Az-Zukhruf: 43

  الزُّخْرُف
Az-Zukhruf: 43

(Imeteremka Makka)


Imeanzia Sura hii kwa harufi mbili za alifbete, na ikafuatia kwa kuitaja Qur'ani na kueleza cheo chake kwa Mwenyezi Mungu. Kisha Sura ikaingia kubainisha msimamo wa wale wanao zifanyia maskhara Risala za Mitume wao, na ikazileta dalili nyingi za kuthibitisha Imani ya Mwenyezi Mungu pekee. Na juu ya hoja hizo wao wakamzulia Mwenyezi Mungu kuwa ana washirika, na wakamfanya kuwa ana watoto wa kike, na wao wanao wa kiume. Na walipo ishiwa na hoja wakashikilia mila za baba zao.
Kisha Sura ikasimulia kisa cha Ibrahim, na ikafuatiliza kule kuyaona makuu makafiri wa Makka ya kwamba Qur'ani iliteremka juu ya Muhammad, wala isiteremke juu ya mmoja katika wakuu wa miji yao miwili. Hayo ni kama kwamba wao ndio wanao zigawanya fadhila za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu alikwisha wagawia maisha yao ya duniani, kwa kuwa wao wenyewe wameshindwa hayo. Kisha Sura ikathibitisha kwamba lau kuwa si kuchukia wasije watu wote wakakufuru basi bila ya shaka angeli mpa kafiri starehe na mapambo na uzuri wote wa duniani. Kadhaalika Sura imebainisha kwamba mwenye kupuuza Haki Mwenyezi Mungu humsalitisha na Shet'ani amwongoze kwenye maangamio. Kisha Sura inasimulia kisa cha Musa na Firauni, na alivyo ghurika Firauni na ufalme wake, na yaliyo mteremkia Firauni na kaumu yake ya mateso ya Mwenyezi Mungu. Na hayo akafuatiwa  kutajwa Bin Maryamu, na kwamba yeye ni mja aliye neemeshwa na Mwenyezi Mungu, na akawaita watu wende kwenye Njia Iliyo Nyooka. Na baada ya kuonya  kwa adhabu ya Siku ya Kiyama itayo wapata walio dhulumu, na kubashiriwa Waumini kuwa watapata Pepo ambayo ndani yake macho yao yatatua, Sura inakhitimisha kueleza kuwa Ufalme wa Mwenyezi Mungu umeenea kote, na hao walio washirikisha naye hawanalo wawezalo. Basi, ewe Muhammad! Wapuuzilie mbali, na useme: Salamu! Watakuja jua!



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
حم﴿١﴾
1. Haa Miym.


وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ﴿٢﴾
2. Na Kitabu kinachobainisha.


إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ﴿٣﴾
3. Hakika Sisi Tumefanya Qur-aan ya Kiarabu ili mpate kutia akilini.


وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ﴿٤﴾
4. Na hakika hii (Qur-aan) iko katika Mama wa Kitabu Kwetu, (Lawhim-Mahfuudhw) bila shaka imetukuka, yenye hikmah.


أَفَنَضْرِبُ عَنكُمُ الذِّكْرَ صَفْحًا أَن كُنتُمْ قَوْمًا مُّسْرِفِينَ﴿٥﴾
5. Je, basi Tuwaachie mbali na ukumbusho kuwa kupuuza kwa vile nyinyi mmekuwa wapindukao mipaka?


وَكَمْ أَرْسَلْنَا مِن نَّبِيٍّ فِي الْأَوَّلِينَ﴿٦﴾
6. Na Manabii wangapi Tumewatuma kwa watu wa awali?



وَمَا يَأْتِيهِم مِّن نَّبِيٍّ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٧﴾
7. Na hawakuwafikia Nabiy yeyote isipokuwa walikuwa wakimfanyia istihzai.


فَأَهْلَكْنَا أَشَدَّ مِنْهُم بَطْشًا وَمَضَىٰ مَثَلُ الْأَوَّلِينَ﴿٨﴾
8. Basi Tukawaangamiza walio na nguvu zaidi kuliko wao na imeshapita mfano wa watu wa awali.


وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ خَلَقَهُنَّ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ﴿٩﴾
9. Na ukiwauliza:  “Ni nani yule aliyeumba mbingu na ardhi?” Bila shaka watasema: “Ameziumba Al-Aziyzul-‘Aliym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mjuzi wa yote).


الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ مَهْدًا وَجَعَلَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴿١٠﴾
10. Ambaye Amekufanyieni ardhi kuwa tandiko, na Akakufanyieni humo njia ili mpate muongoze (mnakotaka).


وَالَّذِي نَزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً بِقَدَرٍ فَأَنشَرْنَا بِهِ بَلْدَةً مَّيْتًا ۚ كَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ﴿١١﴾
11. Na Ambaye Ameteremsha kutoka mbinguni maji kwa kipimo, Tukafufua kwayo nchi iliyokufa, na hivyo ndivyo mtakavyotolewa (makaburini).


وَالَّذِي خَلَقَ الْأَزْوَاجَ كُلَّهَا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ الْفُلْكِ وَالْأَنْعَامِ مَا تَرْكَبُونَ﴿١٢﴾
12. Na Ambaye Ameumba kila kitu jozi (dume na jike), na Akakufanyieni katika merikebu na wanyama mnaowapanda.


لِتَسْتَوُوا عَلَىٰ ظُهُورِهِ ثُمَّ تَذْكُرُوا نِعْمَةَ رَبِّكُمْ إِذَا اسْتَوَيْتُمْ عَلَيْهِ وَتَقُولُوا سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَـٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ﴿١٣﴾
13. Ili mlingamane sawasawa juu ya mgongo wake, kisha mkumbuke neema ya Rabb (Mola) wenu mtakapokaa sawasawa juu yao, na mseme: “Subhaana (Utakasifu) ni wa Ambaye Ametutiishia haya, na tusingeliweza wenyewe kumdhibiti.


وَإِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ﴿١٤﴾
14. “Na hakika kwa Rabb (Mola) wetu, bila shaka tutarejea.”


وَجَعَلُوا لَهُ مِنْ عِبَادِهِ جُزْءًا ۚ إِنَّ الْإِنسَانَ لَكَفُورٌ مُّبِينٌ﴿١٥﴾
15. Na wakamfanyia kati ya waja Wake sehemu (kuwa Allaah Ana watoto), hakika insani bila shaka ni mwingi wa kukufuru, aliye bayana.


أَمِ اتَّخَذَ مِمَّا يَخْلُقُ بَنَاتٍ وَأَصْفَاكُم بِالْبَنِينَ﴿١٦﴾
16. Je, Amejichukulia katika Aliowaumba mabanati, na Akakuchagulieni nyinyi watoto wa kiume?


وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِمَا ضَرَبَ لِلرَّحْمَـٰنِ مَثَلًا ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ﴿١٧﴾
17. Na anapobashiriwa mmoja wao kwa (binti) aliyepigiwa mfano Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah), husawijika uso wake naye ni mwenye kuzuia ghadhabu na huzuni.


أَوَمَن يُنَشَّأُ فِي الْحِلْيَةِ وَهُوَ فِي الْخِصَامِ غَيْرُ مُبِينٍ﴿١٨﴾
18. Ah! Yule aliyelelewa katika mapambo (mwanamke) naye katika mabishano si mbainifu?


وَجَعَلُوا الْمَلَائِكَةَ الَّذِينَ هُمْ عِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ إِنَاثًا ۚ أَشَهِدُوا خَلْقَهُمْ ۚ سَتُكْتَبُ شَهَادَتُهُمْ وَيُسْأَلُونَ﴿١٩﴾
19. Na wakawafanya Malaika ambao ni waja wa Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) kuwa ni wa kike. Je, kwani wameshuhudia uumbaji wao?  Utaandikwa ushahidi wao, na wataulizwa.


وَقَالُوا لَوْ شَاءَ الرَّحْمَـٰنُ مَا عَبَدْنَاهُم ۗ مَّا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ﴿٢٠﴾
20. Na wakasema: “Angelitaka Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) tusingeliyaabudu (hii miungu yetu). Hawana elimu yoyote wa hayo, hawana isipokuwa wanabuni uongo.


أَمْ آتَيْنَاهُمْ كِتَابًا مِّن قَبْلِهِ فَهُم بِهِ مُسْتَمْسِكُونَ﴿٢١﴾
21. Au Tumewapa Kitabu kabla yake (hii Qur-aan), basi wao kwacho wanakishikilia?


بَلْ قَالُوا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّهْتَدُونَ﴿٢٢﴾
22. Bali wamesema: “Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini na hakika sisi tunaongoka kwa nyayo zao.”


وَكَذَٰلِكَ مَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّقْتَدُونَ﴿٢٣﴾
23. Na hivyo ndivyo Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika mji mwonyaji yeyote yule isipokuwa wamesema matajiri wake wenye starehe na taanusi: “Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini, na hakika sisi kwa nyao zao, ni wenye kufuata.”


قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكُم بِأَهْدَىٰ مِمَّا وَجَدتُّمْ عَلَيْهِ آبَاءَكُمْ ۖ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ﴿٢٤﴾
24. (Kila Rasuli) Alisema: “Japo kama nimekujieni na uongofu zaidi kuliko ambao mliyowakuta nao baba zenu?” Wakasema: “Hakika sisi kwa yale mliyotumwa nayo ni wenye kuyakanusha.”


فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ﴿٢٥﴾
25. Basi Tukawalipizia, kisha tazama vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha.


وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ﴿٢٦﴾
26. Na (taja pale) Ibraahiym alipomwambia baba yake na watu wake: “Hakika mimi mwenye kujitoa katika dhima na yale mnayoyaabudu.


إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ﴿٢٧﴾
27. “Isipokuwa Ambaye Ameniumba, basi hakika Yeye Ataniongoa.”


وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿٢٨﴾
28. Na akalifanya neno (la ilaaha illaa-Allaah) lenye kubakia katika kizazi chake ili wapate kurejea.


بَلْ مَتَّعْتُ هَـٰؤُلَاءِ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ جَاءَهُمُ الْحَقُّ وَرَسُولٌ مُّبِينٌ﴿٢٩﴾
29. Bali Niliwastarehesha hawa (makafiri wa Makkah) na baba zao mpaka ikawajia haki (Qur-aan) na Rasuli anayebainisha.


وَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ وَإِنَّا بِهِ كَافِرُونَ﴿٣٠﴾
30. Na ilipowajia haki, walisema: “Hii (Qur-aan) ni sihiri na hakika sisi ni wenye kuikanusha.”


وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ هَـٰذَا الْقُرْآنُ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنَ الْقَرْيَتَيْنِ عَظِيمٍ﴿٣١﴾
31. Na wakasema: “Kwa nini isiteremshwe hii Qur-aan juu ya mtu wa kikabaila kutoka miji miwili?”


أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَتَ رَبِّكَ ۚ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُم مَّعِيشَتَهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِّيَتَّخِذَ بَعْضُهُم بَعْضًا سُخْرِيًّا ۗ وَرَحْمَتُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ﴿٣٢﴾
32. Je, wao wanaigawanya Rahmah za Rabb (Mola) wako? Sisi Tumegawanya baina yao maisha yao katika uhai wa dunia, na Tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengineo daraja (za vyeo) ili wawafanye baadhi yao kuwa watumishi wa wengineo. Na Rahmah ya Rabb wako ni bora kuliko wanayoyajumuisha.


وَلَوْلَا أَن يَكُونَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً لَّجَعَلْنَا لِمَن يَكْفُرُ بِالرَّحْمَـٰنِ لِبُيُوتِهِمْ سُقُفًا مِّن فِضَّةٍ وَمَعَارِجَ عَلَيْهَا يَظْهَرُونَ﴿٣٣﴾
33. Na lau isingelikuwa watu kuwa jamii moja (ya makafiri), Tungelifanya kwa ambaye anamkufuru Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) – kwa ajili ya nyumba zao - dari za fedha na ngazi (pia) wanazozipanda.


وَلِبُيُوتِهِمْ أَبْوَابًا وَسُرُرًا عَلَيْهَا يَتَّكِئُونَ﴿٣٤﴾
34. Na kwenye nyumba zao milango na makochi wanayoyaegemea.


وَزُخْرُفًا ۚ وَإِن كُلُّ ذَٰلِكَ لَمَّا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَالْآخِرَةُ عِندَ رَبِّكَ لِلْمُتَّقِينَ﴿٣٥﴾
35. Na mapambo ya dhahabu. Lakini hayo yote si chochote isipokuwa ni starehe ya uhai wa dunia. Na Aakhirah iliyo kwa Rabb (Mola) wako ni kwa wenye taqwa.


وَمَن يَعْشُ عَن ذِكْرِ الرَّحْمَـٰنِ نُقَيِّضْ لَهُ شَيْطَانًا فَهُوَ لَهُ قَرِينٌ﴿٣٦﴾
36. Na anayejifanya kipofu na ukumbusho wa Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah), Tunamwekea shaytwaan awe ndiye rafiki yake mwandani.


وَإِنَّهُمْ لَيَصُدُّونَهُمْ عَنِ السَّبِيلِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ﴿٣٧﴾
37. Na hakika wao (mashaytwaan) wanawazuia njia (ya uongofu) na wanafikiria kwamba wao wameongoka.


حَتَّىٰ إِذَا جَاءَنَا قَالَ يَا لَيْتَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ بُعْدَ الْمَشْرِقَيْنِ فَبِئْسَ الْقَرِينُ﴿٣٨﴾
38. Mpaka atakapotujia (Siku ya Qiyaamah), atasema (kumwambia rafiki yake): “Laiti ingelikuwa baina yangu na baina yako umbali wa Mashariki mbili (Mashariki na Magharibi), basi ubaya ulioje wa rafiki mwandani.”


وَلَن يَنفَعَكُمُ الْيَوْمَ إِذ ظَّلَمْتُمْ أَنَّكُمْ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ﴿٣٩﴾
39. (Itasemwa): “Haikufaeni chochote leo mlipodhulumu kwamba nyinyi katika adhabu ni wenye kushirikiana.”


أَفَأَنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ أَوْ تَهْدِي الْعُمْيَ وَمَن كَانَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٤٠﴾
40. Je, kwani wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unaweza kusikilizisha viziwi au kumuongoa kipofu na yule aliyekuwa katika upotofu bayana?


فَإِمَّا نَذْهَبَنَّ بِكَ فَإِنَّا مِنْهُم مُّنتَقِمُونَ﴿٤١﴾
41. Na hata kama Tukikuondoa (kukufisha ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi hakika Sisi ni Wenye kuwalipizia.


أَوْ نُرِيَنَّكَ الَّذِي وَعَدْنَاهُمْ فَإِنَّا عَلَيْهِم مُّقْتَدِرُونَ﴿٤٢﴾
42. Au Tukuonyesha yale Tuliyowatishia basi hakika Sisi ni Muqtadiruwn (Wenye Uwezo wa yote) juu yao.


فَاسْتَمْسِكْ بِالَّذِي أُوحِيَ إِلَيْكَ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٤٣﴾
43. Basi shikilia yale uliyofunuliwa Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), hakika wewe uko juu ya nia iliyonyooka.


وَإِنَّهُ لَذِكْرٌ لَّكَ وَلِقَوْمِكَ ۖ وَسَوْفَ تُسْأَلُونَ﴿٤٤﴾
44. Na hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni ukumbusho kwako na kwa watu wako na mtakuja ulizwa.


وَاسْأَلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رُّسُلِنَا أَجَعَلْنَا مِن دُونِ الرَّحْمَـٰنِ آلِهَةً يُعْبَدُونَ﴿٤٥﴾
45. Na waulize wale Tuliowatuma kabla yako miongoni mwa Rasuli Wetu; je, Tulifanya badala ya Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) miungu mingine iabudiwe?”


وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَقَالَ إِنِّي رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٤٦﴾
46. Na kwa yakini Tulimtuma Muwsaa kwa Aayaat (ishara, dalili) Zetu kwa Fir’awn na wakuu wake; akasema: “Hakika mimi ni Rasuli wa Rabb (Mola) wa walimwengu.”


فَلَمَّا جَاءَهُم بِآيَاتِنَا إِذَا هُم مِّنْهَا يَضْحَكُونَ﴿٤٧﴾
47. Basi alipowajia kwa Aayaat (ishara, hoja, dalili) Zetu tahamaki wao wanazicheka.


وَمَا نُرِيهِم مِّنْ آيَةٍ إِلَّا هِيَ أَكْبَرُ مِنْ أُخْتِهَا ۖ وَأَخَذْنَاهُم بِالْعَذَابِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿٤٨﴾
48. Na Hatukuwaonyesha Aayah (ishara) yoyote isipokuwa ni kubwa zaidi kuliko ya mwenziwe na Tukawachukua kwa adhabu ili wapate kurejea (kuamini).


وَقَالُوا يَا أَيُّهَ السَّاحِرُ ادْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ إِنَّنَا لَمُهْتَدُونَ﴿٤٩﴾
49. Na wakasema (kumwambia Muwsaa): “Ee mchawi! Tuombee kwa Rabb (Mola) wako kwa yale Aliyokuahidi kwako. Hakika sisi bila shaka tutaongoka.”


فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِذَا هُمْ يَنكُثُونَ﴿٥٠﴾
50. Lakini Tulipowaondoshea adhabu tahamaki wao wanavunja (ahadi).


وَنَادَىٰ فِرْعَوْنُ فِي قَوْمِهِ قَالَ يَا قَوْمِ أَلَيْسَ لِي مُلْكُ مِصْرَ وَهَـٰذِهِ الْأَنْهَارُ تَجْرِي مِن تَحْتِي ۖ أَفَلَا تُبْصِرُونَ﴿٥١﴾
51. Na Fir’awn akanadi kwa kaumu yake, akasema: “Enyi kaumu yangu! Je, kwani ufalme wa Misri si wangu! Na hii mito inapita chini yangu? Je, hamuoni?


أَمْ أَنَا خَيْرٌ مِّنْ هَـٰذَا الَّذِي هُوَ مَهِينٌ وَلَا يَكَادُ يُبِينُ﴿٥٢﴾
52. “Au mimi (si) bora kuliko huyu (Muwsaa) ambaye ni dhalili, na wala hakaribii kubainisha (kauli haifahamiki).


فَلَوْلَا أُلْقِيَ عَلَيْهِ أَسْوِرَةٌ مِّن ذَهَبٍ أَوْ جَاءَ مَعَهُ الْمَلَائِكَةُ مُقْتَرِنِينَ﴿٥٣﴾
53. “Basi kwanini asitupiwe vikuku vya dhahabu au wakaja pamoja naye Malaika wenye kuambatana (naye)?”


فَاسْتَخَفَّ قَوْمَهُ فَأَطَاعُوهُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ﴿٥٤﴾
54. Basi aliwachezea akili watu wake nao wakamtii. Hakika wao (wenyewe) walikuwa watu mafasiki.


فَلَمَّا آسَفُونَا انتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٥٥﴾
55. Basi walipotukasirisha; Tuliwalipizia, Tukawagharikisha wote.


فَجَعَلْنَاهُمْ سَلَفًا وَمَثَلًا لِّلْآخِرِينَ﴿٥٦﴾
56. Tukawafanya wenye kutangulia (kwenye adhabu) na mfano kwa wengineo.


وَلَمَّا ضُرِبَ ابْنُ مَرْيَمَ مَثَلًا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ﴿٥٧﴾
57. Na mwana wa Maryam (Nabiy ‘Iysaa) aliponukuliwa kama mfano, tahamaki watu wako wanaupigia kelele kuucheka.


وَقَالُوا أَآلِهَتُنَا خَيْرٌ أَمْ هُوَ ۚ مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ﴿٥٨﴾
58. Na wakasema: “Je, miungu yetu ni bora au yeye?” Hawakukupigia mfano huo (wa kulinganisha) isipokuwa tu kutaka kubisha. Bali wao ni watu makhasimu.


إِنْ هُوَ إِلَّا عَبْدٌ أَنْعَمْنَا عَلَيْهِ وَجَعَلْنَاهُ مَثَلًا لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ﴿٥٩﴾
59. Yeye (Nabiy ‘Iysaa) si chochote isipokuwa ni mja Tuliyemneemesha, na Tukamfanya ni mfano kwa wana wa Israaiyl.


وَلَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَا مِنكُم مَّلَائِكَةً فِي الْأَرْضِ يَخْلُفُونَ﴿٦٠﴾
60. Na lau Tungelitaka basi Tungeliwafanya miongoni mwenu (badili yenu) Malaika wanaofuatana halifa katika ardhi.


وَإِنَّهُ لَعِلْمٌ لِّلسَّاعَةِ فَلَا تَمْتَرُنَّ بِهَا وَاتَّبِعُونِ ۚ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ﴿٦١﴾
61. Na hakika yeye (Nabiy ‘Iysaa) ni alama ya Saa (Qiyaamah) basi usiitilie shaka na nifuateni. Hii ndio njia liyonyooka.


وَلَا يَصُدَّنَّكُمُ الشَّيْطَانُ ۖ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ﴿٦٢﴾
62. Na wala asikuzuieni shaytwaan, hakika yeye kwenu ni adui bayana.


وَلَمَّا جَاءَ عِيسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ قَالَ قَدْ جِئْتُكُم بِالْحِكْمَةِ وَلِأُبَيِّنَ لَكُم بَعْضَ الَّذِي تَخْتَلِفُونَ فِيهِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ﴿٦٣﴾
63. Na alipokuja ‘Iysaa kwa hoja bayana, akasema: “Nimekujieni kwa hikmah, na ili nikubainishieni baadhi ya yale mnayokhitilafiana nayo, basi mcheni Allaah na nitiini.


إِنَّ اللَّـهَ هُوَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ﴿٦٤﴾
64. “Hakika Allaah Ndiye Rabb (Mola) wangu na Rabb wenu, basi mwabuduni (Yeye Pekee), hii ndio njia liyonyooka.”


فَاخْتَلَفَ الْأَحْزَابُ مِن بَيْنِهِمْ ۖ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْ عَذَابِ يَوْمٍ أَلِيمٍ﴿٦٥﴾
65. Basi wakakhitilafiana makundi (wakagawanyika) baina yao. Basi ole kwa wale waliodhulumu kutokana na adhabu ya Siku iumizayo.


هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ﴿٦٦﴾
66. Je, wanangojea (nini) isipokuwa Saa (Qiyaamah) iwafikie ghafla nao hawatambui.


الْأَخِلَّاءُ يَوْمَئِذٍ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلَّا الْمُتَّقِينَ﴿٦٧﴾
67. Rafiki wapenzi Siku hiyo watakuwa maadui wao kwa wao isipokuwa wenye taqwa.


يَا عِبَادِ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ﴿٦٨﴾
68. (Ambao Allaah Atasema): “Enyi waja Wangu! Hakuna khofu juu yenu leo, na wala nyinyi hamtohuzunika.”


الَّذِينَ آمَنُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا مُسْلِمِينَ﴿٦٩﴾
69. “Ambao wameamini Aayaat Zetu na wakawa Waislamu.”


ادْخُلُوا الْجَنَّةَ أَنتُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ تُحْبَرُونَ﴿٧٠﴾
70. Ingieni Jannah nyinyi na wake zenu mfurahishwe.


يُطَافُ عَلَيْهِم بِصِحَافٍ مِّن ذَهَبٍ وَأَكْوَابٍ ۖ وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ الْأَنفُسُ وَتَلَذُّ الْأَعْيُنُ ۖ وَأَنتُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٧١﴾
71. Watapitishiwa sahani za dhahabu na bilauri, na humo mna yale yanayotamani nafsi na ya kuburidisha macho, nanyi humo ni wenye kudumu.


وَتِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٧٢﴾
72. Na hiyo ni Jannah ambayo mmerithishwa kwa yale mliyokuwa mkitenda.


لَكُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ كَثِيرَةٌ مِّنْهَا تَأْكُلُونَ﴿٧٣﴾
73. Mtapata humo matunda mengi (kila aina) baadhi yao mnakula.


إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي عَذَابِ جَهَنَّمَ خَالِدُونَ﴿٧٤﴾
74. Hakika wahalifu wamo kwenye adhabu ya (Moto wa) Jahannam ni wenye kudumu.


لَا يُفَتَّرُ عَنْهُمْ وَهُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ﴿٧٥﴾
75. Hawatopumzishwa nayo (adhabu ya Moto), nao humo watakata tamaa.


وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا هُمُ الظَّالِمِينَ﴿٧٦﴾
76. Na wala Hatukuwadhulumu lakini walikuwa wao wenyewe ndio madhalimu.


وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ ۖ قَالَ إِنَّكُم مَّاكِثُونَ﴿٧٧﴾
77. Na wataita: “Ee Maalik (Mlinzi wa Moto)! Na Atumalize (tufe) Rabb (Mola) wako.” Atasema: “Hakika nyinyi ni wenye kubakia (humo).


لَقَدْ جِئْنَاكُم بِالْحَقِّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَكُمْ لِلْحَقِّ كَارِهُونَ﴿٧٨﴾
78. “Kwa yakini Tulikujieni kwa haki, lakini wengi wenu kwa haki ni wenye kukirihika (nayo).”


أَمْ أَبْرَمُوا أَمْرًا فَإِنَّا مُبْرِمُونَ﴿٧٩﴾
79. Au wamepitisha jambo?  Basi hakika Sisi ni Wenye kupitisha (njama).


أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُم ۚ بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ﴿٨٠﴾
80. Au wanadhania kwamba Sisi Hatusikii siri zao na minong’ono yao? Sivyo! (Tunasikia!) Na Wajumbe wetu wako kwao wanaandika.


قُلْ إِن كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ﴿٨١﴾
81. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Kama ingelikuwa Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) Ana waladi (kama mnavyodai), basi mimi (ningekuwa) wa awali kumwabudu.”


سُبْحَانَ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبِّ الْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ﴿٨٢﴾
82. Utakasifu ni wa Rabb (Mola) wa mbingu na ardhi, Rabb wa ‘Arsh kutokana na yale wanayoyaelezea.


فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ﴿٨٣﴾
83. Basi waachilie mbali watumbukie katika porojo na wacheze mpaka wakutane na Siku yao ambayo wameahidiwa.


وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ﴿٨٤﴾
84. Na Yeye Ndiye Ilaah (Muabudiwa wa haki) mbinguni na ardhini (pia, Ndiye Huyo Huyo) Ilaah. Naye Ndiye Al-Hakiymul-‘Aliym (Mwenye hikmah wa yote - Mjuzi wa yote).


وَتَبَارَكَ الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَعِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٨٥﴾
85. Na Amebarikika Ambaye ufalme wa mbingu na ardhi ni Wake na vilivyo baina yake, na Kwake Pekee upo ujuzi wa Saa (Qiyaamah) na Kwake mtarejeshwa.


وَلَا يَمْلِكُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَن شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴿٨٦﴾
86. Na wala wale wanaowaomba badala Yake hawana (uwezo) wa kumiliki ash-shafaa’ah (uombezi wa aina yoyote ule) isipokuwa yule aliyeshuhudia kwa haki nao wanajua.


وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٨٧﴾
87. Na ukiwauliza: Ni nani kawaumba? Bila shaka watasema: “Allaah.”  Basi vipi wanaghilibiwa?


وَقِيلِهِ يَا رَبِّ إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ قَوْمٌ لَّا يُؤْمِنُونَ﴿٨٨﴾
88. Na (Allaah Anajua) kauli yake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Ee Rabb (Mola) wangu!  Hakika hawa watu hawaamini.”


فَاصْفَحْ عَنْهُمْ وَقُلْ سَلَامٌ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ﴿٨٩﴾
89. Basi wapuuzilie mbali (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na sema:  “Salaam” (amani). Na karibuni hivi watakuja jua.




Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com