028 - Hadiyth Ya 28: Kuvumiliana Tabia Mbaya Katika Maisha Ya Ndoa Kwa Kukumbuka Tabia Zilizo Nzuri



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لاَ يَفْرَكْ مُؤْمِنٌ مُؤْمِنَةً إِنْ كَرِهَ مِنْهَا خُلُقًا رَضِيَ مِنْهَا آخَرَ))  مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muumin [mume] asimchukie Muumin [mke]. Asipompendelea kwa tabia fulani ataridhika naye kwa tabia nyingine)).[1]
 
 
Mafunzo Na Hidaaya:
 
  1. Hakuna binaadamu aliyekamilika kwa tabia njema tupu. Kila mwanaadamu ana kasoro zake; aina moja au nyingine.
 
  1. Kuishi pamoja kunadhihirishiana aina za tabia baina ya watu.
 
  1. Inapasa kuvumiliana katika maisha ya ndoa, kwani kila mmoja ni mtihani kwa mwenziwe.
 
 
وَجَعَلْنَا بَعْضَكُمْ لِبَعْضٍ فِتْنَةً أَتَصْبِرُونَ ۗ
Na Tumejaalia baadhi yenu nyinyi kwa nyinyi kuwa ni majaribio (mtihani) je mtavumilia? [2]
 
 
  1. Uislamu unamsisitiza mume kumfanyia wema mke. [An-Nisaa 4: 19].
 
  1. Hadiyth hii ni suluhisho mojawapo la kutatua matatizo baina ya mume na mkewe. [An-Nisaa 5: 128].
 
  1. Inasisitizwa Muislamu kuchagua mke mwema, kwani ndio sababu ya furaha yake duniani na Aakhirah.
 
  1. Hii Hadiyth inamtaka mume awe makini wala asichukue hatua za haraka ambazo zinaweza kuvunja nyumba.
 



[1]  Muslim.
[2]  Al-Furqaan (25: 20).