Al-Muzzammil (73)

سُورَةُ  الْمُزَّمِّل
Al-Muzzammil (73)
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ ﴿١﴾

1. Ee uliyejifunika.

قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٢﴾

2. Simama (kuswali) usiku kucha isipokuwa (muda) mdogo tu.


نِّصْفَهُ أَوِ انقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا ﴿٣﴾
3. Nusu yake, au ipunguze kidogo.

أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا ﴿٤﴾

4. Au izidishe, na soma Qur-aan kwa Tartiylaa (kisomo cha utaratibu upasao).  

إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا ﴿٥﴾

5. Hakika Sisi Tutaweka juu yako kauli nzito.

إِنَّ نَاشِئَةَ اللَّيْلِ هِيَ أَشَدُّ وَطْئًا وَأَقْوَمُ قِيلًا ﴿٦﴾

6. Hakika kuamka usiku (kuswali) kunaathiri zaidi (katika) kuwafikiana (baina ya moyo na ulimi) na kunafaa zaidi kwa maneno (kutua na kufahamika).


إِنَّ لَكَ فِي النَّهَارِ سَبْحًا طَوِيلًا ﴿٧﴾

7. Hakika una mchana mrefu kwa shughuli nyingi.

وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلْ إِلَيْهِ تَبْتِيلًا ﴿٨﴾

8. Na dhukuru Jina la Rabb (Mola) wako, na jitolee Kwake kwa kujitolea (kikamilifu).

رَّبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَاتَّخِذْهُ وَكِيلًا ﴿٩﴾

9. Rabb (Mola) wa Mashariki na Magharibi, hakuna ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye. Basi mfanye (kuwa) Wakiylaa (Mtegemewa kwa yote).

وَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَاهْجُرْهُمْ هَجْرًا جَمِيلًا ﴿١٠﴾

10. Na subiri juu ya yale wayasemayo, na wahame, mhamo mzuri.

وَذَرْنِي وَالْمُكَذِّبِينَ أُولِي النَّعْمَةِ وَمَهِّلْهُمْ قَلِيلًا ﴿١١﴾

11. Na Niache Mimi na wanaokadhibisha walioneemeka; na uwape muhula kidogo.

إِنَّ لَدَيْنَا أَنكَالًا وَجَحِيمًا ﴿١٢﴾

12. Hakika Sisi Tuna minyororo na (Moto wa) Jahiymaah (uwakao kwa ghadhabu).

وَطَعَامًا ذَا غُصَّةٍ وَعَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٣﴾

13. Na chakula cha kukwama kooni, na adhabu iumizayo.

يَوْمَ تَرْجُفُ الْأَرْضُ وَالْجِبَالُ وَكَانَتِ الْجِبَالُ كَثِيبًا مَّهِيلًا ﴿١٤﴾

14. Siku itakayotikisika ardhi na majabali, na majabali yatakuwa kama chungu ya mchanga unaporomoka.

إِنَّا أَرْسَلْنَا إِلَيْكُمْ رَسُولًا شَاهِدًا عَلَيْكُمْ كَمَا أَرْسَلْنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ رَسُولًا ﴿١٥﴾

15. Hakika Sisi Tumekutumieni Rasuli (awe) shahidi juu yenu, kama Tulivyotuma kwa Fir’awn Rasuli.

فَعَصَىٰ فِرْعَوْنُ الرَّسُولَ فَأَخَذْنَاهُ أَخْذًا وَبِيلًا ﴿١٦﴾

16. (Lakini) Fir’awn alimuasi (huyo) Rasuli, Tukamchukuwa mchukuo wa kuangamiza.

فَكَيْفَ تَتَّقُونَ إِن كَفَرْتُمْ يَوْمًا يَجْعَلُ الْوِلْدَانَ شِيبًا ﴿١٧﴾

17. Basi vipi mtaweza kujikinga, kama mkikufuru (na adhabu ya) Siku itakayowafanya watoto kuwa wenye kutoka mvi?

السَّمَاءُ مُنفَطِرٌ بِهِ ۚ كَانَ وَعْدُهُ مَفْعُولًا ﴿١٨﴾

18. Mbingu zitapasuka hapo, Ahadi Yake itatimizwa.

إِنَّ هَـٰذِهِ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا ﴿١٩﴾

19. Hakika hii ni tadhkirah (ukumbusho), basi atakaye ashike njia ya kuelekea kwa Rabb (Mola) wake.

إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدْنَىٰ مِن ثُلُثَيِ اللَّيْلِ وَنِصْفَهُ وَثُلُثَهُ وَطَائِفَةٌ مِّنَ الَّذِينَ مَعَكَ ۚ وَاللَّـهُ يُقَدِّرُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ ۚ عَلِمَ أَن لَّن تُحْصُوهُ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۖ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ ۚ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرْضَىٰ ۙ وَآخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِي الْأَرْضِ يَبْتَغُونَ مِن فَضْلِ اللَّـهِ ۙ وَآخَرُونَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنْهُ ۚ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَقْرِضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا ۚ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٠﴾

20. Hakika Rabb (Mola) wako Anajua kwamba unasimama (kuswali) karibu (na) thuluthi mbili za usiku na (wakati mwengine) nusu yake, na (wakati mwengine) thuluthi yake; na kundi miongoni mwa wale walio pamoja nawe (pia linasimama kuswali). Na Allaah Anakadiria (urefu wa) usiku na mchana. Anajua kwamba hamuwezi kufanya hivyo (kuswali usiku wote), basi Amepokea tawbah yenu. Basi someni kile kilicho chepesi katika Qur-aan. (Allaah) Anajua kwamba watakuweko miongoni mwenu wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wanatafuta fadhila za Allaah, na wengineo wanapigana katika njia ya Allaah. Basi someni kile kilicho chepesi humo. Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na mkopesheni Allaah karadhi nzuri. Na chochote kile cha kheri mnachokadimisha kwa ajili ya nafsi zenu, (basi) mtakikuta kwa Allaah. Ni bora, na ujira mkubwa zaidi. Na muombeni Allaah maghfirah, hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com