KUNA IDADI YA RAKAA – QIYAAMU LLAYL ?
Hakuna
uthibitisho unaoelezea kama sala za usiku zina idadi za rakaa maalum. Ila sunna
iliyothibiti husaliwa rakaa mbili mbili kama ilivyopokelewa na Ibnu ‘Umar
Allah awawie radhi(yeye na baba yake) kutoka kwa hadithi ya Mtume Salla Allahu
‘Alayhi Wasallam
صلاة الليل مثنى مثنى فإذا خشي أحدكم الصبح صلى ركعة واحدة توتر له ما
قد صلى
Sala za usiku (husaliwa) rakaa mbili mbili na akichelea mmoja wenu
kufikiwa na Alfajiri asali rakaa moja ambayo huwa witr aliyoisali
Bukhari na Muslim
Katika Fataawa za Ibnu Tamiyah amesema
( ومن ظنَّ أن قيام رمضان فيه عدد موقت عن النبي- صلى الله عليه وسلم-
لا يزاد
ولا ينقص منه فقد أخطأ ) فيه
الفتاوى 22/272
Mwenye kudhani kwamba sala za usiku za Ramadhaan zimeekewa idadi
maalum na Mtume Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam haizidi wala haipungui basi amekosea.
Fataawa 22/272
فقد سئلت عائشة رضي الله عنها : بكم كان رسول الله صلى الله عليه وسلم
يوتر ؟ قالت : " كان يوتر بأربع وثلاث، وست وثلاث، وعشر وثلاث، ولم يكن يوتر
بأنقص من سبع ولا بأكثر من ثلاث عشرة " رواه أبو داود وأحمد وغيرهما.
،
Aliwahi kuulizwa bibi ‘Aishah Allah amuwie radhi : “Mtume Salla
Allahu ‘Alayhi Wasallam alikuwa akisali Witr rakaa ngapi? Akasema :
Alikuwa akisali rakaa nne kisha husali tatu na akisali sita na (kisha)
tatu na kumi (kisha) na tatu na alikuwa hapunguzi chini ya rakaa saba na wala
hazidishi zaidi ya kumi na tatu