Hadithi Ya 07: Dini Ni Nasiha
الحديث السابع
"الدين النصيحة"
عن
أبي رُقَيَّةَ تَمِيمِ بنِ أوْسٍ الدَّارِيِّ رضي اللهُ عنه: أَنَّ
النَّبي صلى الله عليه وسلم قالَ:((الدِّينُ النَّصِيحَةُ)). قُلْنَا:
لِمَنْ ؟ قالَ: ((للهِ، ولِكِتَابِهِ، ولِرَسُولِهِ، ولِلأَئِمةِ
المُسْلِمِينَ، وعامَّتِهِمْ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 7
DINI NI NASIHA
Kutoka kwa Abu Ruqayyah Tamim Ibn Aus Addarryرضي الله عنه ambaye amesema kuwa Bwana Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Dini
ni nasiha. Tukauliza: Kwa nani? Akasema kwa Allaah (Kukiri Uungu
wake na kwamba Hana mshirika), Kitabu chake (Kukubali kuwa ni maneno ya
Allah yasiyo na shaka), na Mtume wake (Kumkubali na kukubali ujumbe
aliotumwa nao), na kwa Viongozi wa Waislamu (Kuwatii na kuwafuata katika
mema na kuwaasa katika yale wanayokwenda nayo kinyume), na watu wa
kawaida (kuusiana mema na kukatazana mabaya kwa njia nzuri).
Imesimuliwa na Muslim