Adhw-Dhwuhaa (93)


سُورَةُ  الضُّحى
Adhw-Dhwuhaa (93)

(Imeteremka Makka)

 Sura hii imeanza kwa viapo viwili vyenye kueleza nyakati mbili za uchangamfu na za kutulia, ya kwamba kwa hakika Mwenyezi Mungu hakumwacha Mtume wake wala hakumchukia, na kwamba aliyo mtengenezea katika Akhera makao ya juu ni bora zaidi kuliko alio mkirimu duniani. Kisha Subhanahu akaapa kwamba Yeye atampa mpaka aridhike, na yaliyo tangulia ni ushahidi wa yatakayo kuja. Kwani alikuwa yatima, akampatia makaazi; alikuwa amepotea akampa bora ya uwongofu, na alikuwa fakiri akamtajirisha. Kisha Aya zikataka aangaliwe vyema yatima, na asikemewe mwenye kuomba au kuuliza,  na zisimuliwe neema za Mwenyezi Mungu.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَالضُّحَىٰ ﴿١﴾

1. Naapa kwa mchana.

وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ ﴿٢﴾

2. Na (Naapa kwa) usiku unapotanda (na kutulia).

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ ﴿٣﴾

3. Rabb (Mola) wako Hakukutelekeza na wala Hakukuchukia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

وَلَلْآخِرَةُ خَيْرٌ لَّكَ مِنَ الْأُولَىٰ ﴿٤﴾

4. Na bila shaka (uhai wa) Aakhirah ni bora kwako kuliko (uhai) wa awali.

وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰ ﴿٥﴾

5. Na bila shaka Rabb (Mola) wako Atakupa (mpaka) utaridhika.

أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَىٰ ﴿٦﴾

6. Je, kwani Hakukukuta yatima, Akakupa makazi?

وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَىٰ ﴿٧﴾

7. Na Akakukuta umepotea, Akakuhidi?

وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَىٰ ﴿٨﴾

8. Na Akakukuta mhitaji, Akakutosheleza (ukakinaika na kuridhika)?

فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ ﴿٩﴾

9. Kwa hivyo basi yatima usimkandamize..

وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ ﴿١٠﴾

10. Na muulizaji usimkaripie.

وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ ﴿١١﴾

11. Lakini neema ya Rabb (Mola) wako ihadithie.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com