Al-Humazah (104)

سُورَةُ  الْهُمَزَة
Al-Humazah (104)

(Imeteremka Makka)

 
Katika Sura hii kipo kitisho kikubwa kwa mwenye kuzoea kuwakebehi watu kwa ishara au kwa maneno, mwenye kukusanya mali mengi, akayahisabu kwa ajili ya fakhari, na kudhani kuwa mali yake yatambakisha milele duniani.
Na humo vile vile lipo onyo kubwa kwa hao kuwa watatiwa kwenye Moto mkali unao vuruga miili yao na nyoyo zao, na wanafungiwa milango, na juu ya hivyo watafungwa pingu humo basi hawataweza kutaharaki wala kutoka.

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ ﴿١﴾

1. Ole kwa kila mwenye kukashifu (watu) kwa kusengenya, mfedheheshaji kwa ishara (anayekejeli watu kwa uso, macho na mikono).

الَّذِي جَمَعَ مَالًا وَعَدَّدَهُ ﴿٢﴾

2. Ambaye amekusanya mali na kuyahesabu.

يَحْسَبُ أَنَّ مَالَهُ أَخْلَدَهُ ﴿٣﴾

3. Anadhani kwamba mali yake itamdumisha.

كَلَّا ۖ لَيُنبَذَنَّ فِي الْحُطَمَةِ ﴿٤﴾

4. Hasha! Atavurumisha katika Al-Hutwamah.

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْحُطَمَةُ ﴿٥﴾

5. Na nini kitakujulisha ni nini hiyo Al-Hutwamah.

نَارُ اللَّـهِ الْمُوقَدَةُ ﴿٦﴾

6. Ni Moto wa Allaah uliowashwa.

الَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى الْأَفْئِدَةِ ﴿٧﴾

7. Ambao unaopanda nyoyoni

إِنَّهَا عَلَيْهِم مُّؤْصَدَةٌ ﴿٨﴾

8. Hakika juu yao utafungiwa (wasitoke).

فِي عَمَدٍ مُّمَدَّدَةٍ ﴿٩﴾

9. Katika nguzo zilotanuliwa.

waliopotea.


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com