Al-Ma’aarij (70)

سُورَةُ  الْمَعَارِج
Al-Ma’aarij (70)

(Imeteremka Makka)




Katika Sura hii tukufu kipo kitisho kwa Siku ya Kiyama, na kutia khofu kwa urefu wake, na vitisho vikubwa vikubwa, na adhabu ambazo hazikubaliwi kutolewa fidia hata ya wana, wala mke, wala ndugu, wala ukoo mzima. Bali haikubaliwi fidia ya watu wa dunia nzima.
Na katika Sura hii unatolewa kombo udhaifu wa binaadamu wakati wa shida na neema, isipo kuwa aliye okolewa na Mwenyezi Mungu kwa uchamngu, na vitendo vyema. Hao wanasalimika na udhaifu huo.
Humo vile vile yanaelezwa kuchukiza tabia ya makafiri ya kuwa na tamaa ya uharibifu. Na mwishoni anausiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. awawachilie mbali na upumbavu wao na mchezo wao mpaka wakutane na siku yao waliyo ahidiwa.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ ﴿١﴾
1. Muulizaji ameuliza kuhusu adhabu itakayotokea.

لِّلْكَافِرِينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ ﴿٢﴾

2. Kwa makafiri, (adhabu) ambayo hakuna wa kuikinga.

مِّنَ اللَّـهِ ذِي الْمَعَارِجِ ﴿٣﴾

3. Kutoka kwa Allaah Mwenye kumiliki njia za kupandia.

تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ ﴿٤﴾

4. Malaika na Roho (Jibrily) wanapanda Kwake katika siku kiasi chake ni miaka khamsini elfu.

فَاصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا ﴿٥﴾

5. Basi subiri, subira njema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُ بَعِيدًا ﴿٦﴾

6. Hakika wao wanakiona (Qiyaamah) kiko mbali.

وَنَرَاهُ قَرِيبًا ﴿٧﴾

7. Nasi Tunakiona (kiko) karibu.

يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاءُ كَالْمُهْلِ ﴿٨﴾

8. Siku mbingu zitapokuwa kama shaba iliyoyeyushwa (mafuta yachemkayo).

وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ ﴿٩﴾

9. Na majabali yatakuwa kama sufi.

وَلَا يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا ﴿١٠﴾

10.  Na wala rafiki wa dhati hatomuuliza rafiki yake wa dhati.

يُبَصَّرُونَهُمْ ۚ يَوَدُّ الْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِي مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍ بِبَنِيهِ ﴿١١﴾

11. Watafanywa waonane, (lakini) mhalifu atatamani ajikomboe na adhabu siku hiyo kwa (kuwatoa) watoto wake.

وَصَاحِبَتِهِ وَأَخِيهِ ﴿١٢﴾

12. Na mkewe na nduguye.

وَفَصِيلَتِهِ الَّتِي تُؤْوِيهِ ﴿١٣﴾

13. Na jamaa zake wa karibu ambao (waliokuwa) wakimpa makazi.

وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنجِيهِ ﴿١٤﴾

14. Na wale wote waliomo ardhini, kisha aokoke (yeye).

كَلَّا ۖ إِنَّهَا لَظَىٰ ﴿١٥﴾

15. Hasha! Hakika huo ni mwako wa Moto uwakao barabara.

نَزَّاعَةً لِّلشَّوَىٰ ﴿١٦﴾

16. Unararua (unababua na kuunguza kikamilifu) ngozi ya kichwa.


تَدْعُو مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٧﴾

17. (Moto huo) Utamwita yule aliyegeuza mgongo (kuipa mgongo haki) na akageuka (kuasi na kupuuza Qur-aan).

وَجَمَعَ فَأَوْعَىٰ ﴿١٨﴾

18. Na akakusanya (mali), kisha akayarundika.

إِنَّ الْإِنسَانَ خُلِقَ هَلُوعًا ﴿١٩﴾

19. Hakika insani ameumbwa ni mwenye pupa.

إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعًا ﴿٢٠﴾

20. (Pale) Inapomgusa shari, anapapatika (anakuwa na wahka).

وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعًا ﴿٢١﴾

21. Na (pale) inapomgusa kheri, huizuilia.

إِلَّا الْمُصَلِّينَ ﴿٢٢﴾

22. Isipokuwa wanaoswali.

الَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ دَائِمُونَ ﴿٢٣﴾

23. Ambao wenye kudumisha Swalaah zao.

وَالَّذِينَ فِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ مَّعْلُومٌ ﴿٢٤﴾

24. Na wale ambao katika mali zao (huweka) haki (sehemu) maalumu.

لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ ﴿٢٥﴾

25. Kwa ajili ya muombaji na aliyenyimwa (aliyepoteza makazi na mali yake akadhikika).

وَالَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ ﴿٢٦﴾

26. Na ambao wanasadikisha Siku ya Malipo.

وَالَّذِينَ هُم مِّنْ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ ﴿٢٧﴾

27. Na wale ambao kutokana na adhabu ya Rabb (Mola) wao wanaogopa.

إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ ﴿٢٨﴾
28. Hakika adhabu ya Rabb (Mola) wao si ya kusalimika nayo (mtu, isipokuwa yule atakayesalimishwa nayo).

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ ﴿٢٩﴾

29. Na ambao wanahifadhi tupu zao.

إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ ﴿٣٠﴾

30. Isipokuwa kwa wake zao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi.

فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ ﴿٣١﴾

31. Basi yeyote yule atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio warukao mipaka.

وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ ﴿٣٢﴾

32. Na ambao amana zao na ahadi zao wanazichunga (kuzitimiza).

وَالَّذِينَ هُم بِشَهَادَاتِهِمْ قَائِمُونَ ﴿٣٣﴾

33. Na ambao wanasimamisha (imara) ushahidi wao.

 وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿٣٤﴾

34. Na ambao wanahifadhi Swalaah zao.

أُولَـٰئِكَ فِي جَنَّاتٍ مُّكْرَمُونَ ﴿٣٥﴾

35. Hao watakuwa kwenye Jannah wakikirimiwa.

فَمَالِ الَّذِينَ كَفَرُوا قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ ﴿٣٦﴾

36. Basi wana nini waliokufuru wanaharakiza mbele yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)?

عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ عِزِينَ ﴿٣٧﴾

37. (Kukukalia) Kuliani na kushotoni katika makundi!

أَيَطْمَعُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ ﴿٣٨﴾

38. Je, anatumai kila mtu miongoni mwao kwamba ataingizwa Jannah ya Na’iym?

كَلَّا ۖ إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّمَّا يَعْلَمُونَ ﴿٣٩﴾

39. Hapana!  Hakika Sisi Tumewaumba kutokana na kile wanachokijua.

فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ إِنَّا لَقَادِرُونَ ﴿٤٠﴾

40. Basi Naapa kwa Rabb (Mola) wa Mashariki na Magharibi, hakika Sisi bila shaka ni Wenye kuweza.

عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ ﴿٤١﴾

41. Kwamba Tuwabadilishe walio bora kuliko kwao, Nasi Hatushindwi.

فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ ﴿٤٢﴾

42. Basi waachilie mbali watumbukie katika porojo (na upuuzi) na wacheze, mpaka wakutane na siku yao ile wanayoahidiwa.

يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَىٰ نُصُبٍ يُوفِضُونَ ﴿٤٣﴾

43. Siku watapotoka makaburini haraka haraka kama kwamba wanakimbilia mfunda.

خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۚ ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ ﴿٤٤﴾

44. Macho yao yatanyenyekea (kwa khofu), udhalilifu utawafunika. Hiyo ndio ile siku waliyokuwa wakiahidiwa.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com