Hadiyth Ya 22 - Fadhila Za Kutembelea Mgonjwa Na Kumlisha Na Kunywesha Mtu

  

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ يَقُولُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ: يَا ابْنَ آدَمَ مَرِضْتُ فَلَمْ تَعُدْنِي. قَالَ يَا رَبِّ كَيْفَ أَعُودُكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ . قَالَ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّ عَبْدِي فُلَانًا مَرِضَ فَلَمْ تَعُدْهُ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّكَ لَوْ عُدْتَهُ لَوَجَدْتَنِي عِنْدَهُ .يَا ابْنَ آدَمَ اسْتَطْعَمْتُكَ فَلَمْ تُطْعِمْنِي . قَالَ يَا رَبِّ وَكَيْفَ أُطْعِمُكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ . قَالَ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّهُ اسْتَطْعَمَكَ عَبْدِي فُلَانٌ فَلَمْ تُطْعِمْهُ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّكَ لَوْ أَطْعَمْتَهُ لَوَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي . يَا ابْنَ آدَمَ اسْتَسْقَيْتُكَ فَلَمْ تَسْقِنِي . قَالَ يَا رَبِّ كَيْفَ أَسْقِيكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ. قَالَ اسْتَسْقَاكَ عَبْدِي فُلَانٌ فَلَمْ تَسْقِهِ أَمَا إِنَّكَ لَوْ سَقَيْتَهُ وَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي)) مسلم


Kutoka Kwa Abu Hurayrahرضي الله عنه   ambaye alisema kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: ((Allaah عَزَّ وَجَلَّ Atasema siku ya kufufuliwa: Ewe Mwana wa Aadam, Niliumwa na usije kunitazama. Atasema: Ewe Mola, vipi nije kukutazama nawe ni Mola wa ulimwengu wote? Atasema: Ulijua kuwa mja wangu fulani alikuwa mgonjwa na hukwenda kumtazama? Ulijua kuwa ungekwenda ungalinikuta Niko pamoja naye? Ewe mwana wa Aadam, Nilikuomba chakula na hukunipa. Atasema: Ewe Mola, vipi nitakupa chakula na Wewe ni Mola wa ulimwengu wote? Atasema hukujua kuwa mja wangu fulani alikuomba chakula na hukumpa? Hukujua kuwa ungalimpa chakula ungalikuta hayo (jazaa) kwangu mimi? Ewe mwana wa Aadam, nilikuomba maji na hukunipa. Ewe Mola, vipi nitakupa maji na Wewe ni Mola wa ulimwengu wote? Atasema hukujua kuwa mja wangu fulani alikuomba maji na hukumpa? Ungalimpa maji ungalikuta hayo (jazaa) Kwangu Mimi)) [Muslim]