Al-Insaan (76)


سُورَةُ  الإِنْسَان
Al-Insaan  (76)
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

هَلْ أَتَىٰ عَلَى الْإِنسَانِ حِينٌ مِّنَ الدَّهْرِ لَمْ يَكُن شَيْئًا مَّذْكُورًا ﴿١﴾

1. Je, haukumpitia insani wakati katika dahari, hakuwa kitu kinachotajwa?

إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا بَصِيرًا ﴿٢﴾

2. Hakika Sisi Tumemuumba insani kutokana na tone la manii iliyochanganyika ili Tumjaribu; Tukamjaalia mwenye kusikia na kuona.

إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا ﴿٣﴾

3. Hakika Sisi Tumemuongoza njia; (basi) ima (awe) mwenye kushukuru au (awe) mwenye kukufuru.

إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَلَاسِلَ وَأَغْلَالًا وَسَعِيرًا ﴿٤﴾

4. Hakika Sisi Tumewaandalia makafiri minyororo, na pingu na (Moto wa) Sa’iyraa (uwakao kwa nguvu).”

إِنَّ الْأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِن كَأْسٍ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا ﴿٥﴾

5. Hakika Al-Abraar (watu wema) watakunywa katika gilasi (kinywaji cha) mchanganyiko wa kafuri.

عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ اللَّـهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرًا ﴿٦﴾

6. Chemchemu watakayokunywa humo waja wa Allaah, watabubujua mbubujiko.

يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا ﴿٧﴾

7. (Ambao) Wanatimiza nadhiri (zao), na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea.

وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا ﴿٨﴾

8. Na wanalisha chakula juu ya mapenzi yao (kwa hicho wanacholisha) masikini na mayatima na mateka.

إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّـهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا ﴿٩﴾

9. “Hakika sisi tunakulisheni kwa (ajili ya) Wajihi wa Allaah, hatutaki kwenu jazaa na wala shukurani.

إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِيرًا ﴿١٠﴾

10. “Hakika sisi tunakhofu kwa Rabb (Mola) wetu siku inayokunjisha uso ngumu nzito.

فَوَقَاهُمُ اللَّـهُ شَرَّ ذَٰلِكَ الْيَوْمِ وَلَقَّاهُمْ نَضْرَةً وَسُرُورًا ﴿١١﴾

11.  Basi Allaah Atawakinga na shari ya siku hiyo, na Atawakutanisha na mng’ao na furaha.

وَجَزَاهُم بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا ﴿١٢﴾

12. Na Atawalipa Jannah na (nguo za) hariri kwa kusubiri kwao.

مُّتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ ۖ لَا يَرَوْنَ فِيهَا شَمْسًا وَلَا زَمْهَرِيرًا ﴿١٣﴾

13. Wataegemea humo juu ya makochi (ya fakhari), hawatoona humo joto la jua wala baridi kali.

وَدَانِيَةً عَلَيْهِمْ ظِلَالُهَا وَذُلِّلَتْ قُطُوفُهَا تَذْلِيلًا ﴿١٤﴾

14. Na vivuli (vyake) vitakuwa karibu yao, na kuchumwa kwake (matunda) yamening’inizwa (wayafikie).

 وَيُطَافُ عَلَيْهِم بِآنِيَةٍ مِّن فِضَّةٍ وَأَكْوَابٍ كَانَتْ قَوَارِيرَا ﴿١٥﴾

15. Na watazungushiwa vyombo vya fedha, na vikombe vilivyokuwa vya vigae.

قَوَارِيرَ مِن فِضَّةٍ قَدَّرُوهَا تَقْدِيرًا ﴿١٦﴾
16. Vikombe vya vigae vya fedha wamevipima kwa kipimo.

وَيُسْقَوْنَ فِيهَا كَأْسًا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا ﴿١٧﴾

17. Na watanyweshwa humo gilasi (kinywaji) mchanganyiko wake wa tangawizi.

عَيْنًا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلْسَبِيلًا ﴿١٨﴾

18. Chemchemu inayoitwa Salsabiylaa.

وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ لُؤْلُؤًا مَّنثُورًا ﴿١٩﴾

19. Na watawazungukia wavulana wa kudumu (kuwatumikia), utakapowaona, utawadhania ni lulu zilizotawanywa.

وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيمًا وَمُلْكًا كَبِيرًا ﴿٢٠﴾

20. Na utakapoyaona (hayo yaliyoko), utaona neema (zisizo kifani) na ufalme mkubwa.

عَالِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْرٌ وَإِسْتَبْرَقٌ ۖ وَحُلُّوا أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٍ وَسَقَاهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًا طَهُورًا ﴿٢١﴾

21. Juu yao wana nguo nzuri za hariri laini za kijani (kibichi) na za hariri nzito, na watapambwa bangili (vikuku) vya fedha; na Rabb (Mola) wao Atawanywesha kinywaji safi kabisa.

إِنَّ هَـٰذَا كَانَ لَكُمْ جَزَاءً وَكَانَ سَعْيُكُم مَّشْكُورًا ﴿٢٢﴾

22. (Waatambiwa): “Hakika haya ni jazaa yenu, kwani juhudi zenu (za kutenda amali duniani) zimethaminiwa.”

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ تَنزِيلًا ﴿٢٣﴾

23. Hakika Sisi Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Qur-aan uteremsho wa hatua kwa hatua.

فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعْ مِنْهُمْ آثِمًا أَوْ كَفُورًا ﴿٢٤﴾

24. Basi subiri hukumu ya Rabb (Mola) wako, na wala usimtii miongoni mwao atendaye dhambi au mwenye kukufuru.

وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا ﴿٢٥﴾

25. Na lidhukuru Jina la Rabb (Mola) wako asubuhi na jioni.

وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا ﴿٢٦﴾

26. Na katika usiku, msujudie na msabbih usiku (muda) mrefu.

إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ يُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَاءَهُمْ يَوْمًا ثَقِيلًا ﴿٢٧﴾

27. Hakika hawa (makafiri) wanapenda (uhai wa dunia) unaopita haraka kwa muda tu, na wanaacha nyuma yao siku nzito (ya Qiyamaah).

نَّحْنُ خَلَقْنَاهُمْ وَشَدَدْنَا أَسْرَهُمْ ۖ وَإِذَا شِئْنَا بَدَّلْنَا أَمْثَالَهُمْ تَبْدِيلًا ﴿٢٨﴾

28. Sisi Tumewaumba, na Tumetia nguvu viungo vyao; na kama Tukitaka, Tutawabadilisha kama wao mbadiliko (kamilifu).

إِنَّ هَـٰذِهِ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا ﴿٢٩﴾

29. Hakika hii ni tadhkirah (ukumbusho), basi anayetaka achukue njia ya (kuelea kwa) Rabb (Mola) wake.

وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٣٠﴾

30. Na (hamtoweza) kutaka (chochote kile mkitakacho) isipokuwa Atake Allaah; hakika Allaah daima ni ‘Aliyman-Hakiymaa (Mjuzi wa yote - Mwenye hikimah wa yote).

يُدْخِلُ مَن يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ ۚ وَالظَّالِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿٣١﴾

31. Anamuingiza Amtakaye katika Rahmah Yake, na madhalimu Amewaandalia adhabu iumizayo.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com