029 - Hadiyth Ya 29: Aliyekamilika Iymaan Kwa Tabia Na Kumfanyia Wema Mke




عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا, وَخِيَارُكُمْ خِيَارُكُمْ لِنِسَائِهِمْ خُلُقًا)) الترمذي وقال: حديث حسن صحيح
 
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muumin aliyekamilika Iymaan ni aliye na tabia njema kabisa, na wabora wenu ni walio bora kwa wake zao kwa tabia)).[1]
 
Mafunzo Na Hidaaya:
 
  1. Uislamu unasisitiza kuwa na tabia njema kwa kila mtu.
 
  1. Mume anasisitizwa kumfanyia wema mkewe katika maisha ya ndoa, si kumfanyia uovu. [Ar-Ruum 30: 21] ((Wala msisahau fadhila baina yenu)).[2]
 
 
وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ
 
Na kaeni nao kwa wema[3]
 
 
  1. Inapasa kuweko subira baina ya mume na mke katika mitihani inayowakabili ya maisha baina yao. [((Na mkisubiri ni kheri kwenu))[4]

  1. Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kigezo bora kabisa katika kuamiliana na wake [Al-Ahzaab 33: 2]. [Hadiyth: ((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa mke wake, na mimi ni mbora kwa watu wangu wa nyumbani [ahli]))[5] ((Mwanamke ameumbwa kwa ubavu, na sehemu iliyopinda ya ubavu ni juu yake, ukijaribu kuunyoosha utauvunja, na lau utauacha utaendelea kupinda, nakuusieni [kuwafanyia wema]) wake zenu))[6] ((Allaah, Allaah, kwa wanawake,  hao ni wasaidizi wenu walio kwenye mikono yenu, mmewachukuwa kama ni amana kutoka kwa Allaah, na imekuwa halali tupu zao kwenu kwa neno lake Allaah  [Iyjaab na Qubuwl])).[7]
 
 
 



[1]  At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Swahiyh Hasan.
[2]  Al-Baqarah (2: 237).
[3]  An-Nisaa (4: 19).
[4]  An-Nisaa (4: 25).
[5]  Ibn Maajah na Ad-Daarimiy.
[6]  Al-Bukhaariy na Muslim.
[7]  Muslim, Abu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad.