Hadithi Ya 10: Allaah سبحانه وتعالى Ni Mwema Anakubali Kilicho Chema Tu

الحديث العاشر
"إن الله طيب لا يقبل إلا طيبا"

 عن أبي هُرَيْرَةَ رَضي اللهُ عنه قال: قاَل رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((إنَ الله تعالى طَيِّبٌ لا يَقْبَلُ إلا طَيِّباً، وإنَّ الله أَمَرَ المُؤمِنينَ بِمَا أَمَرَ بِهِ المُرْسَلينَ فقال تعالى: {يا أَيُّها الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيَّباتِ واعمَلُوا صالحاً} [المؤمنون: 51] وقال تعالى: {يا أَيُّها الَّذِينَ آمَنُوا كلُوا مِنْ طَيِّباتِ ما رَزَقْناكُمْ} [البقرة: 172] ثُمَّ ذَكَرَ الرَّجُلَ يُطِيلُ السَّفَرَ أشْعَثَ أَغْبَرَ يَمُدُّ يَدَيْهِ إلى السَّماءِ يا رَبُّ يا رَبُّ، ومَطْعَمُهُ حَرَامٌ، ومَشْربُهُ حَرَامٌ، وَمَلْبَسُهُ حَرَامٌ وغُذِّيَ بالحَرَامِ، فأَنَّى يُسْتَجَابُ لهُ!)).  

رَوَاهُ مُسْلِمٌ    
HADITHI YA10
ALLAAH سبحانه وتعالى  NI MWEMA ANAKUBALI KILICHO CHEMA TU.
Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه  ambaye alisema:  Mtume صلى الله عليه وسلم  kasema:
Allaah سبحانه وتعالى ni Mwema na anakubali kilicho chema tu. 
Allaah سبحانه وتعالى ameamrisha Waislamu kufanya yale aliyowaamrisha Mitume, na Yeye   سبحانه وتعالى kasema "Enyi Mitume Kuleni katika vitu vyema na mfanye yaliyo sawa" .   Allaah سبحانه وتعالى akasema :" Enyi mlioamini kuleni katika vitu vyema ambavyo tumekuruzukuni” Kisha akataja (kisa cha yule) mtu aliyesafiri safari ndefu, kachafuka na kajaa mavumbi na huku anayanyua mikono yake mbinguni akisema "Ewe    Mola! Ewe Mola! Nipe kadhaa, nikinge na kadhaa wakati chakula chake cha haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na kivazi chake ni cha haramu, na    anashibishwa na haramu, je, vipi atajibiwa (dua zake?)
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim