HADITHI YA 17 MOLA KAANDIKA UZURI (WEMA) KATIKA KILA KITU

الحديث السابع عشر
"إن الله كتب الإحسان على كل شيء"

 عن أبي يَعْلَى شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رضي اللهُ عنه، عن رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال: ((إنَّ اللهَ كَتَبَ الإِحْسانَ على كلِّ شَيءٍ، فإذا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ، وَإذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذِّبْحَةَ، ولْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ ولْيُرِحْ ذَبيحَتَهُ))

رَوَاهُ مُسْلِمٌ   
HADITHI YA 17
MOLA KAANDIKA UZURI (WEMA) KATIKA KILA KITU
Kutoka kwa Abu Ya’ala  Shaddad Ibn Aws رضي الله عنه  ambaye amesema: Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Mola kaamrisha wema katika kila kitu.  Kwa hiyo unapoua (mnyama), ua vizuri  na unapochinja chinja vizuri.  Basi kila mmoja wenu anoe kisu chake barabara (anapotaka kuchinja) na amuondoshee machungu (asimtese) yule mnyama anayemchinja.
Imesimuliwa na Muslim