Al-‘Alaq (96)


سُورَةُ  الْعَلَق
Al-‘Alaq (96) 

(Imeteremka Makka)


Katika Sura hii upo wito wa kusoma na kujifunza, na kwamba aliye weza kumuumba mtu kutokana na asli nyonge ni Mweza wa kumfunza kuandika kwa kudhibitia ilimu na kutimizia kufahamu, na amfunze aliyo kuwa hayajui. Kwani Yeye Subhanahu ndiye Mwenye kummiminia ilimu mwanaadamu. Na Sura  inanabihisha kwamba utajiri na nguvu huenda zikampelekea mtu kupindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu, lakini marejeo ya wote ni kwa Mwenyezi Mungu mwishoni. Na mazungumzo yanamwelekea kila mwenye kusilihi kusemezwa kuwaonya hao majeuri wanao pinga kheri, kuwaonya kuwa watakuja kushikwa kwa nywele zao za utosi wakibururwa Motoni; na hawatofaliwa na wasaidizi wowote. Na Sura inakhitimisha kwa kuwataka wasikivu wende kinyume na hao wenye inda wanao kadhibisha, na wajijongeze kwa ut'iifu kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾

1. Soma kwa Jina la Rabb (Mola) wako Aliyeumba.

خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾

2. Amemuumba insani kutokana na pande la damu linaloning’inia.

اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾

3. Soma na Rabb (Mola) wako ni Al-Akram (Mkarimu kabisa).

الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾

4. Ambaye Aliyefunza kwa kalamu.

عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾

5. Amemfunza insani yale asiyoyajua.

كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾

6. Hapana! Hakika insani bila shaka amepindukia mipaka (kuasi).

أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾

7. Anapojiona amejitosheleza.

إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ ﴿٨﴾

8. Hakika kwa Rabb (Mola) wako ni marejeo.

أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ ﴿٩﴾

9. Je, umemuona yule anayekataza?

عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ ﴿١٠﴾

10. Mja (pale) anaposwali?

أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ ﴿١١﴾

11. Je, umeona kama (yeye) yumo katika uongofu?

أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ ﴿١٢﴾

12. Au ameamrisha taqwa?

أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٣﴾

13. Je, umeona kama amekadhibisha na akakengeuka?

أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرَىٰ ﴿١٤﴾

14. Je, hajui kwamba Allaah Anaona?

كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ ﴿١٥﴾

15. Hapana! Asipoacha, bila shaka Tutamkokota kwa kishungi (shore juu ya paji la uso).

نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ ﴿١٦﴾

16. Kishungi (shore juu ya paji la uso) kinachokadhibisha chenye makosa.


فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ ﴿١٧﴾

17. Basi na aite washirika wenziwe (wasaidizi).

سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ ﴿١٨﴾
18. Nasi Tutawaita Az-Zabaaniyyah (walinzi wa Moto).

كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب ۩ ﴿١٩﴾

19. Hapana! Usimtii; na sujudu na kurubia (kwa Rabb wako).





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com