Hadithi Ya 24: Enyi Waja Wangu Nimeikataza Nafsi Yangu Dhulma


الحديث الرابع والعشرون

"يا عبادي إني حرمت الظلم على نفسي"

 

عن أبي ذَرٍّ الْغِفاريِّ رضي الله عنه، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم فيما يَرْويهِ عن رَبِّهِ عَزَّ وجَلَّ أَنَّهُ قال: 
(( يا عِبادي إنِّي حَرَّمْتُ الظُلْمَ على نَفْسِي وَ جعَلْتُهُ بَيْنَكُمْ مُحَرَّماً فلا تَظَالَمُوا.
يا عِبادي كُلُّكُمْ ضالٌّ إلا مَنْ هَدَيْتُهُ، فاسْتَهدُوني أهْدِكُمْ.
يا عِبادِي كُلُّكُمْ جائعٌ إلا مَنْ أطْعَمْتُهُ، فاسْتَطْعِمُوني أُطْعِمْكُم.
يا عِبادِي كُلُّكُمْ عَارٍ إلا مَنْ كَسَوْتُهُ، فاسْتكْسوني أَكسُكُم.
يا عِبادِي إِنَّكُمْ تُخْطِئُونَ بالليْلِ والنَّهارِ، وأنا أَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَميعاً، فاسْتَغْفِرُوني أُغْفِر لكُمْ.
يا عِبادِي إِنَّكُمْ لنْ تبْلغُوا ضُرِّي فتَضُرُّوني، ولن تبْلُغُوا نفْعي فَتَنْفعُوني.
يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجِنَّكُمْ كانُوا عَلَى أَتْقَى قَلْبِ رَجُلٍ واحدٍ مِنْكُمْ ما زادَ ذلك في مُلْكي شَيئاً.
يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجِنَّكُمْ كانُوا عَلَى أَفْجَرِ قَلْبِ رَجُلٍ وَاحدٍ مِنْكُمْ ما نَقَصَ ذَلِكَ مِنْ مُلْكي شَيئاً.
يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجنَّكُمْ قاموا في صَعِيدٍ وَاحِدٍ، فَسَأَلُوني، فأَعْطَيْتُ كلَّ واحدٍ مَسْأَلَتَهُ ما نَقَصَ ذلك مِمَّا عِنْدِي إلا كما يَنْقُصُ الْمِخْيَطُ إذا أُدْخِلَ الْبَحْرَ.
يا عِبادِي إنَّما هي أعمَالُكُمْ أُحْصِيها لَكُمْ ثُمَّ أُوَفِّيكُمْ إيَّاها، فَمَنْ وَجَدَ خيْراً فَلْيَحْمَدِ اللهَ، ومَنْ وَجَدَ غَيْرَ ذلك فَلا يَلومَنَّ إلا نَفْسَه))
 رَوَاهُ مُسْلِمٌ   
HADITHI YA 24
ENYI WAJA WANGU NIMEIKATAZA NAFSI YANGU DHULMA

Kutoka kwa Abu Dharr Al-Ghifariy رضي الله عنه   naye kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم  akisimulia yale aliyopokea kutoka kwa  Bwana wake   عَزَّ وَجَلَّ   ni:
Enyi waja Wangu, Nimeikataza nafsi Yangu dhulma na Nimeiharamisha kwenu (hiyo dhulma), kwa hivyo msidhulumiane.
Enyi waja Wangu, nyote mumepotea isipokuwa wale Niliowaongoza, kwa hivyo tafuteni muongozo kutoka Kwangu Nitakuongozeni. 
Enyi waja Wangu nyote mna njaa isipokuwa wale Niliowalisha, kwa hivyo tafuteni chakula kutoka Kwangu na Nitakulisheni.
Enyi waja Wangu, nyote muko uchi isipokuwa wale niliowavika nguo, kwa hivyo tafuteni vazi kutoka Kwangu nitakuvisheni.
Enyi waja Wangu, mnafanya  makosa usiku na mchana, na ninasamehe dhambi zote, kwa hivyo tafuteni msamaha kutoka Kwangu nitakusameheni.
Enyi waja Wangu hamuwezi kunidhuru Mimi wala kuninufaisha.  
Enyi waja Wangu, ingekuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mcha Mungu kama moyo wa mcha Mungu yeyote katika nyinyi, haitaongeza  chochote katika ufalme Wangu.
Enyi waja Wangu, angelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mbaya kama moyo mbaya wa mtu miongoni mwenu (mtu mbaya kupita kiasi) haitonipunguzia chochote katika ufalme Wangu.
Enyi  waja Wangu ingelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi mukasimama pahala pamoja na mkaniomba, na nikawapa kila mmoja alichoomba, haitonipunguzia katika nilicho nacho zaidi kuliko sindano inavyopunguza bahari inapochovya.
Enyi waja Wangu, ni vitendo vyenu ninavyovihesabu, kwa ajili yenu nikakulipeni.  Kwa hivyo anayekuta wema amshukuru Allaah na yule anayekuta yasiokuwa mema (basi) ajilaumu mwenyewe.
Imesimuliwa na Muslim