Al-Qaari’ah (101)

سُورَةُ الْقَارِعَة
Al-Qaari’ah (101)

(Imeteremka Makka)

 

Sura hii inaanza  kwa kitisho cha hiyo AL-QAARIA'H, yaani Inayo gonga, sauti inayo gonga katika masikio ya watu, yaani ndio Kiyama. Na Sura imetaja baadhi ya hali za hiyo sauti inayo gonga khasa kwa mintarafu ya watu na milima. Na ikashughulikia kusimulia hao ambao mizani yao itakuwa nzito kwa kuzidi mema yao, na mizani yao itayo kuwa duni kwa kuzidi maovu yao (na kupunguka mema yao).


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الْقَارِعَةُ ﴿١﴾

1. Al-Qaari’ah (msiba unaogonga gonga).


مَا الْقَارِعَةُ ﴿٢﴾

2. Ni nini hiyo Al-Qaari’ah?

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْقَارِعَةُ ﴿٣﴾

3. Na nini kitakachokujulisha nini hiyo Al-Qaari’ah?

يَوْمَ يَكُونُ النَّاسُ كَالْفَرَاشِ الْمَبْثُوثِ ﴿٤﴾

4. Siku watakapokuwa watu kama vipepeo waliotawanyika.

وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ الْمَنفُوشِ ﴿٥﴾

5. Na majabali yatakuwa kama pamba (sufi) iliyochambuliwa.

فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ ﴿٦﴾

6. Basi yule itakayekuwa mizani yake nzito.


فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ﴿٧﴾

7. Basi huyo atakuwa katika maisha ya kuridhisha.

وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ ﴿٨﴾

8. Na yule itakayekuwa mizani yake khafifu.

فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ ﴿٩﴾

9. Basi makazi yake ni Haawiyah.

وَمَا أَدْرَاكَ مَا هِيَهْ ﴿١٠﴾

10. Na nini kitakachokujulisha ni nini hiyo Haawiyah?

نَارٌ حَامِيَةٌ ﴿١١﴾

11. Ni Moto mkali mno!