Al-Haaqah (69)

سُورَةُ  الْحآقَّة
Al-Haaqah (69)

(Imeteremka Makka)




Sura hii tukufu inaeleza hali za Kiyama, na imetaja yaliyo wasibu watu wa mataifa yaliyo tangulia, ya kuteketezwa, na kuchukuliwa kwa nguvu na shida walipo kadhibisha. Na imetaja namna litavyo pulizwa baragumu, na mageuzi na kuondoka yatakayo zisibu ardhi na milima na mbingu. Na yatakayo tokea baada ya hayo ya kuletwa watu kwa ajili ya hisabu, na kubashiriwa watu wa mkono wa kulia kwa malipo ya ukarimu na neema za daima watakazo zipata, na maonyo ya watu wa kushoto na adhabu chungu. Tena Sura ikakhitimisha kwa kutaja ukweli wa Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. katika Ujumbe alio ufikisha, na ukweli wa Qur'ani ambao ndio ni Haki iliyo yakini.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

الْحَاقَّةُ ﴿١﴾

1. Al-Haaqqah (tukio la haki lisiloepukika; Qiyaamah).

مَا الْحَاقَّةُ ﴿٢﴾

2. Ni nini Al-Haaqqah?

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْحَاقَّةُ ﴿٣﴾

3. Na nini kitakachokujulisha (ni) nini (hiyo) Al-Haaqqah?

كَذَّبَتْ ثَمُودُ وَعَادٌ بِالْقَارِعَةِ ﴿٤﴾

4. Kina Thamuwd na ‘Aad walikadhibisha Al-Qaari’ah (msiba unaogonga gonga ambao ni Qiyaamah).

فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهْلِكُوا بِالطَّاغِيَةِ ﴿٥﴾

5. Ama kina Thamuwd (wao) waliangamizwa kwa atw-twaaghiyah (mshituko wa mfyatuko mkubwa mno).

وَأَمَّا عَادٌ فَأُهْلِكُوا بِرِيحٍ صَرْصَرٍ عَاتِيَةٍ ﴿٦﴾

6. Na ama kina ‘Aad (wao) waliangamizwa kwa kimbunga (tsunanmi) isio na kifani.


سَخَّرَهَا عَلَيْهِمْ سَبْعَ لَيَالٍ وَثَمَانِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومًا فَتَرَى الْقَوْمَ فِيهَا صَرْعَىٰ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ خَاوِيَةٍ ﴿٧﴾

7. Aliwalazimishia masiku saba na michana minane inayofuatana. Basi utaona watu humo wameanguka (wakiwa wamekufa) kama kwamba magogo ya mitende matupu (ya wazi ndani).

فَهَلْ تَرَىٰ لَهُم مِّن بَاقِيَةٍ ﴿٨﴾

8. Basi je, unaona mabakio (yao) yoyote (yale) yaliyobakia?

وَجَاءَ فِرْعَوْنُ وَمَن قَبْلَهُ وَالْمُؤْتَفِكَاتُ بِالْخَاطِئَةِ ﴿٩﴾

9. Na akaja Fir’awn na wale walio kabla yake, na (watu wa) miji iliyopinduliwa (chini juu) na makosa (yao).

فَعَصَوْا رَسُولَ رَبِّهِمْ فَأَخَذَهُمْ أَخْذَةً رَّابِيَةً ﴿١٠﴾

10. Basi wakamuasi Rasuli wa Rabb (Mola) wao; Akawachukua mchukuo wa nguvu.

إِنَّا لَمَّا طَغَى الْمَاءُ حَمَلْنَاكُمْ فِي الْجَارِيَةِ ﴿١١﴾

11. Maji yalipofurika, hakika Sisi Tulikubebeni katika (chombo) kinachokwenda (katika maji).

لِنَجْعَلَهَا لَكُمْ تَذْكِرَةً وَتَعِيَهَا أُذُنٌ وَاعِيَةٌ ﴿١٢﴾

12. Ili tuifanye kuwa ni tadhkiratan (ukumbusho) kwenu, na ibakie katika sikio linalobakisha kumbukumbu.

فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ نَفْخَةٌ وَاحِدَةٌ ﴿١٣﴾

13. Basi itakapopulizwa katika baragumu mpulizo mmoja.

وَحُمِلَتِ الْأَرْضُ وَالْجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةً وَاحِدَةً ﴿١٤﴾

14. Na ikabebwa ardhi na majabali kisha vikavunjwa vunjwa mvunjo mmoja.

فَيَوْمَئِذٍ وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ ﴿١٥﴾

15. Basi siku hiyo ndio litatokea tukio la kutokea (Qiyaamah).

وَانشَقَّتِ السَّمَاءُ فَهِيَ يَوْمَئِذٍ وَاهِيَةٌ ﴿١٦﴾

16. Na mbingu zitapasuka kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu sana.

وَالْمَلَكُ عَلَىٰ أَرْجَائِهَا ۚ وَيَحْمِلُ عَرْشَ رَبِّكَ فَوْقَهُمْ يَوْمَئِذٍ ثَمَانِيَةٌ ﴿١٧﴾

17. Na Malaika watakuwa pembezoni mwake, na (Malaika) wanane watabeba juu yao siku hiyo ‘Arsh ya Rabb (Mola) wako.

يَوْمَئِذٍ تُعْرَضُونَ لَا تَخْفَىٰ مِنكُمْ خَافِيَةٌ ﴿١٨﴾

18. Siku hiyo mtahudhurishwa (kuhukumiwa), hakitafichikia kwenu (chochote) kifichikacho.

فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَيَقُولُ هَاؤُمُ اقْرَءُوا كِتَابِيَهْ ﴿١٩﴾

19. Ama yule atakayepewa kitabu chake kuliani mwake; atasema: “Ha!  Someni kitabu changu!

إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَاقٍ حِسَابِيَهْ ﴿٢٠﴾

20. “Hakika mimi niliyakinisha kuwa ni mwenye kukutana na hesabu yangu!”

فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ﴿٢١﴾

21. Basi yeye atakuwa katika maisha ya kuridhisha.

فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ ﴿٢٢﴾
22. Kwenye Jannah ya juu.

قُطُوفُهَا دَانِيَةٌ ﴿٢٣﴾

23. Kuchumwa kwake (matunda) ni karibu.


كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الْأَيَّامِ الْخَالِيَةِ ﴿٢٤﴾

24. (Wataambiwa): “Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyoyatanguliza katika siku nyingi zilopita.”

وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِشِمَالِهِ فَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُوتَ كِتَابِيَهْ ﴿٢٥﴾

25. Na ama yule atakayepewa kitabu chake kushotoni mwake; atasema: “Laiti nisingelipewa kitabu changu!

وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيَهْ ﴿٢٦﴾

26. “Na wala nisingelielewa hesabu yangu!

يَا لَيْتَهَا كَانَتِ الْقَاضِيَةَ ﴿٢٧﴾

27. “Laiti yangelikuwa (mauti) ndio kumalizika kwangu.

مَا أَغْنَىٰ عَنِّي مَالِيَهْ ۜ ﴿٢٨﴾

28. “Haikunifaa mali yangu.

هَلَكَ عَنِّي سُلْطَانِيَهْ ﴿٢٩﴾

29. “Usultani wangu  (mamlaka, nguvu) umehiliki.”

خُذُوهُ فَغُلُّوهُ ﴿٣٠﴾

30. (Itasemwa): “Mchukueni, na mfungeni pingu.

ثُمَّ الْجَحِيمَ صَلُّوهُ ﴿٣١﴾

31. “Kisha kwenye (Moto wa) Al-Jahiym muingizeni aungue.

ثُمَّ فِي سِلْسِلَةٍ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعًا فَاسْلُكُوهُ ﴿٣٢﴾

32. “Kisha katika minyororo yenye urefu wa dhiraa sabini muingizieni (mfunganisheni).”

إِنَّهُ كَانَ لَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ الْعَظِيمِ ﴿٣٣﴾

33. Hakika yeye alikuwa hamuamini Allaah Mtukufu.

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿٣٤﴾

34. Na wala hahimizi kulisha masikini.

فَلَيْسَ لَهُ الْيَوْمَ هَاهُنَا حَمِيمٌ ﴿٣٥﴾

35. Basi leo hapa hatokuwa na rafiki wa dhati (anayemjali).


وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنْ غِسْلِينٍ ﴿٣٦﴾

36. Na wala (hawatopata) chakula isipokuwa usaha.

لَّا يَأْكُلُهُ إِلَّا الْخَاطِئُونَ ﴿٣٧﴾

37. Hawakili (chakula) hicho isipokuwa wenye makosa.

فَلَا أُقْسِمُ بِمَا تُبْصِرُونَ ﴿٣٨﴾

38. Basi Naapa kwa yale mnayoyaona.

وَمَا لَا تُبْصِرُونَ ﴿٣٩﴾

39. Na yale msiyoyaona.

إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ﴿٤٠﴾

40. Hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni kauli ya Rasuli mtukufu.

وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِرٍ ۚ قَلِيلًا مَّا تُؤْمِنُونَ ﴿٤١﴾

41. Na hiyo si kauli ya mshairi; ni kidogo (sana) yale mnayoyaamini.

وَلَا بِقَوْلِ كَاهِنٍ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na wala si kauli ya kahini; kidogo (sana) yale mnayokumbuka.  

تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٣﴾

43.  Ni uteremsho kutoka kwa Rabb (Mola) wa walimwengu.


وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِيلِ ﴿٤٤﴾

44. Na lau kama (Mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) angetuzulia baadhi za kauli.

لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ ﴿٤٥﴾

45. Bila shaka Tungelimchukua kwa Mkono wa kuume.

ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ ﴿٤٦﴾

46. Kisha bila shaka Tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo (Tukatoa roho).

فَمَا مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَاجِزِينَ ﴿٤٧﴾

47. Basi hakuna mmoja yeyote kati yenu angeliweza kutuzuia naye (kumuadhibu).

وَإِنَّهُ لَتَذْكِرَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٤٨﴾

48. Na hakika hii bila shaka ni tadhkiratun (ukumbusho) kwa wenye taqwa.

وَإِنَّا لَنَعْلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ ﴿٤٩﴾

49. Na hakika Sisi bila shaka Tunajua kwamba miongoni mwenu (wako) wenye kukadhibisha.


وَإِنَّهُ لَحَسْرَةٌ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٥٠﴾

50. Na hakika hii (Qur-aan) bila shaka itakuwa ni majuto makubwa juu ya makafiri (Siku ya Qiyamaah).

وَإِنَّهُ لَحَقُّ الْيَقِينِ ﴿٥١﴾

51. Na hakika hii (Qur-aan) ni haki ya yakini.

فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ ﴿٥٢﴾

52. Basi sabbih kwa Jina la Rabb (Mola) Mtukufu.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com