الْمَائِدَة
Al-Maaidah: 5
(Imeteremka Madina)
Hii
Sura ya Madina. Idadi za Aya zake ni 120. Na hii ni katika Sura zilizo shuka
karibu na mwisho. Humu umebainishwa waajibu wa kutimiza maagano, sawa yakiwa
baina ya mja na Mola wake Mlezi, au baina ya watu wenyewe kwa wenyewe. Na Sura
hii imebainisha baadhi ya vyakula vilivyo harimishwa, kama ilivyo bainisha
vilivyo halali, na kuhalalisha kuwaoa wanawake wa Ahlil Kitabi, Wakristo na
Mayahudi. Zimetajwa pia humu nguzo za udhu na kutayamamu. Kadhaalika imeelezwa
kutakikana kufanya uadilifu na adui. Na Sura hii imeashiria neema za Mwenyezi
Mungu juu ya Waislamu, na waajibu wao kukihifadhi Kitabu chao, na ikaelezea
kuwa Mayahudi wameyatengua maneno kutokana na pahala pake, na Wakristo
wakayasahau baadhi ya mambo waliyo kumbushwa, na kwamba wao wamekufuru kwa kusema
kwao kuwa Masihi ni mwana wa Mungu. Kadhaalika Sura hii inawakanusha Mayahudi
na Wakristo kwa yale madai yao kwamba ati wao ni wana wa Mungu na vipenzi
vyake. Kisha tena Sura hii imekusanya baadhi ya khabari za Mayahudi, kama
ilivyo kusanya kisa cha wana wawili wa Adam. Kisa hichi kinathibitisha
kuwa uvamizi na kudhulumiana ni katika tabia za kibinaadamu. Tena kuwajibika
kumtoza kisasi mwenye kudhulumu ni njia ya kuidhibiti tabia hii mbovu isivuke
mpaka! Na Sura Al Maidah imeeleza adhabu ya kumtia adabu mwenye kufanya fiski
na wizi. Tena baadae ikarejea kubainisha vipi Mayahudi walivyo pindua hukumu za
sharia zilizo kuwamo katika Taurati, na ikabainisha kwamba katika Taurati na
Injili ulikuwapo ukweli na haki kabla ya kuchezewa na kugeuzwa geuzwa. Na ikahakikishwa
kuwa ni waajibu kuhukumu kwa mujibu alivyo teremsha Mwenyezi Mungu. Sura
imeashiria juu ya uadui wa Mayahudi na Wakristo kwa Waumini, na waajibu wa
kutowanyenyekea, na kutowaridhia kwa wanayo tenda, na kuwa ni dharura
kuwapinga. Na Sura imethibitisha kuwa Wakristo wamekufuru kwa kusema kwao
Mwenyezi Mungu ni mmoja wa Watatu! Tena Qur'an katika Sura hii imewasifu baadhi
ya Wakristo ambao wameikubali haki na wakaiamini, na ikamkataza Muumini
kujiharimishia mwenyewe vitu vizuri, na ikabainisha nini kafara ya kuvunja
kiapo. Sura hii kadhaalika imeharimisha ulevi kabisa, na imebainisha ibada za
Hija na cheo cha Alkaaba na miezi mitakatifu, na ikaeleza upotovu wa baadhi ya
mambo waliyo jiharimishia Waarabu wenyewe kwa wenyewe bila ya hoja wala dalili
yoyote, kama ilivyo bainisha wasia wakati wa safari. Mwishoe Sura hii
imekhitimisha kwa kutaja miujiza iliyo tokea kwa Nabii Isa a.s. Na juu ya hiyo
miujiza Banu Israili walimkanya. Pia Sura imetaja kuwa Nabii Isa a.s. hana
dhambi ya walio potoka wakamuabudu, na imeeleza Ufalme wa Mwenyezi Mungu
Subhanahu juu ya mbingu na ardhi, na ukamilifu wa uwezo wake.
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَوْفُوا بِالْعُقُودِ ۚ أُحِلَّتْ لَكُم بَهِيمَةُ الْأَنْعَامِ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ غَيْرَ مُحِلِّي الصَّيْدِ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۗ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ مَا يُرِيدُ ﴿١﴾
1. Enyi mlioamini! Timizeni mikataba. Imehalalishwa kwenu wanyama wa
mifugo wanaopelekwa malishoni, isipokuwa mnaosomewa (humu) - kuwinda
imeharamishwa (pia) mkiwa katika Ihraam. Hakika Allaah Anahukumu Atakayo.
يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحِلُّوا شَعَائِرَ اللَّـهِ وَلَا
الشَّهْرَ الْحَرَامَ وَلَا الْهَدْيَ وَلَا الْقَلَائِدَ وَلَا آمِّينَ
الْبَيْتَ الْحَرَامَ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّن رَّبِّهِمْ وَرِضْوَانًا ۚ وَإِذَا حَلَلْتُمْ فَاصْطَادُوا ۚ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ أَن صَدُّوكُمْ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ أَن تَعْتَدُوا ۘ وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٢﴾
2. Enyi mlioamini! Msihalifu kaida za Dini (na maharamisho) ya
Allaah, wala (taadhima) ya miezi mitukufu wala (kupuuza alama za)
wanyama wanaopelekwa kuchinjwa (Makkah), wala vigwe (vyao), wala
(kuhalifu amani kwa) wanaoiendea Al-Baytal-Haraam wanatafuta (huko) fadhila kutoka kwa Rabb (Mola) wao na Radhi (Zake). Na mkishatoka kwenye Ihraam windeni (mkitaka). Na wala isikuchocheeni chuki ya watu kwa vile walikuzuieni (kufika) Al-Masjidil-Haraam
(kusikupelekeeni) kutaadi. Shirikianeni katika wema na taqwa, na wala
msishirikiane katika dhambi na uadui. Na Mcheni Allaah; hakika Allaah ni
Mkali wa kuakibu.
حُرِّمَتْ
عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ
لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ
وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا
ذَكَّيْتُمْ وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ وَأَن تَسْتَقْسِمُوا
بِالْأَزْلَامِ ۚ ذَٰلِكُمْ فِسْقٌ ۗ الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ ۚ الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لِّإِثْمٍ ۙ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٣﴾
3. Mmeharamishiwa nyamafu (mzoga), na damu, na nyama ya nguruwe, na
kilichotajiwa katika kuchinjwa kwake asiyekuwa Allaah. Na (mnyama
aliyeuawa) kwa kunyongwa, na (aliyekufa kwa) kupigwa, na (aliyekufa kwa)
kuporomoka, na (aliyekufa kwa) kupigwa pembe (na mnyama mwengine), na
aliyeliwa na mnyama mwitu (akafa) isipokuwa mliyewahi kumchinja
(kihalali kabla ya kufa kwake); na (pia mmeharamishiwa) waliochinjwa kwa
ajili ya mizimu, na (pia mmeharamishiwa) kupiga ramli kutokana na
mishale. Hayo kwenu ni ufasiki. Leo wamekata tamaa (kabisa) wale
waliokufuru katika Dini yenu; basi msiwaogope, na Niogopeni (Mimi). Leo
Nimekukamilishieni Dini (yenu), na Nimekutimizieni neema Yangu, na
Nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe (ndio) Dini yenu. Basi atakayefikwa na
dharura na kushurutishwa kutokana na njaa kali (ikampelekea kula
vilivyoharamishwa), pasipo kuelekea dhambi; basi hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).
يَسْأَلُونَكَ مَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۙ وَمَا عَلَّمْتُم مِّنَ الْجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ اللَّـهُ ۖ فَكُلُوا مِمَّا أَمْسَكْنَ عَلَيْكُمْ وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ﴿٤﴾
4. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)
wamehalalishiwa nini? Sema: “Mmehalalishiwa vizuri na mlichowafunza
wanyama (kukiwinda) na ndege wa kuwinda; mnawafunza yale Aliyokufunzeni
Allaah. Basi kuleni walichokukamatieni, na mkitajie Jina la Allaah. Na
mcheni Allaah; hakika Allaah ni Mwepesi wa kuhesabu.
الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ ۖ
وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ
أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ
مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴿٥﴾
5. Leo mmehalalishiwa vizuri. Na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni
halaal kwenu, na chakula chenu ni halaal kwao. Na (mmehalalishwa
kuwaoa) wanawake walioimarisha sitara (wasiozini) miongoni mwa Waumini
wanawake na (pia mmehalalishiwa kuwaoa) wanawake walioimarisha sitara
(wasiozini) miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu; mtakapowapa
mahari yao mkafunga nao ndoa bila ya kufanya uhasharati wala kuchukua
hawara. Na yeyote atakayekufuru iymaan; basi kwa yakini zimebatilika
‘amali zake; naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.
يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا
وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ
وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ
وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم
مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً
فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم
مِّنْهُ ۚ
مَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُم مِّنْ حَرَجٍ وَلَـٰكِن
يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ
تَشْكُرُونَ﴿٦﴾
6. Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Swalaah; osheni nyuso
zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi, na panguseni kwa (kupaka
maji) vichwa vyenu na (osheni) miguu yenu hadi vifundoni. Na mkiwa na
janaba basi jitwaharisheni. Na mkiwa wagonjwa (maji yanawadhuru) au mko
safarini au mmoja wenu akitoka msalani, au mmewagusa (kwa matamanio au
mmejamiiana na) wanawake, kisha hamkupata maji; basi mtayammamu (ikusudieni
ardhi), panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu. Allaah Hataki
kukufanyieni magumu, lakini Anataka kukutwaharisheni na Akutimizieni
neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru.
وَاذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَمِيثَاقَهُ الَّذِي وَاثَقَكُم بِهِ إِذْ قُلْتُمْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿٧﴾
7. Na kumbukeni neema ya Allaah juu yenu na fungamano Lake ambalo
Amekufungamanisheni nalo mliposema: “Tumesikia na Tumetii.” Na mcheni
Allaah; hakika Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi) kwa yaliyomo vifuani.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ لِلَّـهِ شُهَدَاءَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَىٰ أَلَّا تَعْدِلُوا ۚ اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿٨﴾
8. Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Allaah
mkitoa ushahidi kwa uadilifu. Na wala chuki ya watu isikuchocheeni
kutokufanya uadilifu. Fanyeni uadilifu; hivyo ni karibu zaidi na taqwa.
Na mcheni Allaah; hakika Allaah Khabiyr (Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyofichikana) kwa myatendayo.
وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ۙ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ﴿٩﴾
9. Allaah Amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema; (kwamba) watapata maghfirah na ujira adhimu.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ﴿١٠﴾
10. Na waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (na ishara, dalili n.k) Zetu, hao ni watu wa (Moto wa) Al-Jahiym.
يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ
هَمَّ قَوْمٌ أَن يَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ فَكَفَّ أَيْدِيَهُمْ
عَنكُمْ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ﴿١١﴾
11. Enyi mlioamini! Kumbukeni neema ya Allaah juu yenu, pale
walipopania watu kunyosheeni mikono yao (kukushambulieni), kisha Allaah
Akazuia mikono yao kutoka kwenu (kukufikieni). Na mcheni Allaah; na kwa
Allaah pekee watawakali Waumini.
وَلَقَدْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَبَعَثْنَا مِنْهُمُ اثْنَيْ عَشَرَ نَقِيبًا ۖ وَقَالَ اللَّـهُ إِنِّي مَعَكُمْ ۖ
لَئِنْ أَقَمْتُمُ الصَّلَاةَ وَآتَيْتُمُ الزَّكَاةَ وَآمَنتُم بِرُسُلِي
وَعَزَّرْتُمُوهُمْ وَأَقْرَضْتُمُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا
لَّأُكَفِّرَنَّ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَلَأُدْخِلَنَّكُمْ جَنَّاتٍ
تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۚ فَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ﴿١٢﴾
12. Na kwa yakini Allaah Alichukua fungamano la wana wa Israaiyl na
Tukawapelekea miongoni mwao wakuu kumi na mbili. Na Allaah Akasema:
“Hakika Mimi Niko pamoja nanyi; mtakaposimamisha Swalaah, na kutoa
Zakaah, na kuamini Rasuli Wangu, na kuwaunga mkono, na kumkopesha Allaah
mkopo mzuri; bila shaka Nitakufutieni maovu yenu, na Nitakuingizeni
Jannaat zipitazo chini yake mito. Na yeyote atakayekufuru baada ya hapo
miongoni mwenu; basi kwa yakini amepotea njia iliyo sawa.”
فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ لَعَنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةً ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ ۙ وَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ ۚ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىٰ خَائِنَةٍ مِّنْهُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاصْفَحْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ﴿١٣﴾
13. Kwa (sababu ya) kuvunja kwao fungamano lao, Tuliwalaani na
Tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanageuza maneno (ya Allaah) kutoka
mahali pake, na wakasahu sehemu ya yale waliyokumbushwa kwayo. Na
utaendelea kupata (habari za) khiana kutoka kwao isipokuwa wachache
miongoni mwao. Basi wasamehe na achilia mbali (maudhi yao). Hakika
Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.
وَمِنَ
الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ أَخَذْنَا مِيثَاقَهُمْ فَنَسُوا
حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ فَأَغْرَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ
وَالْبَغْضَاءَ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۚ وَسَوْفَ يُنَبِّئُهُمُ اللَّـهُ بِمَا كَانُوا يَصْنَعُونَ﴿١٤﴾
14. Na kwa wale waliosema: “Hakika sisi ni Naswaaraa” Tulichukua
fungamano lao, wakasahau sehemu ya yale waliyokumbushwa kwayo. Basi
Tukapandikiza baina yao uadui na bughudha mpaka Siku ya Qiyaamah. Na
Allaah Atawajulisha waliyokuwa wakiyatenda.
يَا
أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا
مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ ۚ قَدْ جَاءَكُم مِّنَ اللَّـهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ﴿١٥﴾
15. Enyi Ahlal-Kitaab! Hakika amekwishakujieni Rasuli Wetu
anayekubainishieni mengi katika yale mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu,
na anasamehe mengi. Kwa yakini imekufikieni kutoka kwa Allaah nuru na
Kitabu bayana.
يَهْدِي
بِهِ اللَّـهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَهُ سُبُلَ السَّلَامِ وَيُخْرِجُهُم
مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِهِ وَيَهْدِيهِمْ إِلَىٰ
صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿١٦﴾
16. Allaah Anamwongoza kwacho yeyote atayefuata Radhi Zake katika
njia za salama; na Anawatoa katika viza kuingia katika nuru kwa idhini
Yake, na Anawaongoza kuelekea njia iliyonyooka.
لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۚ
قُلْ فَمَن يَمْلِكُ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا إِنْ أَرَادَ أَن يُهْلِكَ
الْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ۗ وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿١٧﴾
17. Kwa yakini, wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah Ndiye Al-Masiyh mwana wa Maryam.” Sema: “Nani anayemiliki chochote mbele ya Allaah, Akitaka kumhilikisha Al-Masiyh
mwana wa Maryam na mama yake na walioko ardhini wote? Na ufalme ni wa
Allaah Pekee wa mbingu na ardhi na vyote vilivyo baina yake, Anaumba
Atakacho. Na Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).
وَقَالَتِ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَىٰ نَحْنُ أَبْنَاءُ اللَّـهِ وَأَحِبَّاؤُهُ ۚ قُلْ فَلِمَ يُعَذِّبُكُم بِذُنُوبِكُم ۖ بَلْ أَنتُم بَشَرٌ مِّمَّنْ خَلَقَ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۚ وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ﴿١٨﴾
18. Na Mayahudi na Manaswara wamesema: “Sisi ni wana wa Allaah na
vipenzi Vyake.” Sema: “Kwa nini basi Anakuadhibuni kwa dhambi zenu? Bali
nyinyi ni watu miongoni mwa Alioumba. Anamghufuria Amtakaye na
Anamuadhibu Amtakaye. Na ufalme ni wa Allaah Pekee wa mbingu na ardhi na
vyote vilivyo baina yake na Kwake Pekee ndio mahali pa kuishia.
يَا
أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ عَلَىٰ
فَتْرَةٍ مِّنَ الرُّسُلِ أَن تَقُولُوا مَا جَاءَنَا مِن بَشِيرٍ وَلَا
نَذِيرٍ ۖ فَقَدْ جَاءَكُم بَشِيرٌ وَنَذِيرٌ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿١٩﴾
19. Enyi Ahlal-Kitaab! Kwa yakini amekwishakujieni Rasuli
Wetu anaekubainishieni (Dini) katika kipindi cha kusita (kisichokuwa) na
Rasuli. Msije kusema: “Hakutujia mbashiriaji yeyote wala mwonyaji”. Kwa
yakini amekujieni mbashiriaji na mwonyaji. Na Allaah juu ya kila kitu
ni Qadiyr (Muweza).
وَإِذْ
قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ
عَلَيْكُمْ إِذْ جَعَلَ فِيكُمْ أَنبِيَاءَ وَجَعَلَكُم مُّلُوكًا
وَآتَاكُم مَّا لَمْ يُؤْتِ أَحَدًا مِّنَ الْعَالَمِينَ﴿٢٠﴾
20. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)
pale Muwsaa alipoambia kaumu yake: “Enyi kaumu yangu! Kumbukeni neema
ya Allaah juu yenu Alipojaalia miongoni mwenu Nabiy, na Akakufanyeni
wenye kumiliki (mambo yenu mkawa huru) na Akakupeni yale Asiyowahi kumpa
yeyote miongoni mwa walimwengu.”
يَا
قَوْمِ ادْخُلُوا الْأَرْضَ الْمُقَدَّسَةَ الَّتِي كَتَبَ اللَّـهُ
لَكُمْ وَلَا تَرْتَدُّوا عَلَىٰ أَدْبَارِكُمْ فَتَنقَلِبُوا خَاسِرِينَ﴿٢١﴾
21. “Enyi kaumu yangu! Ingieni ardhi iliyotakaswa ambayo
Amekuandikieni Allaah kwenu, na wala msirudi nyuma kugeuka (kukimbia
kupigana katika njia ya Allaah, hivyo) mtageuka kuwa wenye
kukhasirika.”
قَالُوا
يَا مُوسَىٰ إِنَّ فِيهَا قَوْمًا جَبَّارِينَ وَإِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا
حَتَّىٰ يَخْرُجُوا مِنْهَا فَإِن يَخْرُجُوا مِنْهَا فَإِنَّا دَاخِلُونَ﴿٢٢﴾
22. Wakasema: “Ee Muwsaa! Hakika humo kuna watu majabari; nasi
hatutaingia humo mpaka (majabari) watoke humo; watakapotoka humo; hapo
(ndio) sisi tutaingia.”
قَالَ
رَجُلَانِ مِنَ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِمَا
ادْخُلُوا عَلَيْهِمُ الْبَابَ فَإِذَا دَخَلْتُمُوهُ فَإِنَّكُمْ
غَالِبُونَ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿٢٣﴾
23. Wakasema watu wawili miongoni mwa wale waliokhofu (kuasi, ambao)
Allaah Aliowaneemesha (walisema): “Waingilieni katika mlango;
mkiwaingilia, basi hakika nyinyi mtashinda. Na kwa Allaah Pekee
tawakalini ikiwa nyinyi ni Waumini”.
قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا أَبَدًا مَّا دَامُوا فِيهَا ۖ فَاذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَاتِلَا إِنَّا هَاهُنَا قَاعِدُونَ﴿٢٤﴾
24. Wakasema: “Ee Muwsaa! Hakika sisi hatutoingia humo abadani madamu wamo (hao majabari); basi nenda wewe na Rabb (Mola) wako mkapigane, hakika sisi tutabakia hapa hapa.”
قَالَ رَبِّ إِنِّي لَا أَمْلِكُ إِلَّا نَفْسِي وَأَخِي ۖ فَافْرُقْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ﴿٢٥﴾
25. (Muwsaa) Akasema: “Rabb (Mola) wangu! Hakika mimi similiki ila nafsi yangu na ndugu yangu; basi Tutenganishe baina yetu na watu mafasiki.”
قَالَ فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيْهِمْ ۛ أَرْبَعِينَ سَنَةً ۛ يَتِيهُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ فَلَا تَأْسَ عَلَى الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ﴿٢٦﴾
26. (Allaah) Akasema: “Basi hakika ardhi hiyo imeharamishwa kwao
miaka arubaini; watatangatanga ardhini. Basi usisikitike juu ya watu
mafasiki.”
وَاتْلُ
عَلَيْهِمْ نَبَأَ ابْنَيْ آدَمَ بِالْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا
فَتُقُبِّلَ مِنْ أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ الْآخَرِ قَالَ
لَأَقْتُلَنَّكَ ۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّـهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ﴿٢٧﴾
27. Na wasomee (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) habari za wana wawili wa Aadam; kwa haki walipotoa qurbaan
(swadaqah) ikakubaliwa ya mmoja wao, na haikukubaliwa ya mwengine;
(asiyekubaliwa) akasema: “Nitakuua.” (Aliyekubaliwa) Akasema: “Hakika
Allaah Anatakabalia wenye taqwa”.
لَئِن بَسَطتَ إِلَيَّ يَدَكَ لِتَقْتُلَنِي مَا أَنَا بِبَاسِطٍ يَدِيَ إِلَيْكَ لِأَقْتُلَكَ ۖ إِنِّي أَخَافُ اللَّـهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ﴿٢٨﴾
28. “Ukininyoshea mkono wako ili uniue, mimi sitokunyoshea mkono wangu kukuua; hakika mimi namkhofu Allaah Rabb (Mola) wa walimwengu.”
إِنِّي أُرِيدُ أَن تَبُوءَ بِإِثْمِي وَإِثْمِكَ فَتَكُونَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الظَّالِمِينَ﴿٢٩﴾
29. Hakika mimi nataka ubebe dhambi zangu na dhambi zako hapo utakuwa
miongoni mwa watu wa Motoni; na hiyo ndiyo jazaa ya madhalimu.
فَطَوَّعَتْ لَهُ نَفْسُهُ قَتْلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُ فَأَصْبَحَ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴿٣٠﴾
30. Basi (aliyekataliwa swadaqah,) nafsi yake ikamwezesha kwa wepesi
kumuua ndugu yake; akamuua na akawa miongoni mwa waliokhasirika.
فَبَعَثَ اللَّـهُ غُرَابًا يَبْحَثُ فِي الْأَرْضِ لِيُرِيَهُ كَيْفَ يُوَارِي سَوْءَةَ أَخِيهِ ۚ قَالَ يَا وَيْلَتَىٰ أَعَجَزْتُ أَنْ أَكُونَ مِثْلَ هَـٰذَا الْغُرَابِ فَأُوَارِيَ سَوْءَةَ أَخِي ۖ فَأَصْبَحَ مِنَ النَّادِمِينَ﴿٣١﴾
31. Kisha Allaah Akamleta kunguru akifukua katika ardhi ili
amwonyeshe vipi asitiri maiti ya ndugu yake. (Muuaji) Akasema: “Ole
wangu! Hivi nimeshindwa kuwa kama huyu kunguru nikamsitiri ndugu yangu?”
Akawa miongoni mwa wajutao.
مِنْ
أَجْلِ ذَٰلِكَ كَتَبْنَا عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَن قَتَلَ
نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ
النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ
جَمِيعًا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم بَعْدَ ذَٰلِكَ فِي الْأَرْضِ لَمُسْرِفُونَ﴿٣٢﴾
32. Kwa ajili ya hivyo, Tukawaandikia (shariy’ah) wana wa
Israaiyl kwamba; atakayeiua nafsi bila ya nafsi (kuua), au (bila ya)
kufanya ufisadi katika ardhi; basi ni kama ameua watu wote. Na
atakayeiokoa (kumsaidia kuishi) basi ni kama amewaokoa watu wote. Na
bila shaka walifikiwa na Rasuli Wetu kwa hoja bayana; kisha wengi
miongoni mwao baada ya hayo wamekuwa wapindukao mipaka ya kuasi.
إِنَّمَا
جَزَاءُ الَّذِينَ يُحَارِبُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَسْعَوْنَ فِي
الْأَرْضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوا أَوْ يُصَلَّبُوا أَوْ تُقَطَّعَ
أَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم مِّنْ خِلَافٍ أَوْ يُنفَوْا مِنَ الْأَرْضِ ۚ ذَٰلِكَ لَهُمْ خِزْيٌ فِي الدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٣٣﴾
33. Hakika jazaa ya wale wanaompiga vita Allaah na Rasuli Wake na
wanafanya bidii kufanya ufisadi katika ardhi; ni kwamba wauawe au
wasulubiwe au wakatwe mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho (mkono wa
kulia kwa mguu wa kushoto, na mkono wa kushoto kwa mguu wa kulia) au
kuhamishwa katika nchi. Hiyo ndiyo hizaya yao duniani. Na Aakhirah
watapata adhabu kuu.
إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن قَبْلِ أَن تَقْدِرُوا عَلَيْهِمْ ۖ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٣٤﴾
34. Isipokuwa wale waliotubia kabla ya kuwashinda nguvu basi jueni kwamba hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).
يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ
الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ﴿٣٥﴾
35. Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na tafuteni Kwake al-wasiylah (njia za 'ibaadah kumkurubia); na fanyeni jihaad katika njia Yake mpate kufaulu.
إِنَّ
الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ أَنَّ لَهُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا
وَمِثْلَهُ مَعَهُ لِيَفْتَدُوا بِهِ مِنْ عَذَابِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَا
تُقُبِّلَ مِنْهُمْ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٣٦﴾
36. Hakika wale waliokufuru, kama watakuwa na yale yote yaliyomo
ardhini na mfano wake pamoja nayo, ili watoe fidia kwayo kuepukana na
adhabu ya Siku ya Qiyaamah, hayatokubaliwa kutoka kwao, na watapata
adhabu iumizayo.
يُرِيدُونَ أَن يَخْرُجُوا مِنَ النَّارِ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنْهَا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّقِيمٌ﴿٣٧﴾
37. Watataka kutoka katika Moto (kwa kila njia); lakini wao si wenye kutoka kamwe humo, na watapata adhabu ya kudumu.
وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَيْدِيَهُمَا جَزَاءً بِمَا كَسَبَا نَكَالًا مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٣٨﴾
38. Mwizi mwanamume na mwizi mwanamke wakateni mikono yao (kitanga
cha mkono wa kulia); ni malipo kwa yale waliyoyachuma, ndio adhabu ya
mfano kutoka kwa Allaah. Na Allaah ni ‘Aziyzun-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye hikmah wa yote).
فَمَن تَابَ مِن بَعْدِ ظُلْمِهِ وَأَصْلَحَ فَإِنَّ اللَّـهَ يَتُوبُ عَلَيْهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٣٩﴾
39. Basi atakayetubia baada ya dhulma yake na akatengenea (kwa
kutenda vitendo vizuri); basi Allaah Atapokea tawbah yake. Hakika Allaah
ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).
أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ وَيَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٤٠﴾
40. Je hujui ya kwamba ni Allaah Pekee Anao ufalme wa mbingu na
ardhi? Humwadhibu Amtakae na Humghufiria Amtakae. Na Allaah juu ya kila
kitu ni Qadiyr (Muweza).
يَا
أَيُّهَا الرَّسُولُ لَا يَحْزُنكَ الَّذِينَ يُسَارِعُونَ فِي الْكُفْرِ
مِنَ الَّذِينَ قَالُوا آمَنَّا بِأَفْوَاهِهِمْ وَلَمْ تُؤْمِن
قُلُوبُهُمْ ۛ وَمِنَ الَّذِينَ هَادُوا ۛ سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ سَمَّاعُونَ لِقَوْمٍ آخَرِينَ لَمْ يَأْتُوكَ ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ مِن بَعْدِ مَوَاضِعِهِ ۖ يَقُولُونَ إِنْ أُوتِيتُمْ هَـٰذَا فَخُذُوهُ وَإِن لَّمْ تُؤْتَوْهُ فَاحْذَرُوا ۚ وَمَن يُرِدِ اللَّـهُ فِتْنَتَهُ فَلَن تَمْلِكَ لَهُ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۚ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَمْ يُرِدِ اللَّـهُ أَن يُطَهِّرَ قُلُوبَهُمْ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٤١﴾
41. Ee Rasuli! Wasikuhuzunishe wale wanaokimbilia kukufuru miongoni
mwa wasemao kwa midomo yao: “Tumeamini” na hali nyoyo zao hazikuamini.
Na miongoni mwa Mayahudi wanaosikiliza kwa makini kwa ajili ya uongo,
wanaosikiliza kwa makini kwa ajili ya watu wengine (wakubwazao)
wasiokufikia. Wanageuza maneno kutoka mahali pake; wanasema (kuwaambia
wafuasi wao): “Mkipewa haya (tunayokuambieni kutoka kwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)
basi yachukueni, na msipopewa hayo basi jihadharini!”. Na yule ambaye
Allaah Anataka kumtia mtihanini, hutamiliki juu yake (uwezo wa
kumsaidia) chochote mbele ya Allaah. Hao ndio ambao Allaah Hakutaka
kuzitakasa nyoyo zao. Watapata hizaya duniani na Aakhirah watapata
adhabu kuu.
سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ أَكَّالُونَ لِلسُّحْتِ ۚ فَإِن جَاءُوكَ فَاحْكُم بَيْنَهُمْ أَوْ أَعْرِضْ عَنْهُمْ ۖ وَإِن تُعْرِضْ عَنْهُمْ فَلَن يَضُرُّوكَ شَيْئًا ۖ وَإِنْ حَكَمْتَ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴿٤٢﴾
42. (Hao) Wenye kusikiliza kwa makini uongo, walaji mno wa haraam. Basi wakikujia (ee Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم
wahukumu baina yao au wapuuze. Na ukiwapuuza, hawatoweza kukudhuru
chochote. Na kama ukihukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika
Allaah Anapenda wafanyao uadilifu.
وَكَيْفَ يُحَكِّمُونَكَ وَعِندَهُمُ التَّوْرَاةُ فِيهَا حُكْمُ اللَّـهِ ثُمَّ يَتَوَلَّوْنَ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا أُولَـٰئِكَ بِالْمُؤْمِنِينَ﴿٤٣﴾
43. Na vipi watakufanya wewe kuwa hakimu (wao) na hali wana Tawraat
iliyomo ndani yake hukumu ya Allaah; kisha baada ya hayo wanakengeuka.
Na hao si wenye kuamini.
إِنَّا أَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ ۚ
يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ أَسْلَمُوا لِلَّذِينَ هَادُوا
وَالرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ بِمَا اسْتُحْفِظُوا مِن كِتَابِ
اللَّـهِ وَكَانُوا عَلَيْهِ شُهَدَاءَ ۚ فَلَا تَخْشَوُا النَّاسَ وَاخْشَوْنِ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ﴿٤٤﴾
44. Hakika Tumeteremsha Tawraat humo mna mwongozo na nuru; ambayo
kwayo, Nabiy waliojisalimisha (kwa Allaah) waliwahukumu Mayahudi na Ar-Rabbaniyyuwna (Wanavyuoni wafanyao mno ‘ibaadah na kufanyia kazi elimu zao) na Al-Ahbaar (Wanavyuoni mafuqahaa
wa dini) pia (walihukumu kwa hiyo Tawraat) kwa sababu waliyokabidhiwa
kuhifadhi Kitabu cha Allaah; na wakawa mashahidi juu yake. Basi
msiwaogope watu, bali Niogopeni (Mimi), na wala msibadili Aayaat Zangu kwa thamani ndogo. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.
وَكَتَبْنَا
عَلَيْهِمْ فِيهَا أَنَّ النَّفْسَ بِالنَّفْسِ وَالْعَيْنَ بِالْعَيْنِ
وَالْأَنفَ بِالْأَنفِ وَالْأُذُنَ بِالْأُذُنِ وَالسِّنَّ بِالسِّنِّ
وَالْجُرُوحَ قِصَاصٌ ۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِ فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَّهُ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿٤٥﴾
45. Na Tumewaandikia (shariy’ah) humo kwamba uhai kwa uhai,
na jichokwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, jino kwa jino; na
majaraha (kulipizana) kisasi. Lakini atakayetolea swadaqah (haki yake
akasemehe) kwayo, basi itakuwa ni kafara kwake. Na yeyote asiyehukumu
kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu.
وَقَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِم بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ ۖ
وَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ
يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ﴿٤٦﴾
46. Na Tukatuma, kufuatisha nyao zao (Mitume hao), ‘Iysaa mwana wa
Maryam akisadikisha yale yaliyoko kabla yake katika Tawraat. Na Tukampa
Injiyl iliyomo ndani yake mwongozo na nuru; na isadikishayo yale
yaliyokuwa kabla yake katika Tawraat, na mwongozo na mawaidha kwa wenye
taqwa.
وَلْيَحْكُمْ أَهْلُ الْإِنجِيلِ بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فِيهِ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴿٤٧﴾
47. Na watu (waliopewa) Injiyl wahukumu kwa yale Aliyoyateremsha
Allaah ndani yake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha
Allaah, basi hao ndio mafasiki.
وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ ۖ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ عَمَّا جَاءَكَ مِنَ الْحَقِّ ۚ لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجًا ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَـٰكِن لِّيَبْلُوَكُمْ فِي مَا آتَاكُمْ ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ﴿٤٨﴾
48. Na Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki kinachosadikisha yale (yaliyokuja katika) Vitabu vilivyokuwa kabla yake na muhayminan
(chenye kudhibiti, kushuhudia nakuhukumu) juu yake (hivo Vitabu). Basi
hukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah; na wala usifuate hawaa
zao kwa kuacha haki iliyokujia. Kwa kila (ummah) katika nyinyi
Tumeujaalia shariy’ah namanhaj. Nakama Angetaka Allaah
Angelikufanyeni ummah mmoja; lakini (Allaah Amekufanyeni hivyo) ili
Akujaribuni katika yale Aliyokupeni. Basi shindaneni katika mambo ya
kheri. Kwa Allaah Pekee ndio marejeo yenu nyote; kisha Atakujulisheni
yale mliyokuwa mkikhitilafiana.
وَأَنِ
احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ
وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ إِلَيْكَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ﴿٤٩﴾
49. Na wahukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, na wala
usifuate hawaa zao, na jihadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya
yale Aliyokuteremshia Allaah. Na wakikengeuka, basi jua kuwa hakika
Allaah Anataka kuwasibu (adhabu) kwa baadhi ya madhambi yao. Na
hakikawengi katika watu ni mafasiki.
أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ﴿٥٠﴾
50. Je, wanataka (uwahukumu kwa) hukumu ya kijaahiliyyah? (ujinga kabla ya Uislamu). Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu? (Yanafahamika haya) kwa watu wenye yakini.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿٥١﴾
51. Enyi mlioamini! Msifanye Mayahudi na Manaswara marafiki
wandani na ushirikiano. Wao kwa wao ni marafiki wandani. Na yeyote
atakayewafanya marafiki wao wandani; basi hakika yeye ni miongoni mwao.
Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu.
فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَىٰ أَن تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ ۚ
فَعَسَى اللَّـهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ
فَيُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا أَسَرُّوا فِي أَنفُسِهِمْ نَادِمِينَ﴿٥٢﴾
52. Basi utawaona wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi (ya shaka
naunafiki) wanakimbilia kwao wakisema: “Tunakhofu isitusibu mgeuko. Basi
Huenda Allaah Akaleta ushindi au jambo (lolote jengine) litokalo Kwake;
wakawa wenye kujuta kwa waliyoyaficha katika nafsi zao.
وَيَقُولُ الَّذِينَ آمَنُوا أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ ۙ إِنَّهُمْ لَمَعَكُمْ ۚ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَأَصْبَحُوا خَاسِرِينَ﴿٥٣﴾
53. Na wale walioamini wanasema: “Je, hawa ndio wale ambao waliapa
kwa (jina la) Allaah kwa viapo vyao vya nguvu, kwamba hakika wao
wapopamoja nanyi?” Zimebatilika ‘amali zao, na wamekuwa wenye
kukhasirika.
يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ
يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى
الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ
اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ﴿٥٤﴾
54. Enyi mlioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini
yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao
watampenda; wanyenyekevu kwa Waumini, wenye nguvu juu ya makafiri;
wanafanya jihaad katika njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama ya
(yeyote) anayelaumu. Hiyo ni fadhila ya Allaah Humpa Amtakaye. Na Allaah
niWaasi’un-‘Aliym (Mwenye wasaa - Mjuzi wa yote).
إِنَّمَا
وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ
يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ﴿٥٥﴾
55. Hakika Waliyy (Mlinzi, Msimamizi) wenu ni Allaah na
Rasuli Wake nawale walioamini, ambao wanasimamisha Swalaah na wanatoa
Zakaah nahali ya kuwa wananyenyekea.
وَمَن يَتَوَلَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا فَإِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْغَالِبُونَ﴿٥٦﴾
56. Na atakayemfanya Allaah kuwa ni Waliyy (Mlinzi, Msimamizi) na Rasuli Wake na wale walioamini (atafuzu); kwani hakika kundi la Allaah ndio washindi.
يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الَّذِينَ اتَّخَذُوا
دِينَكُمْ هُزُوًا وَلَعِبًا مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن
قَبْلِكُمْ وَالْكُفَّارَ أَوْلِيَاءَ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿٥٧﴾
57. Enyi mlioamini! Msiwafanye wale walioifanya Dini yenu mzaha na
mchezo - miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu, (pamoja na)
makafiri (kuwa ndio) marafiki wandani na ushirikiano. Na mcheni Allaah,
kamanyinyi ni Waumini (kweli).
وَإِذَا نَادَيْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ اتَّخَذُوهَا هُزُوًا وَلَعِبًا ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ﴿٥٨﴾
58. Na mnapoita (kuadhini) katika Swalaah; huifanyia mzaha na mchezo. Hivyo ni kwa kuwa wao ni watu wasiotia akilini.
قُلْ
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ هَلْ تَنقِمُونَ مِنَّا إِلَّا أَنْ آمَنَّا
بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلُ وَأَنَّ
أَكْثَرَكُمْ فَاسِقُونَ﴿٥٩﴾
59. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaab Je, mnatuchukia tu kwa vile tumemwamini
Allaah na (tunaamini) yale yaliyoteremshwa kwetu na (pia tunaamini) yale
yaliyoteremshwa kabla; na kwamba wengi wenu ni mafasiki?”
قُلْ هَلْ أُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكَ مَثُوبَةً عِندَ اللَّـهِ ۚ مَن لَّعَنَهُ اللَّـهُ وَغَضِبَ عَلَيْهِ وَجَعَلَ مِنْهُمُ الْقِرَدَةَ وَالْخَنَازِيرَ وَعَبَدَ الطَّاغُوتَ ۚ أُولَـٰئِكَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضَلُّ عَن سَوَاءِ السَّبِيلِ﴿٦٠﴾
60. Sema: “Je, nikujulisheni yaliyo maovu zaidi kuliko hayo kwa
malipo (mabaya) mbele ya Allaah?” Yule ambaye Allaah Amemlaani na
Akamghadhibikia na Akawafanya miongoni mwao manyani na nguruwe na
wakaabudu twaaghuwt, hao wana mahali pabaya mno (Aakhirah) na wapotofu zaidi na njia iliyo sawa (duniani)
وَإِذَا جَاءُوكُمْ قَالُوا آمَنَّا وَقَد دَّخَلُوا بِالْكُفْرِ وَهُمْ قَدْ خَرَجُوا بِهِ ۚ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا كَانُوا يَكْتُمُونَ﴿٦١﴾
61. Na wanapokujieni husema: “Tumeamini.” Na hali wameingia na
ukafiri na wakatoka nao. Na Allaah Anajua zaidi yale waliyokuwa
wakiyaficha.
وَتَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يُسَارِعُونَ فِي الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٦٢﴾
62. Na utawaona wengi miongoni mwao wanakimbilia katika dhambi na
uadui na kula kwao haraam. Ubaya ulioje yale waliyokuwa wakiyatenda.
لَوْلَا يَنْهَاهُمُ الرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ عَن قَوْلِهِمُ الْإِثْمَ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَصْنَعُونَ﴿٦٣﴾
63. Mbona hawawakatazi Ar-Rabbaniyyuwna (Wanavyuoni wafanyao mno ‘ibaadah na kufanyia kazi elimu zao) na Al-Ahbaar (Wanavyuoni mafuqahaa wa dini) kuhusu kauli zao za dhambi na ulaji wao wa haraam. Bila shaka ubaya ulioje yale waliyokuwa wakitenda.
وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَانًا وَكُفْرًا ۚ وَأَلْقَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۚ كُلَّمَا أَوْقَدُوا نَارًا لِّلْحَرْبِ أَطْفَأَهَا اللَّـهُ ۚ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا ۚ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ﴿٦٤﴾
64. Na Mayahudi wakasema: “Mkono wa Allaah umefumbwa.” (Siyo, bali)
mikono yao ndio iliyofumbwa; na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema. Bali
Mikono Yake (Allaah) imefumbuliwa Hutoa Atakavyo. Kwa yakini
yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb (Mola) wako,
yatawazidisha wengi miongoni mwao (hao Mayahudi) upindukaji mipaka ya
kuasi na kufuru. Na Tumewatilia baina yao uadui na bughudha mpaka Siku
ya Qiyaamah. Kila wanapouwasha moto wa vita (dhidi yako), Allaah
Huuzima. Na wanafanya bidii kufanya ufisadi katika ardhi. Na Allaah
Hapendi mafisadi.
وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْكِتَابِ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَكَفَّرْنَا عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَأَدْخَلْنَاهُمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ﴿٦٥﴾
65. Na lau kama Ahlal-Kitaab wangeamini na wakawa na taqwa, bila shaka Tungeliwafutia maovu yao, na bila shaka Tungeliwaingiza katika Jannaat za neema (za kila aina).
وَلَوْ
أَنَّهُمْ أَقَامُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِم
مِّن رَّبِّهِمْ لَأَكَلُوا مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِم ۚ مِّنْهُمْ أُمَّةٌ مُّقْتَصِدَةٌ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ سَاءَ مَا يَعْمَلُونَ﴿٦٦﴾
66. Na lau kama wangeliisimamisha Tawraat na Injiyl na yale yaliyoteremshwa kwao kutoka kwa Rabb
(Mola) wao; bila shaka wangelikula (rizki) kutoka juu yao na chini ya
miguu yao. Miongoni mwao ni wastani (wanaofuata Tawraat na Injiyl kwa
kiasi), na wengi wao wanayoyafanya ni mabaya mno
يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ﴿٦٧﴾
67. Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb
(Mola) wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha ujumbe Wake. Na
Allaah Atakuhifadhi dhidi ya watu. Hakika Allaah Haongoi watu makafiri.
قُلْ
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَسْتُمْ عَلَىٰ شَيْءٍ حَتَّىٰ تُقِيمُوا
التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ ۗ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَانًا وَكُفْرًا ۖ فَلَا تَأْسَ عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ﴿٦٨﴾
68. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaab! Hamko juu ya chochote mpaka muisimamishe (shariy’ah ya) Tawraat na Injiyl na yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Rabb (Mola) wenu. Kwa yakini yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako, yatawazidisha wengi miongoni mwao upindukaji mipaka ya kuasi na kufuru. Basi usisikitike juu ya watu makafiri.
إِنَّ
الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالصَّابِئُونَ وَالنَّصَارَىٰ
مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَا
خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٦٩﴾
69. Hakika wale walioamini (Allaah na Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)
na wale (kabla ya Uislamu;) Mayahudi na Masabai (waabudu nyota) na
Manaswara, atakayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho na akatenda mema,
basi awatokuwa na khofu na wala hawatohuzunika
لَقَدْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَأَرْسَلْنَا إِلَيْهِمْ رُسُلًا ۖ كُلَّمَا جَاءَهُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُهُمْ فَرِيقًا كَذَّبُوا وَفَرِيقًا يَقْتُلُونَ﴿٧٠﴾
70. Kwa yakini Tulichukua fungamano la wana wa Israaiyl na
Tukawapelekea Rasuli. Basi kila alipowajia Rasuli kwa yale yasiyoyapenda
nafsi zao; kundi waliwakadhibisha (Rasuli hao) na kundi wakawaua.
وَحَسِبُوا أَلَّا تَكُونَ فِتْنَةٌ فَعَمُوا وَصَمُّوا ثُمَّ تَابَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ثُمَّ عَمُوا وَصَمُّوا كَثِيرٌ مِّنْهُمْ ۚ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ﴿٧١﴾
71. Na walidhani kwamba haitokuwa fitnah (mitihani au adhabu), basi
wakawa vipofu na wakawa viziwi; kisha Allaah Akapokea tawbah yao; kisha
(tena) wengi wao wakawa vipofu na wakawa viziwi. Na Allaah ni Baswiyr (Mwenye kuona) kwa yale wayatendayo.
لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾
72. Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni Al-Masiyh mwana wa Maryam.” Na Al-Masiyh alisema: “Enyi wana wa Israaiyl! Mwabuduni Allaah, Rabb (Mola) wangu na Rabb
wenu. (Kwani) Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah
Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni Motoni. Na madhalimu
hawatopata mwenye kunusuru yeyote.”
لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٧٣﴾
73. Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu. ”Na hali hapana ilaah (muabudiwa wa haki) isipokuwa Ilaah Mmoja (Pekee). Na wasipoacha yale wanayoyasema, bila ya shaka itawagusa wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo.
أَفَلَا يَتُوبُونَ إِلَى اللَّـهِ وَيَسْتَغْفِرُونَهُ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٧٤﴾
74. Je hawatubii kwa Allaah na wakamwomba maghfira? Na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).
مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ ۖ كَانَا يَأْكُلَانِ الطَّعَامَ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ الْآيَاتِ ثُمَّ انظُرْ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٧٥﴾
75. Al-Masiyh mwana wa Maryam si chochote ila ni Rasuli (tu); bila shaka Wamekwishapita kabla yake Rasuli (wengine). Na mama yake ni swiddiyqah (mkweli). Wote wawili walikuwa wanakula chakula (na hali Allaah Hali). Tazama jinsi Tunavyowabainishia Aayaat (ishara, dalili n.k) kisha tazama vipi wanavyoghilibiwa (kuacha haki).
قُلْ أَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا ۚ وَاللَّـهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٧٦﴾
76. Sema: “Vipi mnaabudu asiyekuwa Allaah asiyemiliki (uwezo wa) kukudhuruni wala kukunufaisheni! Na Allaah Ndiye As-Samiy’ul-‘Aliym” (Mwenye kusikia yote - Mjuzi wa yote).
قُلْ
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ غَيْرَ الْحَقِّ وَلَا
تَتَّبِعُوا أَهْوَاءَ قَوْمٍ قَدْ ضَلُّوا مِن قَبْلُ وَأَضَلُّوا
كَثِيرًا وَضَلُّوا عَن سَوَاءِ السَّبِيلِ﴿٧٧﴾
77. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaab! Msipindukie mipaka katika
dini yenu bila ya haki; na wala msifuate hawaa za watu waliokwishapotea
kabla na wakapotosha wengi na wakapotea njia iliyo sawa.”
لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ﴿٧٨﴾
78. Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israaiyl kwa
lisani ya Daawuwd na ‘Iysaa mwana wa Maryam. Hivyo ni kwa sababu ya
(kuendelea) kuasi kwao na walikuwa wakitaadi.
كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ﴿٧٩﴾
79. Walikuwa hawakatazani munkari waliyofanya. Uovu ulioje waliyokuwa wakiyafanya.
تَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنفُسُهُمْ أَن سَخِطَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ وَفِي الْعَذَابِ هُمْ خَالِدُونَ﴿٨٠﴾
80. Utawaona wengi miongoni mwao (Mayahudi) wanawafanya marafiki (wa
karibu, walinzi) wale waliokufuru. Ubaya ulioje yale yaliyowatangulizia
nafsi zao, (nayo ni) kuwa Allaah Amewaghadhibikia, na katika adhabu wao
ni wenye kudumu.
وَلَوْ
كَانُوا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالنَّبِيِّ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مَا
اتَّخَذُوهُمْ أَوْلِيَاءَ وَلَـٰكِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ﴿٨١﴾
81. Na lau wangelikuwa wanamwamini Allaah na (huyu) Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kwake, wasingeliwafanya hao marafiki wandani na ushirikiano, lakini wengi miongoni mwao ni mafasiki.
لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا ۖ وَلَتَجِدَنَّ أَقْرَبَهُم مَّوَدَّةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ﴿٨٢﴾
82. Bila shaka utawakuta walio maadui zaidi kuliko watu (wote) kwa
wale walioamini, ni Mayahudi na wale washirikina. Na bila shaka
utawakuta walio karibu zaidi kwa mapenzi kwa Waumini ni wale wanaosema:
“Sisi ni Manaswara.” Hivyo ni kwa kuwa miongoni mwao kuna Qissiysiyna (Makasisi) na Ruhbaan (Wamonaki - watawa) na kwamba wao hawatakabari.
وَإِذَا سَمِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَى الرَّسُولِ تَرَىٰ أَعْيُنَهُمْ تَفِيضُ مِنَ الدَّمْعِ مِمَّا عَرَفُوا مِنَ الْحَقِّ ۖ يَقُولُونَ رَبَّنَا آمَنَّا فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨٣﴾
83. Na wanaposikia yale yaliyoteremshwa kwa Rasuli utaona macho yao
yanachururika machozi kutokana na yale waliyoyatambua ya haki. Wanasema:
“Rabb (Mola) wetu tumeamini, basi Tuandike pamoja na wenye kushuhudia.”
وَمَا
لَنَا لَا نُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا جَاءَنَا مِنَ الْحَقِّ وَنَطْمَعُ
أَن يُدْخِلَنَا رَبُّنَا مَعَ الْقَوْمِ الصَّالِحِينَ ﴿٨٤﴾
84. “Na kwa nini Tusimwamini Allaah na haki iliyotufikia na hali tunatumai Rabb (Mola) wetu Atuingize (Jannah) pamoja na Swalihina?”
فَأَثَابَهُمُ اللَّـهُ بِمَا قَالُوا جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٥﴾
85. Basi Allaah Akawalipa kwa yale waliyoyasema, Jannaat zipitizao chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Na hiyo ndio jazaa ya wafanyao ihsaan.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿٨٦﴾
86. Na wale waliokufuru na wakazikadhibisha Aayaat (na ishara, dalili) Zetu hao ni watu wa (Moto wa) Al-Jahiym.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحَرِّمُوا طَيِّبَاتِ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٨٧﴾
87. Enyi mlioamini! Msiharamishe vizuri Aliyokuhalalishieni Allaah, na wala msitaadi. Hakika Allaah Hapendi wenye kutaadi.
وَكُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي أَنتُم بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿٨٨﴾
88. Na kuleni katika vile Alivyowaruzuku Allaah vya halaal na vizuri. Na mcheni Allaah Ambaye nyinyi mnamwamini.
لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ
فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا
تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٨٩﴾
89. Allaah Hatokuchukulieni kukuadhibuni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakuchukulieni kwa (kuvunja) viapo mlivyoapa kwa niyyah
mlioifunga thabiti. Basi kafara yake (ya kuvunja viapo hivi) ni kulisha
maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu, au kuwavisha
nguo, au kuacha huru mtumwa. Lakini asiyeweza kupata (moja katika hayo),
basi afunge Swiyaam siku tatu. Hiyo ndio kafara ya viapo vyenu
mnapoapa. Na hifadhini viapo vyenu (msiape kila mara). Hivyo ndivyo
Allaah Anavokubainishieni Aayaat (na hukmu) Zake mpate kushukuru.
يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ
وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ
فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾
90. Enyi mlioamini! Hakika ulevi na kamari na (kuabudu) masanamu, na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli; (yote hayo) ni rijsun (uchafu) katika kitendo cha shaytwaan; basi jiepusheni navyo, mpate kufaulu.
إِنَّمَا
يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ
فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ
الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾
91. Hakika shaytwaan anataka kukutilieni baina yenu uadui na bughudha
katika ulevi na kamari na akuzuieni na kumdhukuru Allaah na (akuzuieni
pia) Swalaah; basi je mtaacha (maasi hayo)?
وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَاحْذَرُوا ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿٩٢﴾
92. Na mtiini Allaah na mtiini Rasuli na tahadharini! Mkikengeuka,
basi jueni kwamba juu ya Rasuli Wetu ni (jukumu tu la) kufikisha ujumbe
bayana.
لَيْسَ
عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا
طَعِمُوا إِذَا مَا اتَّقَوا وَّآمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ثُمَّ
اتَّقَوا وَّآمَنُوا ثُمَّ اتَّقَوا وَّأَحْسَنُوا ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿٩٣﴾
93. Hakuna lawama juu ya wale walioamini na wakatenda mema katika
vile walivyokula (kabla ya kuharimishwa) ikiwa watakuwa na taqwa na
wakaamini na wakatenda mema; kisha wakawa na taqwa na wakaamini, kisha
wakawa na taqwa na wakafanya ihsaan. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.
يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَيَبْلُوَنَّكُمُ اللَّـهُ بِشَيْءٍ مِّنَ
الصَّيْدِ تَنَالُهُ أَيْدِيكُمْ وَرِمَاحُكُمْ لِيَعْلَمَ اللَّـهُ مَن
يَخَافُهُ بِالْغَيْبِ ۚ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٩٤﴾
94. Enyi mlioamini! Bila shaka Allaah Atakujaribuni kwa baadhi ya
wanyama wa kuwinda inayowafikia mikono yenu na mikuki yenu, ili Allaah
Ajue mwenye kumkhofu kwa ghayb. Na atakayetaadi baada ya hayo, basi atapata adhabu iumizayo.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْتُلُوا الصَّيْدَ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۚ
وَمَن قَتَلَهُ مِنكُم مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاءٌ مِّثْلُ مَا قَتَلَ مِنَ
النَّعَمِ يَحْكُمُ بِهِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ هَدْيًا بَالِغَ
الْكَعْبَةِ أَوْ كَفَّارَةٌ طَعَامُ مَسَاكِينَ أَوْ عَدْلُ ذَٰلِكَ
صِيَامًا لِّيَذُوقَ وَبَالَ أَمْرِهِ ۗ عَفَا اللَّـهُ عَمَّا سَلَفَ ۚ وَمَنْ عَادَ فَيَنتَقِمُ اللَّـهُ مِنْهُ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٩٥﴾
95. Enyi mlioamini! Msiue mawindo na hali mko katika ihraam.
Na atakayemuua (mnyama) miongoni mwenu kwa kusudi, basi malipo yake
itakuwa (kuchinja) kilicho sawa na alichokiua katika wanyama (wa mifugo
wa malishoni). Ahukumu kwacho (watu) wawili walio waadilifu miongoni
mwenu. Mnyama huyo afikishwe Ka’bah (akachinjwe), au kafara ya kulisha
maskini, au badala ya hayo, kufunga swiyaam ili aonje matokeo
maovu ya jambo lake. Allaah Ameshasamehe yaliyopita; na yeyote
atakayerudia (kufanya) tena, basi Allaah Atamlipizia (adhabu). Na Allaah
ni ‘Aziyz (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika), Mwenye kulipiza.
أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ الْبَحْرِ وَطَعَامُهُ مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِلسَّيَّارَةِ ۖ وَحُرِّمَ عَلَيْكُمْ صَيْدُ الْبَرِّ مَا دُمْتُمْ حُرُمًا ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٩٦﴾
96. Mmehalalishiwa mawindo ya bahari na chakula chake ni manufaa
kwenu na kwa wasafiri. Na mmeharamishiwa mawindo ya nchi kavu madamu
mtakuwa katika ihraam. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake (Pekee) mtakusanywa.
جَعَلَ اللَّـهُ الْكَعْبَةَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ قِيَامًا لِّلنَّاسِ وَالشَّهْرَ الْحَرَامَ وَالْهَدْيَ وَالْقَلَائِدَ ۚ ذَٰلِكَ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَأَنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٩٧﴾
97. Allaah Amejaalia Ka’bah Nyumba Tukufu kuwa simamio (tegemeo) la
watu, na (pia Ameijaalia) miezi mitukufu na wanyama wa kafara (dhabihu)
na vigwe (alama ya waliokusudiwa kafara). Hivyo ili mpate kujua kuwa
Allaah Anajua yale yaliyomo mbinguni na ardhini na kwamba Allaah ni kwa
kila kitu ‘Aliym (Mjuzi).
اعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ وَأَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٩٨﴾
98. Jueni kuwa Allaah ni Mkali wa kuakibu na kwamba Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).
مَّا عَلَى الرَّسُولِ إِلَّا الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا تَكْتُمُونَ ﴿٩٩﴾
99. Hapana (jukumu) juu ya Rasuli ila ubalighisho wa ujumbe. Na Allaah Anayajua yale mnayoyadhihirisha na yale mnayoyaficha.
قُل لَّا يَسْتَوِي الْخَبِيثُ وَالطَّيِّبُ وَلَوْ أَعْجَبَكَ كَثْرَةُ الْخَبِيثِ ۚ فَاتَّقُوا اللَّـهَ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Sema: “Haviwi sawasawa khabiyth (watu waovu na kila uovu; kauli, amali n.k) na twayyib (watu wema na kila zuri) japokuwa utakupendekezea wingi wa khabiyth”. Basi mcheni Allaah, enyi wenye akili ili mpate kufaulu.
يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ
لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْأَلُوا عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ الْقُرْآنُ
تُبْدَ لَكُمْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهَا ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٠١﴾
101. Enyi mlioamini! Msiulizie mambo ambayo mkifichuliwa
yatakusikitisheni. Na mkiyaulizia pale inapoteremshwa Qur-aan
mtafichuliwa. Allaah Ameyasamehe hayo. Na Allaah ni Ghafuwrun-Haliym (Mwingi wa kughufuria - Mpole wa kuwavumilia waja).
قَدْ سَأَلَهَا قَوْمٌ مِّن قَبْلِكُمْ ثُمَّ أَصْبَحُوا بِهَا كَافِرِينَ ﴿١٠٢﴾
102. Walikwishayauliza (mambo) hayo watu wa kabla yenu, kisha wakawa kwayo ni makafiri.
مَا جَعَلَ اللَّـهُ مِن بَحِيرَةٍ وَلَا سَائِبَةٍ وَلَا وَصِيلَةٍ وَلَا حَامٍ ۙ وَلَـٰكِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۖ وَأَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿١٠٣﴾
103. Allaah Hakujaalia (uharamu wowote wa) bahiyrah (ngamia aliyezaa matumbo matano), wala saaibah (ngamia aliyeachiliwa kwa nadhiri), wala waswiylah (kondoo aliyezaa matumbo saba), wala haam (fahali lililozalisha matumbo kumi), lakini wale waliokufuru wanamtungia Allaah uongo, na wengi wao hawatumii akili.
وَإِذَا
قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ
قَالُوا حَسْبُنَا مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۚ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ ﴿١٠٤﴾
104. Na wanapoambiwa: “Njooni (katika) yale Aliyoyateremsha Allaah na
kwa Rasuli” Husema: “Yanatutosheleza yale tuliyowakuta nayo baba zetu”.
Je, japokuwa walikuwa baba zao hawajui chochote na wala hawakuongoka?
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٠٥﴾
105. Enyi mlioamini! Ni juu yenu (majukumu ya) nafsi zenu.
Hawakudhuruni waliopotoka ikiwa mmeongoka. Kwa Allaah Pekee ni marejeo
yenu nyote, kisha Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
يَا
أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا شَهَادَةُ بَيْنِكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ
الْمَوْتُ حِينَ الْوَصِيَّةِ اثْنَانِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ أَوْ
آخَرَانِ مِنْ غَيْرِكُمْ إِنْ أَنتُمْ ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ
فَأَصَابَتْكُم مُّصِيبَةُ الْمَوْتِ ۚ
تَحْبِسُونَهُمَا مِن بَعْدِ الصَّلَاةِ فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ إِنِ
ارْتَبْتُمْ لَا نَشْتَرِي بِهِ ثَمَنًا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۙ وَلَا نَكْتُمُ شَهَادَةَ اللَّـهِ إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الْآثِمِينَ ﴿١٠٦﴾
106. Enyi mlioamini! Ushahidi (uweko kushuhudiwa) baina yenu
yanapohudhuria mauti (kwa) mmoja wenu wakati anapousia. Waweko
(mashahidi) wawili wenye uadilifu miongoni mwenu; au wawili wengine
ghairi yenu (wasio Waislamu) mnapokuwa safarini ukakufikeni msiba wa
mauti. Muwazuie (wawili hao) baada ya Swalaah, na waape kwa (jina la)
Allaah mkitilia shaka (ushahidi wao. Hivyo waseme): “Hatutobadilisha
kwayo (viapo vyetu) kwa thamani yoyote ile japo akiwa ni jamaa yetu wa
karibu. Na wala hatutoficha ushuhuda wa Allaah. (Kwani tukifanya
hivyo) hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye kutenda dhambi.”
فَإِنْ
عُثِرَ عَلَىٰ أَنَّهُمَا اسْتَحَقَّا إِثْمًا فَآخَرَانِ يَقُومَانِ
مَقَامَهُمَا مِنَ الَّذِينَ اسْتَحَقَّ عَلَيْهِمُ الْأَوْلَيَانِ
فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ لَشَهَادَتُنَا أَحَقُّ مِن شَهَادَتِهِمَا وَمَا
اعْتَدَيْنَا إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠٧﴾
107. Ikigundilikana kwamba hao wawili wana hatia ya dhambi (kwa
kusema uongo katika waliyoyashuhudia); basi wawili wengine wasimame
mahali pao katika walio karibu zaidi (na mrithiwa) miongoni mwa
waliokuwa na haki ki-shariy’ah; basi waape kwa (jina la) Allaah
(kwa kusema): “Bila shaka ushahidi wetu ni wa kweli zaidi kuliko
ushahidi (wa wawili) wao; nasi hatukutaadi; (ikiwa tumefanya hivyo),
hakika hapo tutakuwa miongoni mwa madhalimu.
ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يَأْتُوا بِالشَّهَادَةِ عَلَىٰ وَجْهِهَا أَوْ يَخَافُوا أَن تُرَدَّ أَيْمَانٌ بَعْدَ أَيْمَانِهِمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاسْمَعُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴿١٠٨﴾
108. Hivyo inaelekea zaidi ya kwamba watatoa ushahidi kama ipasavyo
au watakhofu visije vikaletwa viapo (vingine) baada ya viapo vyao. Na
mcheni Allaah na sikizeni! Na Allaah Haongoi watu mafasiki.
يَوْمَ يَجْمَعُ اللَّـهُ الرُّسُلَ فَيَقُولُ مَاذَا أُجِبْتُمْ ۖ قَالُوا لَا عِلْمَ لَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١٠٩﴾
109. (Tahadharini) Siku Allaah Atakayowakusanya Rasuli na Kuwaambia:
“Mlijibiwa nini?” (Rasuli) Watasema: “Hatuna ujuzi nalo; hakika Wewe
Ndiye ‘Allaamu (Mjuzi) wa ghayb.
إِذْ
قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ اذْكُرْ نِعْمَتِي عَلَيْكَ
وَعَلَىٰ وَالِدَتِكَ إِذْ أَيَّدتُّكَ بِرُوحِ الْقُدُسِ تُكَلِّمُ
النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا ۖ وَإِذْ عَلَّمْتُكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ۖ وَإِذْ تَخْلُقُ مِنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ بِإِذْنِي فَتَنفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِي ۖ وَتُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ تُخْرِجُ الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِي ۖ
وَإِذْ كَفَفْتُ بَنِي إِسْرَائِيلَ عَنكَ إِذْ جِئْتَهُم بِالْبَيِّنَاتِ
فَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ
﴿١١٠﴾
110. (Siku) Allaah Ataposema: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Kumbuka neema Yangu juu yako na juu ya mama yako; Nilipokusaidia kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام;
unasemesha watu katika utoto na utuuzimani; na (kumbuka) Nilipokufunza
Kitabu na Hikmah na Tawraat na Injiyl; na (kumbuka pale) ulipotengeneza
kutokana na udongo kama umbo la ndege kwa idhini Yangu; ukapulizia
likawa ndege kwa idhini Yangu; na ulipowaponyesha vipofu na ubarasi kwa
idhini Yangu; na ulipowatoa wafu (kutoka makaburini mwao) kwa idhini
Yangu; na Nilipowazuia wana wa Israaiyl dhidi yako (kutaka kuua)
ulipowajia kwa hoja bayana; wakasema wale waliokufuru miongoni mwao:
“Haya si chochote ila ni sihiri bayana.”
وَإِذْ أَوْحَيْتُ إِلَى الْحَوَارِيِّينَ أَنْ آمِنُوا بِي وَبِرَسُولِي قَالُوا آمَنَّا وَاشْهَدْ بِأَنَّنَا مُسْلِمُونَ ﴿١١١﴾
111. Na (kumbuka pale) Nilipowatia ilhamu Al-Hawariyyiyna (wafuasi, Answaar
wako) kwamba: “Niaminini Mimi na Rasuli Wangu.” Wakasema: “Tumeamini na
shuhudia kwamba sisi ni Waislamu (tuliojisalimisha kwa Allaah).”
إِذْ
قَالَ الْحَوَارِيُّونَ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ هَلْ يَسْتَطِيعُ
رَبُّكَ أَن يُنَزِّلَ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ ۖ قَالَ اتَّقُوا اللَّـهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١١٢﴾
112. (Kumbuka pale) waliposema Al-Hawariyyiyna: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je Anaweza Rabb (Mola) wako Kututeremshia maaidah (meza iliyotandazwa chakula) kutoka mbinguni?” (‘Iysaa) Akasema: “Mcheni Allaah, kama nyinyi ni Waumini.”
قَالُوا
نُرِيدُ أَن نَّأْكُلَ مِنْهَا وَتَطْمَئِنَّ قُلُوبُنَا وَنَعْلَمَ أَن
قَدْ صَدَقْتَنَا وَنَكُونَ عَلَيْهَا مِنَ الشَّاهِدِينَ ﴿١١٣﴾
113. (Al-Hawariyyiyna) Wakasema: “Tunataka kula
katika hicho; na (ili) nyoyo zetu zitulie; na tujue kwamba kwa yakini
umetuambia kweli; na kwayo tuwe miongoni wa wanaoshuhudia.”
قَالَ
عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ اللَّـهُمَّ رَبَّنَا أَنزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً
مِّنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيدًا لِّأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً
مِّنكَ ۖ وَارْزُقْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١٤﴾
114. Akasema ‘Iysaa mwana wa Maryam: “Ee Allaah, Rabb (Mola) wetu, Tuteremshie maaidah kutoka mbinguni (ili) iwe kwetu ni sikukuu kwa wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu; na iwe Aayah (ishara, hoja) itokayo Kwako; basi Turuzuku; kwani Wewe ni Mbora wa wenye kuruzuku”.
قَالَ اللَّـهُ إِنِّي مُنَزِّلُهَا عَلَيْكُمْ ۖ فَمَن يَكْفُرْ بَعْدُ مِنكُمْ فَإِنِّي أُعَذِّبُهُ عَذَابًا لَّا أُعَذِّبُهُ أَحَدًا مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿١١٥﴾
115. Akasema Allaah: “Hakika Mimi Nitaiteremsha kwenu; (lakini)
atakayekufuru miongoni mwenu baada ya hapo; basi hakika Nitamuadhibu
adhabu (ambayo) Sitomuadhibu mmoja yeyote katika walimwengu.”
وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١١٦﴾
116. Na (Tahadhari Siku) Allaah Atakaposema: “Ee ‘Iysaa mwana wa
Maryam! Je, wewe uliwaambia watu: “Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni
miungu miwili pasi naya Allaah?” (‘Iysaa) Atasema: “Subhaanak
(Utakasifu ni Wako)! Hainipasi mimi kusema yasiyo kuwa haki kwangu;
ikiwa nimesema hayo basi kwa yakini Ungeliyajua; Unayajua yale yote
yaliyomo katika nafsi yangu; na wala (mimi) sijui yale yaliyomo katika
Nafsi Yako; hakika Wewe ni ‘Allaamu (Mjuzi) wa ghayb.
مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلَّا مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۚ وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿١١٧﴾
117. “Sijawaambia (lolote) ila yale Uliyoniamrisha kwayo kwamba: Mwabuduni Allaah Rabb (Mola) wangu na Rabb wenu. Na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao. Uliponichukua juu (mbinguni) Ulikuwa Wewe Ar-Raqiyba (Mwenye kuchunga) juu yao. Na Wewe juu ya kila kitu ni Shahiyd” (Mwenye kushuhudia).
إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾
118. “Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni waja Wako; na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Al-‘Aziyzul-Hakiym” (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye hikmah wa yote).
قَالَ اللَّـهُ هَـٰذَا يَوْمُ يَنفَعُ الصَّادِقِينَ صِدْقُهُمْ ۚ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١١٩﴾
119. Allaah Atasema: “Hii ndiyo Siku itakayowafaa as-Swaadiqiyna ukweli wao; watapata Jannaat zipitazo chini yake mito; ni wenye kudumu humo abadi. Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Huko ni kufuzu adhimu.”
لِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا فِيهِنَّ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٢٠﴾
120. Ni wa Allaah (Pekee) ufalme wa mbingu na ardhi na yale yote yaliyomo humo. Naye juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).
Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com