An-Nabaa (78)

سُورَةُ  النَّبَاء
An-Nabaa (78)

(Imeteremka Makka)


Sura hii imethibitisha khabari ya kufufuliwa, na inawahadharisha hao wenye kutilia shaka jambo hilo. Na ikasimamisha hoja na dalili juu ya kuwezekana kwake kwa kuyaeleza yanayo onekana ya kudra ya Mwenyezi Mungu. Na ikatilia mkazo kuwepo kwake, na ikataja baadhi ya alama zake. Kisha ikataja khatima ya wenye kuasi, na khatima ya wachamngu. Na ikamalizikia kwa kuonya na kukhofisha kwa siku hiyo inayo tisha.
 
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

عَمَّ يَتَسَاءَلُونَ ﴿١﴾

1. Kuhusu nini wanaulizana?

عَنِ النَّبَإِ الْعَظِيمِ ﴿٢﴾

2. Kuhusu habari (iliyo) kuu mno.


الَّذِي هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ ﴿٣﴾

3. Ambayo wao wanakhitilafiana ndani yake.

كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ﴿٤﴾
4. Hasha! Hivi karibuni watajua.

ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ﴿٥﴾

5. Kisha hasha! Hivi karibuni watajua.

أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ مِهَادًا ﴿٦﴾

6. Je, kwani Hatukuijaalia ardhi kuwa tandiko?

وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا ﴿٧﴾

7. Na majabali kuwa (kama) vigingi (vya ardhi)?


وَخَلَقْنَاكُمْ أَزْوَاجًا ﴿٨﴾

8. Na Tukakuumbeni jozi (dume na jike).

وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا ﴿٩﴾

9. Na Tukajaalia usingizi wenu (kama) wa mapumziko (na raha).

وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا ﴿١٠﴾

10. Na Tukajaalia usiku kuwa (kama) libasi (mnayofunikwa).

وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا ﴿١١﴾

11. Na Tukajaalia mchana kuwa ni wa (kutafuta) maisha.

وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا ﴿١٢﴾

12. Na Tukajenga juu yenu (mbingu) saba imara.


وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا ﴿١٣﴾

13. Na Tukajaalia taa ing’arayo na yenye joto.

وَأَنزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاءً ثَجَّاجًا ﴿١٤﴾

14. Na Tukateremsha kutoka mawinguni maji yanayomwagika kwa kasi kubwa.

لِّنُخْرِجَ بِهِ حَبًّا وَنَبَاتًا ﴿١٥﴾

15. Ili Tutoe kwayo nafaka na mimea.

وَجَنَّاتٍ أَلْفَافًا ﴿١٦﴾

16. Na mabustani yanayosongomana.

إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ كَانَ مِيقَاتًا ﴿١٧﴾

17. Hakika siku ya Hukumu ni wakati maalumu.

يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا ﴿١٨﴾
18. Siku itakayopulizwa katika baragumu, mtakuja makundi makundi.


وَفُتِحَتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ أَبْوَابًا ﴿١٩﴾

19. Na mbingu zitafunguliwa, zitakuwa milango.

وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا ﴿٢٠﴾

20. Na majabali yataendeshwa, yatakuwa sarabi.

إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا ﴿٢١﴾

21. Hakika (Moto wa) Jahannam utakuwa wenye kuvizia.

لِّلطَّاغِينَ مَآبًا ﴿٢٢﴾

22. Kwa walioruka mipaka wakaasi ndio mahali (pao) pa kurejea.

لَّابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا ﴿٢٣﴾

23. Watabakia humo dahari.

لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا ﴿٢٤﴾

24. Hawatoonja humo (chochote cha) baridi na wala kinywaji.

إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا ﴿٢٥﴾

25. Isipokuwa maji yachemkayo na usaha.

جَزَاءً وِفَاقًا ﴿٢٦﴾

26. Jazaa inayowafikiana kabisa (na yale waliyoyatenda).

إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا ﴿٢٧﴾

27. Hakika wao walikuwa hawataraji hesabu.

وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا ﴿٢٨﴾

28. Na walikadhibisha Aayaat Zetu kukadhibisha kwa nguvu.

وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا ﴿٢٩﴾

29. Na kila kitu Tumekidhibiti kwa kuandika.

فَذُوقُوا فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا ﴿٣٠﴾

30. Basi onjeni (malipo yenu), kwani Hatutokuzidishieni (chochote) isipokuwa adhabu.

إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا ﴿٣١﴾

31. Hakika wenye taqwa watapata mafanikio.

حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا ﴿٣٢﴾

32. Mabustani na mizabibu (Peponi).

وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا ﴿٣٣﴾

33. Na wanawake wenye vifua vya kujaa wa hirimu (na waume zao).

وَكَأْسًا دِهَاقًا ﴿٣٤﴾

34. Na kikombe kilojaa (pomo).

لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا ﴿٣٥﴾

35. Hawatosikia humo (ya) upuuzi na wala (ya) kukadhibisha.

جَزَاءً مِّن رَّبِّكَ عَطَاءً حِسَابًا ﴿٣٦﴾

36. Jazaa kutoka kwa Rabb (Mola) wako tunukio la kutosheleza.

رَّبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الرَّحْمَـٰنِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا ﴿٣٧﴾

37. Rabb (Mola) wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah), hawatomiliki kutoka Kwake (idhini) ya kumsemesha.

يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّا ۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَـٰنُ وَقَالَ صَوَابًا ﴿٣٨﴾

38. Siku atakayosimama Ruwh (Jibriyl) na Malaika safusafu; hawatozungumza isipokuwa yule ambaye Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) Amempa idhini (ya kuzungumza), na (hapo) atasema yaliyo sahihi.

ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الْحَقُّ ۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ مَآبًا ﴿٣٩﴾

39. Hiyo ni Siku ya haki; basi atakaye achukue (njia ya) marudio kwa Rabb (Mola) wake.

إِنَّا أَنذَرْنَاكُمْ عَذَابًا قَرِيبًا يَوْمَ يَنظُرُ الْمَرْءُ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ وَيَقُولُ الْكَافِرُ يَا لَيْتَنِي كُنتُ تُرَابًا ﴿٤٠﴾

40. Hakika Sisi Tumekuonyeni adhabu (iliyo) karibu, Siku mtu atakapotazama yale iliyokadimisha mikono yake; na kafiri (siku hiyo) atasema: “Laiti ningelikuwa mchanga.”



Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com