقُوا مِن بَعْدُ وَقَاتَلُوا ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿١٠﴾

10. Na mna nini nyinyi (hata mkawa) hamtoi katika njia ya Allaah, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Allaah Pekee. Hawi sawa miongoni mwenu aliyetoa kabla ya Ushindi (wa Makkah) na akapigana. Hao watapata daraja kubwa kabisa kuliko wale waliotoa baada (ya ushindi) na wakapigana.  Na wote Allaah Amewaahidi Al-Husnaa (Jannah).  Na Allaah kwa yote myatendayo ni Khabiyr (Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana).

مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ وَلَهُ أَجْرٌ كَرِيمٌ ﴿١١﴾

11. Nani ambaye atamkopesha Allaah karadha nzuri kisha (Allaah) Amuongezee maradufu na apate ujira mtukufu.


يَوْمَ تَرَى الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ يَسْعَىٰ نُورُهُم بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِم بُشْرَاكُمُ الْيَوْمَ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٢﴾

12. Siku utakayowaona Waumini wa kiume na Waumini wa kike, nuru zao zinakimbilia mbele yao na kuliani kwao; (wataambiwa): “Bishara njema kwenu leo! Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Huko ndiko kufuzu kukubwa.”

يَوْمَ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالْمُنَافِقَاتُ لِلَّذِينَ آمَنُوا انظُرُونَا نَقْتَبِسْ مِن نُّورِكُمْ قِيلَ ارْجِعُوا وَرَاءَكُمْ فَالْتَمِسُوا نُورًا فَضُرِبَ بَيْنَهُم بِسُورٍ لَّهُ بَابٌ بَاطِنُهُ فِيهِ الرَّحْمَةُ وَظَاهِرُهُ مِن قِبَلِهِ الْعَذَابُ ﴿١٣﴾

13. Siku wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike watakapowaambia wale walioamini: “Tungojeeni, tupate (mwangaza) kutokana na nuru yenu!” (Itasemwa): “Rudini nyuma yenu, na mshike huko nuru (yenu)!” Kisha utawekwa ukutwa baina yao wenye mlango, ndani mna Rahmah na nje kwa upande wake wa mbele mna adhabu.

يُنَادُونَهُمْ أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ وَلَـٰكِنَّكُمْ فَتَنتُمْ أَنفُسَكُمْ وَتَرَبَّصْتُمْ وَارْتَبْتُمْ وَغَرَّتْكُمُ الْأَمَانِيُّ حَتَّىٰ جَاءَ أَمْرُ اللَّـهِ وَغَرَّكُم بِاللَّـهِ الْغَرُورُ ﴿١٤﴾

14. (Wanafiki) Watawaita (Waumini): “Je, kwani hatukuwa pamoja nanyi?” Watasema: “Ndio! Lakini nyinyi mmezifitini nafsi zenu, na mkangojea kutazama (yatusibu ya kutusibu mpate kufurahia); na mkatia shaka, na ikakulaghaini matumaini ya uongo mpaka ikaja amri ya Allaah; na akakughuruni mdanganyifu (Ibliys) kuhusu Allaah.

فَالْيَوْمَ لَا يُؤْخَذُ مِنكُمْ فِدْيَةٌ وَلَا مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ مَأْوَاكُمُ النَّارُ ۖ هِيَ مَوْلَاكُمْ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٥﴾

15. Basi leo haitochukuliwa kutoka kwenu fidia na wala kutoka kwa waliokufuru. Makazi yenu ni Moto, huo ndio rafiki yenu, na uovu ulioje mahali pa kurejea mwishoni.

أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿١٦﴾

16. Je, haujafika wakati kwa walioamini kwamba zinyenyekee nyoyo zao kwa dhikri[1] ya Allaah na (kwa) yale yaliyoteremka ya haki, na wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla, ukawarefukia muda, kisha zikawa ngumu nyoyo zao? Na wengi miongoni mwao ni mafasiki.

اعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١٧﴾

17. Eleweni kwamba Allaah Anahuisha ardhi baada ya kufa kwake. Amekwishakubainishieni Aayaat ili mpate kutia akilini.

إِنَّ الْمُصَّدِّقِينَ وَالْمُصَّدِّقَاتِ وَأَقْرَضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا يُضَاعَفُ لَهُمْ وَلَهُمْ أَجْرٌ كَرِيمٌ ﴿١٨﴾

18. Hakika wanaume watoao swadaqah na wanawake watoao swadaqah na (wale) waliomkopesha Allaah karadha mzuri, Atawazidishia maradufu, na watapa ujira mtukufu.


وَالَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصِّدِّيقُونَ ۖ وَالشُّهَدَاءُ عِندَ رَبِّهِمْ لَهُمْ أَجْرُهُمْ وَنُورُهُمْ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿١٩﴾

19. Na wale waliomwamini Allaah na Rasuli Wake, hao ndio Asw-Swiddiquwn na Ash-Shuhadaa mbele ya Rabb (Mola) wao. Watapa ujira wao na nuru yao. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat Zetu hao ni watu wa (Moto wa) Al-Jahiym.

اعْلَمُوا أَنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَزِينَةٌ وَتَفَاخُرٌ بَيْنَكُمْ وَتَكَاثُرٌ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ ۖ كَمَثَلِ غَيْثٍ أَعْجَبَ الْكُفَّارَ نَبَاتُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَكُونُ حُطَامًا ۖ وَفِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَغْفِرَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٌ ۚ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿٢٠﴾

20. Eleweni kwamba uhai wa dunia ni mchezo na pumbao na mapambo, na kufakharishana baina yenu na kukithiri katika mali na auladi; ni kama mfano wa mvua inayowafurahisha wakulima mimea yake, kisha yananyweya, basi utayaona yamepiga manjano, kisha yanakuwa yenye kumeng’enyeka (mabuwa). Na Aakhirah (kuna) adhabu kali, na (pia kuna) maghfirah kutoka kwa Allaah na Radhi. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni sterehe danganyifu.

سَابِقُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا كَعَرْضِ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أُعِدَّتْ لِلَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٢١﴾

21. Kimbilieni katika (kuomba) maghfirah ya Rabb (Mola) wenu na Jannah, upana wake kama upana wa mbingu na ardhi, imeandaliwa kwa wale waliomwamini Allaah na Rasuli Wake. Hiyo ni fadhila ya Allaah, Humpa Amtakaye. Na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu.

مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٢٢﴾

22. Hakuna msiba wowote unaokusibuni katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umo katika Kitabu (Lawhum-Mahfuudhw) kabla Hatujauumba (huo msiba). Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.

لِّكَيْلَا تَأْسَوْا عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا تَفْرَحُوا بِمَا آتَاكُمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ ﴿٢٣﴾

23. Ili msisononeke juu ya yale yaliyokuondokeeni na wala msifurahie kwa yale Aliyokupeni (Allaah); na Allaah Hapendi kila mwenye kujinata, anayejifakharisha.

الَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبُخْلِ ۗ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿٢٤﴾

24. Ambao wanaofanya ubakhili na (kisha) wanaamrisha watu ubakhili. Na atakayekenguka, basi hakika Allaah Ndiye Al-Ghaniyyul-Hamiyd (Mkwasi - Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote daima)


لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ ۖ وَأَنزَلْنَا الْحَدِيدَ فِيهِ بَأْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّـهُ مَن يَنصُرُهُ وَرُسُلَهُ بِالْغَيْبِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٢٥﴾

25. Kwa yakini Tuliwapeleka Rasuli Wetu kwa hoja bayana, na Tukateremsha pamoja nao Kitabu na mizani ili watu wasimamie uadilifu. Na Tukateremsha chuma chenye nguvu shadidi na manufaa kwa watu, na ili Allaah Atambue yule anayemnusuru (kwa kuinusuru Dini Yake) na (yule anayemuunga mkono) Rasuli Wake kwa ghayb. Hakika Allaah ni Qawiyyun-‘Aziyz (Mwenye nguvu zote daima - Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima).

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا وَإِبْرَاهِيمَ وَجَعَلْنَا فِي ذُرِّيَّتِهِمَا النُّبُوَّةَ وَالْكِتَابَ ۖ فَمِنْهُم مُّهْتَدٍ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿٢٦﴾

26. Na kwa yakini Tulimtuma Nuwh, na Ibraahiym, na Tukajaalia katika dhuriya wao (wawili hawa) Unabii na Kitabu. Basi miongoni mwao (wako) waongofu, na wengi wao ni mafasiki.

ثُمَّ قَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِم بِرُسُلِنَا وَقَفَّيْنَا بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ وَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ وَجَعَلْنَا فِي قُلُوبِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ رَأْفَةً وَرَحْمَةً وَرَهْبَانِيَّةً ابْتَدَعُوهَا مَا كَتَبْنَاهَا عَلَيْهِمْ إِلَّا ابْتِغَاءَ رِضْوَانِ اللَّـهِ فَمَا رَعَوْهَا حَقَّ رِعَايَتِهَا ۖ فَآتَيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا مِنْهُمْ أَجْرَهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿٢٧﴾

27. Kisha Tukawafuatisha nyao zao Rasuli Wetu, na Tukamfuatisha ‘Iysaa mwana wa Maryam, na Tukampa Injiyl. Na Tukaweka katika nyoyo za wale waliomfuata upole na Rahmah na uruhubani (utawa, ‘ibaadah hadi kujizuia kutokuoa au kutokuolewa); wameubuni (wao wenyewe) Hatukuwaandikia hayo juu yao isipokuwa ni kutafuta Radhi za Allaah. Lakini hawakuuchunga ipasavyo kuchungwa. Basi Tukawapa wale walioamini miongoni mwao ujira wao, na wengi wao ni mafasiki.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَآمِنُوا بِرَسُولِهِ يُؤْتِكُمْ كِفْلَيْنِ مِن رَّحْمَتِهِ وَيَجْعَل لَّكُمْ نُورًا تَمْشُونَ بِهِ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٨﴾

28. Enyi mlioamini! Mcheni Allaah, na muaminini Rasuli Wake. (Allaah) Atakupeni sehemu mbili kati ya Rahmah Zake, na Atakujaalieni Nuru mnatembea nayo, na Atakughufurieni; na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).

لِّئَلَّا يَعْلَمَ أَهْلُ الْكِتَابِ أَلَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّن فَضْلِ اللَّـهِ ۙ وَأَنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٢٩﴾

29. Ili waelewe Ahlul-Kitaabi kwamba hawana uwezo wa chochote katika fadhila za Allaah, na kwamba fadhila zimo Mkononi mwa Allaah, (na kwamba Allaah) Humpa Amtakaye, na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu.




Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com