Hadiyth Ya 33 Mja Mwenye Kusubiri Anapoondokewa Na kipenzi Chake Hulipwa Pepo



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى مَا لِعَبْدِي الْمُؤْمِنِ عِنْدِي جَزَاءٌ إِذَا قَبَضْتُ صَفِيَّهُ مِنْ أَهْلِ الدُّنْيَا ثُمَّ احْتَسَبَهُ إِلَّا الْجَنَّةُ)) البخاري


Kutoka kwa Abu Hurayrahرضي الله عنه  ambaye amesema: kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: ((Allaah Aliyetukuka Anasema: Haitokuwa jazaa ya mja wangu Muumini Ninapomchukulia kipenzi chake bora katika wakazi wa duniani kisha akastahamili kwa ajili Yangu, haitakua ila ni Pepo)) [Al-Bukhaariy]